Kumekucha Tanzania: Barrick na Serikali ya Tanzania waunda Kampuni ya Madini

Pascal habari njema 84% kwa 16% ?!. Wasomi wazalendo wako wapi nchi ?!

..walisema tuko ktk VITA YA KIUCHUMI na majizi ya Accacia / Barrick.

..sasa tunaambiwa matokeo ya vita hiyo ni Barrick kupata 84% ya hisa na Tz kupata 16%.

..Nashangazwa na wanaoshangilia matokeo haya na kuona kuna ushindi.
 
Chief mbinguni

"....Hatahivyo, makubaliano ya mwisho ya umiliki na namna ya uendeshaji wa Kampuni ya Twiga na migodi yake mitatu bado haijawekwa wazi na Mamlaka za Serikali au Barrick wenyewe. "

Yawezekana, makubaliano ya mwisho ya wanahisa yakawa tofauti ni hiyo 84:16 unayoitukana


Serikali kuwa na 16% kwenye hiyo kampuni maana yake serikali haitakuwa na nguvu wala sauti katika maamuzi ; maamuzi ya mwisho hutolewa na mwenye majority shareholding tusidanganyike!! Serikali ikikubali utaratibu huo bado tutakuwa tunaibiwa kama zamani hatutakuwa tumefanya lolote la maana!
 
84/16 what is that shit?? And you call that mapambano..... Nia ya kuendeleza sekta ya madini my ass!!!!!


Halafu Pascal Mayalla anasema economic benefits will be split 50/50 how? Whatever you refer to as economic benefits will have to be split according to the shareholding structure [84/16] ,huo ndio utaratibu wa corporate governance!

Msidanganyike hapa tumelaliwa kwasababu wawakilishi wetu ni vilaza!!! Ndio hao hao walimdanganya JIWE kwa kumpa figures za uwongo mpaka akatuahidi kila mmoja wetu kuwa tutanunuliwa NOAH mpaka Leo hatujaona hata IST!!!!
 
Ukisikia "mwano" katikati ya usiku mzito ujue kuna jambo kubwa na nyeti. Sharti uamuke pamoja na Wanazengo

Katika kile kinachotajwa na wafuatiliaji wa sekta ya madini Nchini Tanzania kuwa na mwendelezo chanya za Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dr. John Pombe Magufuli kunufanika ipasavyo na sekta ya Madini, hatimaye kampuni ya Madini ya Barrick Gold ya Canada na Serikali ya Tanzania wameanzisha kampuni mpya ya Madini itakayokuwa ya ubia yaani joint venture company.

Kampuni hiyo mpya [TWIGA MINERALS CORPORATION LTD] tayari imesajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inachukua uendeshaji na mali zote za iliyokuwa kampuni ya Madini ya ACACIA.

Kampuni hiyo ya Madini ya Twiga ambayo makao yake makuu yatakuwa mkoani Mwanza, itaendesha migodi ya dhahabu ya Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara.

Kwa mujibu ya makubaliano ya awali kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania, umiliki wa kampuni hiyo ulitarajiwa kuwa 84% kwa Barrick na 16% kwa Tanzania. Hatahivyo, makubaliano ya mwisho ya umiliki na namna ya uendeshaji wa Kampuni ya Twiga na migodi yake mitatu bado haijawekwa wazi na Mamlaka za Serikali au Barrick wenyewe.

Juhudi hizi za Serikali ya Dr. Magufuli katika kufikia makubaliano haya yanafungua ukurasa mpya wenye matumaini kwa manufaa ya Nchi ya Tanzania kunufaika na rasilimali za madini mbalimbali.

Pia, yanaongeza chachu kwa Serikali kuendelea kujadiliana na Makampuni mengine ya Madini ikiwemo TanzaniteOne Mining Ltd (TML) ili Serikali ya Tanzania inufainike zaidi na Madini kwa ustawi wa Taifa na vizazi vyetu na vinavyokuja.

Katika hatua nyingine, wachambuzi na wafuatiliaji wa Sekta ya Madini katika Bara la Afrika wameipongeza Serikali ya Tanzania chini ya Rais wake Dr. Magufuli kwa kusimama imara dhidi ya mikataba ya madini isiyonufaisha bara la Afrika na hivyo kuhakikisha Afrika inapiga hatua chanya kuelekea maendeleo ya watu wake.
Mnatuchanganya jamani! Vipi kuhusu zile trillions zetu!
Serikali yetu sikivu inaungana na hayo majizi tena?
 
..walisema tuko ktk VITA YA KIUCHUMI na majizi ya Accacia / Barrick.

..sasa tunaambiwa matokeo ya vita hiyo ni Barrick kupata 84% ya hisa na Tz kupata 16%.

..Nashangazwa na wanaoshangilia matokeo haya na kuona kuna ushindi.
Ni majuzi tu Mkapa alikuwa akipingwa kuhusu mikataba hii mibovu ya madini. Lakini hawa wanaoshangilia leo pia walimshangilia vile vile, na kuwaita wenye maoni tofauti "wavivu wa kufikiri".

Leo hii rasilimali yetu, nchi yetu tunashangilia kuambulia 16% ?!. WaTanganyika tumerogwa sehemu si bure. Kama mazuzu vile aliyoyaona Mwl 1967 Mungu amrehemu.
 
Back
Top Bottom