Kumekucha: Siri ya chaguzi za 2000 na 2005 kuwekwa hadharani na polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumekucha: Siri ya chaguzi za 2000 na 2005 kuwekwa hadharani na polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ochu, Sep 22, 2008.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Askari kulipua siri ya uchaguzi Z’bar

  na Mwandishi Wetu, Zanzibar


  SAKATA la kukwama mafao ya askari wastaafu wa vikozi vya SMZ, limechukua sura mpya, baada ya baadhi yao kutishia kufichua siri ya jinsi walivyotumika katika uchaguzi mkuu wa 2000 na 2005 Zanzibar.

  Wakizungumza na Tanzania Daima jana, askari hao walisema wanatoa wiki mbili, mapandekezo ya mafao yao mapya, yawe yamezingatiwa na Wizara ya Fedha na Uchumi Zanzibar, vinginevyo watamwaga siri hiyo.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti, askari hao walisema kwa kuwa sheria iliyotumika kuandaa viwango vipya vya mafao yao ilipitishwa na Baraza la Wawakilishi na kusainiwa na Rais wa Zanzibar, hakuna chombo kingine chenye uwezo wa kupinga maamuzi hayo.

  Walisema Wizara ya Fedha na Uchumi, ilipaswa kugundua kasoro zinazojitokeza kabla ya muswada wa sheria kuwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi na kusainiwa na Rais wa Zanzibar, kama sheria.

  Askari hao walisema wanashangazwa na mapendekezo hayo kuzuiliwa wakati miongoni mwa wajumbe wa tume hiyo ni watendaji wakuu Serikalini.

  “Hapa kinachoonekana hawathamini mchango wetu, tumetumika sana kwenye uchaguzi na tunajua mambo mengi, hiki ni choyo cha watendaji wa Wizara ya Fedha”, alisema afisa mmoja mstaafu ambaye alifikia cheo cha juu katika kikosi cha KMKM.

  Walisema inashangaza kuona watendaji wa Wizara ya Fedha, wamekuwa na kinyongo kulipa mafao yao wakati baadhi yao wameajiriwa hivi karibuni na wanamiliki mali nyingi, yakiwemo majumba na magari.

  Walisema hivi sasa taratibu zimeshakamilika za kuzungumza na mwanasheria atakayesimamia kesi yao mahakamani.

  Wiki iliyopita, Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Hassan Haji Wambi, alisema mapendekezo ya mafao ya askari hao wastaafu yamekwama baada ya kutokea mgongano wa kisheria kati ya Sheria ya Tume ya Uajiri namba 7 ya mwaka 2007 na sheria ya fedha ya mwaka 2005.

  Alisema sheria ya Wizara ya Fedha, inalazimisha kuwepo mashauriano kabla ya viwango vipya vya mafao kupangwa, ili kuepusha kuathiri bajeti kuu ya Serikali.

  Alisema kutokana na hali hiyo serikali imeamua kuwalipa askari wote viwango vya zamani, wakati suala hilo likiendelea kutafutiwa ufumbuzi na mamlaka husika.

  Mafao ya askari hao wastaafu yamerekebishwa na kuongezwa kwa zaidi ya asilimia 50 ya viwango walivyokuwa wakipata zamani, lakini walilazimika kulipwa kwa viwango vya zamani baada ya kujitokeza hali hiyo.

  Askari wa vikosi vya SMZ wamekuwa wakitajwa katika ripoti mbali mbali za uchaguzi kuwa ni miongoni mwa wanaoshiriki katika uchaguzi na kusababisha malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa.


  SOURCE: tANZANIA dAIMA
   
 2. D

  Darwin JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Walimsaidia mwizi kwahio na wao ni wezi.
  Wangekua mashujaa wangetaja hizo siri pale pale baaada ya uchaguzi kwa manufaa ya wazanzibari na sio sasa.

  Hakuna jipya hapa

  Waliutumia uaskari wao kwa manufaa yao wakati ule sasa wameona serikali hio hio haiwajali ndio wanasema wana siri.

  Mzalendo wa kweli ni yule anayejali nchi yake bila kupewa hata ndururu.
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kinyesi kilichokauka kimepata umande mwingi mpaka kimerudi kuwa rojo, nacho chaanza kutoa harufu!

  Mwaka huu tutasikia mengi!
   
 4. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Siri hiyo tunaijua,ni jinsi walivyofanikisha wizi wa kura.Lakini tunasemaaa,kila mwizi ana arobaini yake.
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Sep 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  zanzibar ni mali yetu binafsi tumeinunua ile toka kwa karume sasa sijui ni siri gani ambazo hazijulikani wakati ni mali yetu binafsi
   
 6. S

  Stone Town Senior Member

  #6
  Sep 22, 2008
  Joined: May 28, 2007
  Messages: 108
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asalamu Alaykum.

  Hakuna jambo lolote ambalo ni siri kila kitu kinafahamika askari wa vikosi ambavyo amiziri jeshi wao ni rais wa zanzibar amani abeid karume walitumika kupga kura zaidi ya mara moja, pia walitumika kuwasimamia wapiga kura kutoka mashamba na kuja mijini na kuwakingia kifua walipoona wasimamizi wa chaguzi kuanza kuingia khofu juu ya watu wasiofahamika ambao walikuja katika vituo vya kupigia vilivyopo mjini wao walikuwa wakisimama mbele na nyuma kuwalinda hadi line refu ilipomalizika na pia jengine walikuwa ni miongoni mwa wachapaji viboko kwa wanachama wa vyama vya upinzani.

  Sasa wanataka kumwaga siri gani zaidi ya hizo ambzo hazijulikani maana hawana jipya wao wameshiriki kikamilifu katika kumpatia ushindi amiri jeshi mkuu wao bwana karume na hilo kila mmoja analifahamu sio jambo jipya wala sio jambo la siri na kama sasa hivi ndio wanashutuka na kujua kuwa walifanya makosa basi hata bado hawajashituka watashituka zaidi kutokana na makosa yao waliyowatendea watu ambao wameshashukuru maana mambo ya visiwani sio kulipiza kisasi ni kushukuru Mungu tu na laiti ingekuwa kuna mambo ya kulipizana kisasi basi pasengalikalika Tanzania hii kungekuwa na mauaji makubwa kutokana na vitendo vinavyofanywa na hawa vikosi vya SMZ dhidi ya raia wasio na hatia ambao wanaonekana wana mtazamo tofauti na chama cha CCM.

  Kikundi kinachoitwa Janjaweed ambacho kipo chini ya hifadhi ya CCM Zanzibar na ambacho kinafadhiliwa na CCM kimefanya mambo makubwa sana wakati wa uchaguzi lakini Mungu katika kuwafedhehi leo hii wanajidai wanataka kutoa siri leo tena?

  stone towner
   
 7. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,305
  Trophy Points: 280
  Wastaafu eleweni shetani hana urafiki wa kudumu na mwanadamu.... Ilikuwaje mkafanya urafiki na shetani????????
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kila muosha maiti ataoshwa .Sasa ukweli ndiyo huo .Walidhulumu haki kwa majigambo na mateso nao sasa wanapokea kile walicho wafanyia wenzao
   
 9. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Ha-ha-ha-hha-hah!
  Duh!.... Ha-ha-hah!
  .
   
 10. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Teana mie naona hao jamaa WEWEKEWE NGUMU WASIPATE HATA SENTI. Wakome!
   
 11. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #11
  Sep 23, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani watakachofanya ni kutoa ushahidi kuwadhihirishia watanzania kuwa walichokisema CUF kwa miaka yote hii ni kweli tupu.

  Hao wazee nao wakome kuchumia tumbo
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Kweli wastaafu hawathamini kabisa jamani watu wametumikia miaka 20 plus......hadi 40 yrs wengine jamani leo mnawaona kama hawafai hizii sera zenu mbovu jamani maana kama wao wanafanyiwa hivyo nasi tukija zeeka tutafanyiwa hivyo hivyo ni mbaya sana ila kwa wanasiasa 5 yrs wanalipana mil 40....ni haki kweli????inasikitisha sana maana wale wanadai haki yao walipenii
   
 13. M

  Masatu JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  "Kapu la mjanja mjenga hatii mkono"
   
Loading...