Kumekucha: Polisi wapewa siku saba kuwaomba msamaha Walemavu

Mbona mnawapiga mabom wale jamaa wa tarime walioenda "kujionea huruma" kwenye mali zao walizoambiwa na pombe kuwa acacia anawaibia?
Huko mimi sipo. Nilichojaribu kumwelewesha jamaa yangu ni kwamba, hao waliopigwa wanapaswa kujionea huruma kwenye sanduku la kura. Ukimchagua shetani basi ujue umeyakubali na mambo yake yote.
 
Haisikitishi, inafundisha. Hao hao wakipewa tisheti hurukwa akili wakadhani shetani ana rafiki. Huu mwaka acha tutandikwe mpaka akili ziturudie
Tena yule mwakilishi wao akalamba ukatibu wizara ya sheria jina nmemsahau
Baada ya kuwa mstari wa mbele kipindi cha kampeni
 
Huko mimi sipo. Nilichojaribu kumwelewesha jamaa yangu ni kwamba, hao waliopigwa wanapaswa kujionea huruma kwenye sanduku la kura. Ukimchagua shetani basi ujue umeyakubali na mambo yake yote.
Kura zipi mkuu!!
Kama ni zile za Lubuva basi itakuwa umejitoa ufahamu makusudi ili uwaongopee baadhi ya members kanakwamba una busara!!!
 
Kila aliefanyiwa udhalilshaji alipwe kiwango fulani cha fedha na wote wapatiwe simu, mbona kuna mengine yanawezekana kama la Noah?
 
Kura zipi mkuu!!
Kama ni zile za Lubuva basi itakuwa umejitoa ufahamu makusudi ili uwaongopee baadhi ya members kanakwamba una busara!!!
Nina busara na ndio maana ya kwangu (japo ilifeli kwa sababu za kijecha) niliipeleka mahali sahihi. Tangu awali nilifahamu kuwa shetani hana rafiki. Lakini hao tunaowaonea huruma leo, walikuwa wakipeperusha bendera na kujipamba na matisheti kisa tu Ya Moto Band na Diamond wametumbuiza.

Unapojitoa ufahamu kwenye sanduku la kura basi fahamu zinakurudia ukishapata marungu mawili matatu. Naamini next time hawatapita mitaani kukampenia maafa yao wenyewe
 
Au wamwambie bosi wao awape Noah zao mapema!! Hii inaweza kutuliza mambo kidogo.
 
Nina busara na ndio maana ya kwangu (japo ilifeli kwa sababu za kijecha) niliipeleka mahali sahihi. Tangu awali nilifahamu kuwa shetani hana rafiki. Lakini hao tunaowaonea huruma leo, walikuwa wakipeperusha bendera na kujipamba na matisheti kisa tu Ya Moto Band na Diamond wametumbuiza.

Unapojitoa ufahamu kwenye sanduku la kura basi fahamu zinakurudia ukishapata marungu mawili matatu. Naamini next time hawatapita mitaani kukampenia maafa yao wenyewe
Aliyemuelewa huyu anyooshe kidole tafadhali!!
 
Katikati ya kashfa ya Lugumi Jeshi la Polisi lilisifiwa kuwa ni safi kwa asilimia 99.99. Usafi huo pengine unatokana na mambo kama haya!
 
NYIE LUMUMBA UWA NI WEPESI KUSIFIA SANA MBONA HILI AMJA SIFIA TUMESHAWAZOEA KUSIFIA HADI UJINGA
 
Nina busara na ndio maana ya kwangu (japo ilifeli kwa sababu za kijecha) niliipeleka mahali sahihi. Tangu awali nilifahamu kuwa shetani hana rafiki. Lakini hao tunaowaonea huruma leo, walikuwa wakipeperusha bendera na kujipamba na matisheti kisa tu Ya Moto Band na Diamond wametumbuiza.

Unapojitoa ufahamu kwenye sanduku la kura basi fahamu zinakurudia ukishapata marungu mawili matatu. Naamini next time hawatapita mitaani kukampenia maafa yao wenyewe
Ni bora tuwape mamangi UKAWA maana kila mtu atakuwa anafanya atakacho hakuna kutii sheria wala nini, mishahara kila mtu 9000000000000000000000000000000000000000, Maandamo mpaka kwenye chumba cha ikulu ni wewe tu, ukitaka kuiba kwiba tu. Popoooooz
 
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa siku saba kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwaomba msamaha walemavu kwa udhalilishaji waliowafawanyia.

Pia wamelitaka jeshi hilo kulipa fidia ya baiskeli za walemavu 30, zilizoharibiwa kutokana na shambulizi la polisi pamoja na simu za mkononi na fedha.

Wamesema wasipofanya hivyo, watachukua hatua za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani.

Juni 16 mwaka huu, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam liliwaadhibu watu wenye ulemavu waliokuwa wakifanya maandamano ya kupinga kuzuiwa kuingia katikati ya jiji wakiwa na bajaji zao.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga alisema siku hiyo polisi walitumia nguvu iliyopitiliza na kinyume cha utaratibu kwa kufanya manyanyaso yaliyopitiliza kwa walemavu wanawake ambao walifunuliwa nguo zao na askari wa kiume.

“Jambo hili ni fedheha , udhalilishaji na linatweza utu wa mwanamke na kitendo hiki si cha kiungwana na tunakikemea vikali,”alisema.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaama jana, Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo ya Kiuchumi kwa Watu Wenye Ulemavu, David Nyendo alisema walemavu hawakufanya maandamano bali ni madereva wa bajaji walikwenda kumwona Mkurugenzi wa Manispaa wapewe sehemu maalumu ya kupaki bajaji zao.

“Ndani ya siku saba, Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi hilo, kwa namna yoyote ile litakavyoona vema lijitokeze hadharani kuwaomba msamaha watu wenye ulamavu na taifa kwa ujumla kwa kitendo cha udhalilishaji kilichotekelezwa na maafisa wake.

“Kinyume na hapo hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi ya Jeshi la Polisi.

“Pia ndani ya muda huo hu, tunaliomba jeshi hilo litoe fidia ama nafuu kwa waathirika wa shambulizi hilo ambazo ni; baiskeli za walemavu 30 ambazo ziliharibika kutokana na shambulizi la polisi,”alisema Nyendo.

Chanzo: Mtanzania
Yaani NSATO MARIJANI aje hadharani kuomba Radhi ! Itakuwa maajabu ya dunia .
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom