Kumekucha! Siku tatu kabla ya uchaguzi, Polisi wa Tanzania waanza kutembeza kipigo kwa Wapinzani

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Leo polisi wameumiza wafuasi na wanachama wa Chadema kwa mabomu ya machozi, kijana moja amepigwa risasi ya moto pajani, na sasa anapelekwa Bugando.

polisi-Mara1.jpg Polisi-Mara2.jpg Polisi-Mara6.jpg Polisi-Mara4.jpg Polisi-Mara3.jpg Polisi-Mara5.jpg
 
Zipo habari kuwa wanachama watatu wa chadema wamepigwa risasi na polisi leo mchana huko shirati, wakati wanampokea msafara wa mgombea ubunge wa chadema bw Owawa, wote wako hospitali ya shirati na wawili hali zao mbaya.
 
kwa nini wamepigwa risasi?
 
Hii picha ni S. Africa kwenye vurugu za kuwafukuza wageni.

Cc Moderator
Rafiki,hawa ndugu ni WaTanzania kama wewe na mimi. Huyo alolala hapo anatishirt inanembo ya twiga. Ni raia wenzetu.
Polisi na vyombo vya dola na watanzania wote,tukumbuke sisi ni taifa moja.Siasa ni namna ya kujitawala.
Wakati mwingine Hekima itumike. Mbona wafuasi wa UKAWA hawajawahi kumpiga mtu? Ninyi polisi na CCM ni amani ipi mnaihubiri ilhali ni nyie waanzishaji wa vurgu na mauaji?
 
wanahubiri amani bila haki haipo!
 
Tuma hizo picha ICC... noted..!!!

Taja mahali, muda na polisi wa mahali husika...!!!

ICC inakamata hata askari akiuua raia mmoja tu..!!!
 
Wananchi wenzangu, mawasiliano kama mnavyojua si rahisi lakini naomba tujitahidi kuzitoa taarifa kama hizi kila tunapozipata. Uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu na kila hila itatumika kuwanyima wananchi haki yao ya kumchagua wanayemtaka, Kwa kuwa fore warned ni fore armed ni juhudi zetu waanchi kuhakikisha haturuhusu hali kama hiyo itokee na kwa kuwa hatuna uwezo zaidi ya kupiga kelele, lazima tusinyamaze.

Ikitokea kwamba taarifa hii si ya kweli, nitakuwa wa kwanza kuomba radhi kwa usumbufu. Sina lengo baya, la hasha, ila nina jukumu la kuufahamisha Umma wa Watanzania wajue kinachotokea kila nikipata taarifa. Kulinda amani ni jukumu letu sote na yeyote yule ambaye lengo lake ni kuleta machafuko kwa kuwanyima wapiga kura haki yao ni vizuri tumuanike wananchi wamuone haijalishi kama ni mlinda amani mwenyewe, hii nchi ni yetu sote.
 
Back
Top Bottom