Kumekucha: Parliament to discuss EPA, Richmond -Speaker

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
14,971
12,323
Parliament to discuss EPA, Richmond -Speaker

2008-06-01 10:45:11
By Staff Reporter

The Speaker of the National Assembly, Samuel Sitta, said yesterday the coming budget session of the Union Parliament will discuss the External Arrears Payment Account and the Richmond power contract scandals fully.

Sitta was speaking to Managing Directors of media houses in Dar es Salaam who asked him a number of questions on a number of issues.

The budget session is the longest of all the house sessions and is due to begin early this month.

Sitta said he would be stunned if the government did not present initial reports on measures it was taking against those mentioned in the scandals.

The House made 23 recommendations to the government to work in the Richmond scam.

It also allowed a request by the government to make a thorough investigation into the EPA scandals.

The government had promised to investigate the scam within six months.

SOURCE: Sunday Observer

Comment on this article
 
Bunge kuidhibiti Serikali

2008-06-01 12:36:22
Na Mashaka Mgeta

Bunge la Muungano limejizatiti kuweka kanuni zitakazoongeza wigo katika kusimamia Serikali. Miongoni mwa kanuni hizo, ni ile inayowafanya Spika na Naibu Spika, kutokuwa na fungamano katika chama chochote cha siasa.

Hayo yalisemwa jana na Spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta, alipokuwa akizungumza na Wahariri Watendaji na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.

Alisema kanuni zilizopo sasa, zilitungwa mwaka 2004, hivyo kuzifanya zikose uwezo wa kukidhi changamoto zilizopo sasa.

Alisema, hivi sasa, Spika na Naibu Spika wanapata shinikizo kutoka vyama vya siasa, hali inayoathiri utendaji kwa mujibu wa sheria na kanuni za kibunge.

Aidha, alisema kupitia mabadiliko hayo, Bunge litaunda kamati ya Bunge ya kutunga sheria, itakayotekeleza majukumu ambayo hivi sasa yapo chini ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Alisema kamati hiyo, itatoa msaada wa kisheria katika masuala kama vile kuwasilisha muswada bungeni, inapobainika haja ya kutunga sheria itakayotumika dhidi ya mambo yanayowakera wananchi.

Bw. Sitta, alisema kamati hiyo itapitia na kupendekeza njia bora za kuboresha ama kufuta sheria kandamizi, badala ya kusubiri hatua hiyo kuchukuliwa na idara ya mahakama.

Alizitaja kamati nyingine kuwa ni ya Ukimwi inayoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Bi. Lediana Mng`ong`o na ile ya sheria ndogondogo.

Alisema miongoni mwa kazi za kamati hiyo, ni kushughulikia sheria ndogondogo, zikiwemo zinazotungwa na Mawaziri, huku zikiwa zinakinzana na sheria mama ya nchi.

Bw. Sitta, alisema sheria hizo zitakapobainika, na kuonekana zinaathiri utendaji na kusababisha ukiritimba, zitafutwa.

Alisema mabadiliko mengine yalihusu mpango wa kumuuliza Waziri Mkuu maswali ya moja kwa moja,
Pia alisema mabadiliko yatafanywa katika kamati ya Bunge ya mashirika ya umma, inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Kabwe Zitto.

Alisema mabadiliko hayo yatahusu jina, kwa vile mashiriki ya umma yanayohusika katika kamati hiyo, ni yale yenye hisa za Serikali zinazoanzia 50 na zaidi.

Bw. Sitta alisema mabadiliko hayo yataiwezesha kamati hiyo, kushughulikia mashirika mengine yenye hisa chini ya 50, zinazomilikiwa na Serikali.

Spika alisema ili kudhibiti utoro kwa baadhi ya wabunge, umeandaliwa utaratibu wa kufanya mahudhurio baada ya kukamilika kwa shughuli za Bunge.

Alisema utaratibu wa sasa unaotumika kuwaorodhesha wabunge kabla ya vikao, haukuwa na ufanisi kutokana na hila zilizofanywa na baadhi yao.

Hata hivyo, Bw. Sitta, alisema umma unapaswa kumpima kutokana na mageuzi anayoyafanya kuliwezesha Bunge kutekeleza wajibu na majukumu yake kwa maslahi ya umma.

Alisema licha ya kuwapo watu wanaohoji uadilifu wake, hawezi kubadilika katika kutekeleza azma hiyo.

``Ukichukua umri wangu na mambo niliyoyapitia, ninaamini nipo makini sana na wala siwezi kubadilika hata kidogo,`` alisema huku akionekana kujiamini.

Aidha, alisema yupo tayari kukabiliana na changamoto zinazotokana na vitendo vya baadhi ya watu wanaompinga.

``Ninaungwa mkono na wabunge, wapiga kura walionichagua katika jimbo la Urambo Mashariki, wadau wa maendeleo, Jumuiya ya Ulaya na taasisi za Marekani, hao wote si wajinga,`` alisema.

Aliongeza, ``kama wabunge wangekuwa hawaniungi mkono, hivi sasa ningekuwa nimeshatupwa nje``.

SOURCE: Nipashe
 
Kama nia ya mh Spika ni kuidhibiti serikali kisawasawa basi hiyo ni move nzuri, kuiachia serikali loopholes ambazo matokeo yake ni haya ya kuhujumu uchumi wa nchi bila watuhumiwa kuchukuliwa hatua kali ni jambo linalotukwamisha sana.
 
Haya ndiyo mambo ya kufanya na yana make sense kwangu. Mmeunda tume zimekuja na majibu na mapendekezo then you work on it. Naunga mkono hatua hizi za maendeleo.
 
Heko Mh Sita kwa hilo nakupa tano. Lakini isiwe story tu ya kuwafurahisha waandishi wa habari. Tunataka uchukue hatua na kuyashia hayo unayosema.
 
Heko Mh Sita kwa hilo nakupa tano. Lakini isiwe story tu ya kuwafurahisha waandishi wa habari. Tunataka uchukue hatua na kuyashia hayo unayosema.

Mbona watu wengine hawajadili hii issue wanasubiri ushambenga ndiyo wajadili. Hongere Mr. Zero kwa kutufahamisha hili.
 
Hata mimi naona kama kweli bunge litaamua kuidhibiti serikali basi itakuwa ni hatua kubwa mbele.

Ila na wenyewe wadhibitiwe ili wasianze kujipandishia mishahara na marupurupu.
 
Kiwira kwanza, ikisharudishwa mikononi mwa wananchi mengine yote yanakuja na yatajipa ila wananchi tutashinda tu, mafisadi wote wataangamia hakuna masamaha wala hoja, hizo hoja zimemshinda Lowassa sasa hatuwezi kuishia pale tu tunasonga mbeleee!
 
Great points!
Kumbe issue hapa ni kuirudisha Kiwira mikononi mwa wananchi sasa kwa nini hao wabunge ambao unataka kujipandisha chati kwa mgongo wa Mkapa wasipeleke issue bungeni kwa watu wanaotuwakilisha na sidhani kama inawez akuchukua dk. 20 na ushee kama bunge likiamua hivyo.
 
Kazi ya wanasiasa ni kupiga kelele majukwaani, kama vile mkapa alivyokwenda kupiga kelele kwenye jukwaa la kwao, sasa labda ni mkapa anyetaka kujipandisha chati kwa mingongo yetu wananchi, sidhani kwenye hilo kuna anyehitaji kuambiwa ona, na ni haki yetu wananchi kudai any answers toka kwa viongozi wetu wa sasa na wa zamani,

Wa kutusemea ni wabunge wetu, sio anybody else, wabunge ni lazima waweke hoja kwa public kwanza kupima kama unakubalika and then ndio iende bungeni kwa hiyo sasa tuko kwenye the right track!

Haponi mtu hapa, fisadi ni fisadi tu hata awe mkapa rais wa zamani, the good thing ni kwamba maovu yake mengi tumeambiwa na marafiki zake mwenyewe!.
 
naona tunaanza kuamka humu kitu ambacho ni kizuri ! angalau taratibu lakini tutafika. great analysis.
 
Kazi ya wanasiasa ni kupiga kelele majukwaani, kama vile mkapa alivyokwenda kupiga kelele kwenye jukwaa la kwao, sasa labda ni mkapa anyetaka kujipandisha chati kwa mingongo yetu wananchi, sidhani kwenye hilo kuna anyehitaji kuambiwa ona, na ni haki yetu wananchi kudai any answers toka kwa viongozi wetu wa sasa na wa zamani,

Wa kutusemea ni wabunge wetu, sio anybody else, wabunge ni lazima waweke hoja kwa public kwanza kupima kama unakubalika and then ndio iende bungeni kwa hiyo sasa tuko kwenye the right track!

Haponi mtu hapa, fisadi ni fisadi tu hata awe mkapa rais wa zamani, the good thing ni kwamba maovu yake mengi tumeambiwa na marafiki zake mwenyewe!.

Kama data tulizopewa humu ni za kweli. Ni sababu gani zilizowafanya hao wabunge wamkataze Mtikila kudai haki yake kwenye chombo kinachotambuliwa kisheria, mahakama? Kama sio kuwa issue itakufa bila kupalamia mkongoni.
 
Parliament to discuss EPA, Richmond -Speaker

2008-06-01 10:45:11
By Staff Reporter

Sitta said he would be stunned if the government did not present initial reports on measures it was taking against those mentioned in the scandals.

The House made 23 recommendations to the government to work in the Richmond scam.

It also allowed a request by the government to make a thorough investigation into the EPA scandals.

The government had promised to investigate the scam within six months.

SOURCE: Sunday Observer

Comment on this article

So even in the Serikali na CCM yenyewe kuna mgawanyiko Babkubwa.

I just read in Tanzania Daima kuwa Msekwa is for Wagombea Binafsi and also Sitta kind of sound leaning towards that direction. Then who within CCM and Serikali is against Wagombea Binafsi?

Will this issue end up being Kikao maalum cha CC na NEC and some people be threatened and asked to shut the hell up?

CCM kuna kazi na Kalumekenge karibu shule itamshinda!
 
hilo gazeti la mbowe likiongozwa na mbowe mwenyewe, wapo kwenye kampeni hao ! sasa wao mambo ya ccm wameyajuaje kama si unafiki huo au ndio kama vile mbowe alivyosema kwamba wapinzani wametumwa na ccm kuchezea nchi ?
 
Habari nzuri kama bunge litakuwa la mtindo huo.Waziri mkuu anauliza papo kwa papo na mengineyo.
 
Kama data tulizopewa humu ni za kweli. Ni sababu gani zilizowafanya hao wabunge wamkataze Mtikila kudai haki yake kwenye chombo kinachotambuliwa kisheria, mahakama? Kama sio kuwa issue itakufa bila kupalamia mkongoni.

Katika dataz nilisema kuwa Mtikila ametoa one condition, nayo ni kuwa iwapo hawatamburuza mkapa kwenye sheria, after a period of time yeye atamburuza,

Iwapo wabunge wamerudisha Bandari yetu wananchi watashindwa nini tena kuhusu Mkapa? Kwani yeye hajui kuwa sasa maji yako shingoni?
 
Hujajibu swali. Nimeuliza sababu za kumkataza wewe unanielezea condition. Nashangaa sana inakuwa rahisi kumpalamia Mkapa kwamba hajajibu wakati sisi wenyewe humu tuko hivyo hivyo nadhani hiyo inadhibitisha kauli yako mwenyewe uliyoitoa humu. Na hiyo bandari iliyorudishwa ni ipi tena? Kuna tofauti kati ya mamlaka na wakala sijui wewe unazungumzia nini hapa.
 
Heko Mh Sita kwa hilo nakupa tano. Lakini isiwe story tu ya kuwafurahisha waandishi wa habari. Tunataka uchukue hatua na kuyashia hayo unayosema.
naona hapo unawakweza hao waandishi wa habari... ingependeza kwa kusema kuwafurahisha wananchi na sio waandishi wa habari pekee!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom