Teknocrat
JF-Expert Member
- Oct 20, 2018
- 3,807
- 8,424
Habari Wana Jamvi,
Katika pita pita za kuchambua, kudadisi, kufuatilia, kuchunguza na kuperuzi baadhi ya mambo yanayo endelea kwa maslahi ya taifa letu, mara baada ya report ya CAG kutoka na baadhi ya raia kuhoji kuhusu hatima ya project ambazo aliacha Marehemu Magufuli.
Raia tumefumbuliwa macho na CAG (Japo kuna baadhi yetu tulikua macho kibishi bishi kweli, hata kipindi Marehemu alipojaribu kutumwagia pilipili na upupu machoni ili tuyafumbe, na aliona haitoshi akaamua kututoboa macho kabisa tusione).
Nimekutana na hii issue ya project ya bomba la mafuta, ambayo nimeileta kama hoja binafsi mbele ya "BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA JAMIIFORUMS" ijadiliwe. Mheshimiwa Speaker, naomba muongozo niwakilishe hoja;
Nirudi kwenye mada husika,
Hivi karibuni, mara baada ya Rais Mama Samia kuapishwa tu, siku ya pili alifanya ziara ya kikazi kwenda nchini Uganda kufuatilia makubaliano yaliofikiwa na Rais Museven pamoja na Marehemu Magufuli.
Project hio ambayo inategemewa kuwa ndio bomba refu zaidi duniani la kusafirisha mafuta, lenye thamani ya Mabillioni Ya USD, ambalo linatarajiwa kuwa na;
1) Bomba Zenye Unene Wa 24" (Insulated 24 Inch Pipeline).
2) Ujazo Wa 216,000 Bopd (Design Capacity).
3) Bomba Refu Kuliko Yote Duniani Ya Kusafirisha Mafuta Kwa Kuyachemsha (Longest Trace Heated Pipeline In The World).
4) Mafuta Ghafi Mpaka Yenye Nyuzi Joto 45°C (45°C PP).
5) Vituo 16 Vya Usimamizi Na Plant 1 Ya Kukoat Mafuta Ghafi (16 Camps & 1 Coating Plant).
6) Vituo 6 Vya Kusukuma Mafuta (6 Pump Stations PS).
7) Vituo 2 Vya Kupunguza Presha (2 Reduction Pressure Stations PRS).
8) Generator Za Kisasa Katika Kituo PS 3 & PS 5 Na Terminal.
9) Marine Storage & Export Terminal.
Swala la mkataba wa makubaliano wa hio project ya bomba la mafuta liliwekwa wazi na Rais Magufuli alipo mkaribisha chato Rais Museven mnamo mwaka jana, na aliliongelea kabla ya umauti kumfika mwaka huu.
Tanzania iliingia makubaliano na Uganda ya ujenzi wa bomba hilo lenye thamani ya Mabillioni mara baada ya kuipiga chini Kenya (Ambayo awali ndio ilianza majadiliano na Uganda).
Rais Magufuli alisema "Tanzania ndio nchi itakayo faidika zaidi na bomba hilo kwa asilimia 70%" pindi alipomkaribisha Rais Museven chato, jambo ambalo raia waliamini na kufurahishwa sana nchi nzima. Raia kwenye hii project walijua hakika tumepiga bingo haijawahi kutokea katika taifa letu (70% si mchezo).
Binafsi, nlishtuka na mahesabu hayakuingia akilini, yaani Tanzania ipate 70%, halafu 30% Uganda na Kampuni Ya Total wagawane. Ila sikuwa jinsi ila kuamini kwasababu mikataba haikuwekwa wazi.
Hivi karibuni, report zimeanza kuwekwa wazi na wahusika wa project hio (Ikiwemo kampuni kubwa ya Mafuta Duniani TOTAL) mara baada ya Rais Samia kufanya ziaya ya kikazi nchini Uganda na kukamilisha sambamba na kumalizia kazi alioianza Rais aliemtangulia.
Mataifa ya wenzetu HAYANA USIRI pamoja na kuwa na UWAZI kwenye mambo yenye maslahi ya kitaifa na makampuni yao. Tofauti na hapa kwetu.
REPORT; Tanzania itapata 5% (Sio 70% kama Magufuli alivyosema na kuwaaminisha Raia), Ugands itapata 15%, wakati CNOON Ltd itapata 8%, na 72% zitachukuliwa na kampuni nguli kutoka nchini France ya TOTAL.
View attachment 1762911
HOJA YANGU;
Sio Tanzania kupewa asilimia chache (5%) katika hio project, hapana, hata tungepewa 2% isingekuwa tatizo. ila point ni "KWANINI VIONGOZI WALITUMIA UONGO KUWAAMINISHA WANANCHI".
Hii sio mara ya kwanza viongozi wa nchi kudanganya raia, ilitokea kwenye;
1) Swala la ATCL kuwaaminisha watanzania kwamba shirika linafanya kazi kwa "FAIDA" kupelekea hata kuipa serikali gawio la faida.
2) Swala la Corona, raia walidanganywa na kuaminishwa kwamba hakuna Corona nchini, ila watu wengi walipoteza maisha kwa Corona (Mpaka baadhi ya Viongozi Wa Vyama Vya Upinzani na Maproffesor Wa Ngazi Za Juu).
3) Swala la kuaminisha watanzania kwamba hakuna ufisadi na upotevu wa hela za wanyonge katika serikali ya awamu ya 5. Ila report ya CAG imetoa hati mbaya kwa baadhi ya wizara kwasababu ya matumizi makubwa ya pesa za watanzania (Wizara nyingine kutumia hela zaidi ya budget walizowekewa).
KUDOS.............Soma uelewe wewe mdudu. Sio unakimbilia kubweka bweka hovyo kama una kichaa cha mbwa (distemper).
Nenda kwenye thread za Diamond Platnumz mkabishane kama amenunua ndege au amenunua kipeperushi hicho, huku hapakufai kijana.
Mzee wenu alikua ana laana ya uongo.