Kumekucha Tanzania: Barrick na Serikali ya Tanzania waunda Kampuni ya Madini

mapinduzi daima

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
1,725
2,698
Ukisikia "mwano" katikati ya usiku mzito ujue kuna jambo kubwa na nyeti. Sharti uamuke pamoja na Wanazengo

Katika kile kinachotajwa na wafuatiliaji wa sekta ya madini Nchini Tanzania kuwa na mwendelezo chanya za Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dr. John Pombe Magufuli kunufanika ipasavyo na sekta ya Madini, hatimaye kampuni ya Madini ya Barrick Gold ya Canada na Serikali ya Tanzania wameanzisha kampuni mpya ya Madini itakayokuwa ya ubia yaani joint venture company.

Kampuni hiyo mpya [TWIGA MINERALS CORPORATION LTD] tayari imesajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inachukua uendeshaji na mali zote za iliyokuwa kampuni ya Madini ya ACACIA.

Kampuni hiyo ya Madini ya Twiga ambayo makao yake makuu yatakuwa mkoani Mwanza, itaendesha migodi ya dhahabu ya Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara.

Kwa mujibu ya makubaliano ya awali kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania, umiliki wa kampuni hiyo ulitarajiwa kuwa 84% kwa Barrick na 16% kwa Tanzania. Hatahivyo, makubaliano ya mwisho ya umiliki na namna ya uendeshaji wa Kampuni ya Twiga na migodi yake mitatu bado haijawekwa wazi na Mamlaka za Serikali au Barrick wenyewe.

Juhudi hizi za Serikali ya Dr. Magufuli katika kufikia makubaliano haya yanafungua ukurasa mpya wenye matumaini kwa manufaa ya Nchi ya Tanzania kunufaika na rasilimali za madini mbalimbali.

Pia, yanaongeza chachu kwa Serikali kuendelea kujadiliana na Makampuni mengine ya Madini ikiwemo TanzaniteOne Mining Ltd (TML) ili Serikali ya Tanzania inufainike zaidi na Madini kwa ustawi wa Taifa na vizazi vyetu na vinavyokuja.

Katika hatua nyingine, wachambuzi na wafuatiliaji wa Sekta ya Madini katika Bara la Afrika wameipongeza Serikali ya Tanzania chini ya Rais wake Dr. Magufuli kwa kusimama imara dhidi ya mikataba ya madini isiyonufaisha bara la Afrika na hivyo kuhakikisha Afrika inapiga hatua chanya kuelekea maendeleo ya watu wake.
 
Bange mbichi. Umiliki wa 84% per 16%? Halafu mtaanza mapambio yenu ya kipumbavu. Hatudanganyiki. Nyambafuuuuu

Chief mbinguni

"....Hatahivyo, makubaliano ya mwisho ya umiliki na namna ya uendeshaji wa Kampuni ya Twiga na migodi yake mitatu bado haijawekwa wazi na Mamlaka za Serikali au Barrick wenyewe. "

Yawezekana, makubaliano ya mwisho ya wanahisa yakawa tofauti ni hiyo 84:16 unayoitukana
 
Serikali tayari ilishajitoa kwenye masuala ya kufanya biashara NA kuruhusu soko huria, yenyewe ibaki ktk kukusanya kodi tu.Nashangaa KWA sasa Serikali hiyo hiyo inarudi tena Kuna kufanya biashara kupitia mlango WA nyuma.
 
Chief mbinguni

"....Hatahivyo, makubaliano ya mwisho ya umiliki na namna ya uendeshaji wa Kampuni ya Twiga na migodi yake mitatu bado haijawekwa wazi na Mamlaka za Serikali au Barrick wenyewe. "

Yawezekana, makubaliano ya mwisho ya wanahisa yakawa tofauti ni hiyo 84:16 unayoitukana
Sasa hizo hisa zinatofauti na huu mrahaba tunaopata?
 
Serikali tayari ilishajitoa kwenye masuala ya kufanya biashara NA kuruhusu soko huria, yenyewe ibaki ktk kukusanya kodi tu.Nashangaa KWA sasa Serikali hiyo hiyo inarudi tena Kuna kufanya biashara kupitia mlango WA nyuma.
Comrade, kiuhalisia kuna sekta nyeti kwa Nchi ikiwemo raslimali mfano Madini, Serikali LAZIMA iwe na mkono wake ndani ili kuhakikisha manufaa yanapatikana.

Hata katika Nchi za dunia ya kwanza, kuna maeneo Serikali zina mikono yao kwa umiliki wa HISA
 
Ivi barrick pekee ndio kampuni inayochimba madini tanzania hakuna makampuni mengine?

bado tunaibiwa pakubwa sana.
 
Back
Top Bottom