Kumekucha: "Msiba wa Taifa" Toleo la 4..

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Jipatie nakala yako hapa chini na ukiweza unaweza kuchapisha na kuwapatia wale wasioweza kupata kwa njia ya mtandao.

kumekucha4.png
 

Attachments

  • kumekucha4.pdf
    2.4 MB · Views: 924
Ndio gazeti la kwanza kulisoma baada ya Msiba Mkubwa huu kulifika taifa. taarifa za kina ... RIP kwa wote .. na poleni wafiwa na Watanzania wote!!
 
CCM Kampeni zake kutafuta ukubwa Igunga, VODACOM kuendekeza hela zaidi na Miss Tanzania kuvutiwa zaidi na kuanika mapaja hata kwa siku za msiba mzito kama huu nchini mwetu wananchi tunasema vitendo vyenu kamwe HAVIKUBALIKI hata kidogo!!!!!!!!!!!
 
 
Kwa upande wa bara licha ya maneno mengi ya wanasiasa kuhusu ‚mikakati‛ na ‚michakato‛ mingi ya kuboresha usalama barabarani bado ajali za mabasi zim-eendelea kupukutisha wananchi wengi katika mazingira ambayo yanaonekana bado yangeweza kuepupika. Ajali za mara kwa mara za mabasi zimekuwa kama masimulizi ya kujirudia rudia huku viongozi na watendaji wakisiasa wakitoa matamko mbalimbali ya ‚kukemea‛ tabia za ‚madereva‛. Kwa miaka nenda rudi matamko hayo hayajaonekana kuzuia au hata kupunguza kwa kiasi kikubwa athari zinazotokana na ajali za barabarani.

Wikiendi hii taifa limekumbwa na simanzi kubwa kwasababu watu wengi (zaidi ya 200) wamefariki kwa wakati mmoja. Ukweli ni kuwa Ajali za barabarani zinaua wengi sana kuliko hawa waliotutoka kwa mkupuo, ila takwimu hazitunzwi sawa sawa nchini Tanzania. Nilipendekeza idara zinazohusiana na usafiri zitoe takwimu za ajali kila mwaka ili tuone tunaelekea wapi na ajali ajali ajali, kwa sababu ni suala la muda tu, hata mimi ntakuwa mmoja wa hao wanaoteketea safarini, ikiwa hatua za kweli hazitachukuliwa na wale wenye dhamana ya kuzimaliza.

Asante kwa kulifafanulia hili la ajali za barabarani na kuanisha ajali za majini. Ni Hatari sana ukiwa unasafiri Tanzania!
 
MMKJ kazi nzuri ila jaribu tena ku edit donate paypal button link kwasababu inaleta error. Wewe inaoneka sio marketer mzuri (lol) yaani link zote zinafanya kazi kasoro money link.
 
tunafaidi sisi wa mitandaoni,laiti TBC1 ingekuwa macho basi tungewapa habari hii ili waweze kuwasomea wadao wao

shukrani mkuu
 
Mlikuwa mnalalamika kuwa MEDIA in TANZANIA iko kimyaaa....well, media MOGUL kama Juma Pinto wa JAMBO LEO alikuwa huko kuwapa Support VODACOM

ANGALIZO - Huwezi kumuita Juma Pinto "Media Mogul" wakati ana gazeti moja tu la udaku wa CCM ambalo uchapaji wake unalipiwa na Rostam Aziz kutokana na makampuni kutotaka kuweka matangazo yake mle sababu ya ushabiki wa gazeti kwa CCM na hivyo gazeti kukosa hela za kujiendesha.
Media mogul ni mtu ambaye ana influence kubwa kwenye media hasa kutokana na uwekezaji mkubwa alionao kwenye sekta hiyo.
 
Jipatie nakala yako hapa chini na ukiweza unaweza kuchapisha na kuwapatia wale wasioweza kupata kwa njia ya mtandao.

View attachment 37032


Ni kawaida yetu wakuu,hapo tutapeana salamu za rambirambi,tutapeana pole,tutajenga na minara ya kumbukumbu,tutafanya uchunguzi usiokuwa na tija nk,nasima uchunguzi usiokuwa na tija kwa maana kwamba hii si ajali ya kwanza...kwa mwezi huu tu Tanzania inaweza kuwa imepoteza watu wasiopungua 1000 kwa ajali...tena hizi ni zile ambazo tunapata taarifa zake.....kama kawaida viongozi wetu wanatoa salamu za rambirambi kwa wafiwa na kuwapa pole majeruhi...Najiuliza maswali mengi sana na sipati majibu exactly what happens in Tanzania currently...ni kama kuna laana inakula taifa hili na sisi hatuna habari.....Baada ya kuzama meli ya MV Bukoba serikali ilisema itafanya campaingn safisha usafiri wa majini...ni kweli kwa kipindi cha miezi michache meli na boti kadhaa zilifungiwa kufanya biashara...lakini kama kawaida ya Watanzania baada ya kusahau yale machungu tukarudi kulekule...boti na meli zimechoka,zina kutu na zinabeba watu zaidi ya uwezo wake ambacho ndio inasemekana ni chanzo cha hii ajali ya Zenji...Unaweza kuwalaumu wasafiri kwamba kwanini walikubali kupanda meli ambayo tayari ina mzigo mkubwa..jibu ni wazi NI UMASKINI WA WATANZANIA usafiri wa taabu,ukikosa meli moja unatakiwa usubiri siku mbili au tatu,kwanini watu wasijazane?

MAONI YANGU:
Serikali iiache siasa kwenye uhai wa watanzania,SUMATRA kazi yao ni kukusanya faini tu za watu bila kutimiza wajibu wao..vyanzo vya ajali za barabarani na majini mara nyingi ni mwendo kasi,ubovu wa hivyo vyombo,kubeba mizigo kupita kawaida...........serikali tuchukue hatua,tume zinaundwa na sitashangaa kama hii ajali tume ikiundwa,lakini JE? Tunafanyia kazi maoni ya hizo tume? TUACHE SIASA KWENYE UHAI WA WATANZANIA JAMANI...!!!!
 
Wewe mange idd pili si ulikuwa muhimbili wadi ya watoto wagonjwa ukijifanya una huruma kweli,vpi umeweka msiba wa kitaifa kwenye blogu yako wakati unajirusha huku,,is this counting the blessing???!!tatizo la watu kama nyie ni kujionyesha but in reality sio wazalendo wa ukweli. Mnatafuta umaarufu tuuu deeply you all fake.....
 
Asante kwa kijarida, pole sana kwa wote waliofikwa na msiba mkuu! Mungu azilaze roho zao mahala pema peponi...Amen!
 
Inasikitisha sana nikikumbuka ilivyokuwa kwenye MV Bukoba mwaka 1996 ni tofauti kabisa na Mv Spice ya 2011 sijafahamu mpaka sasa wale wa MV Bukoba walikuwa ni binaadamu na hawa wa Mv Spice walikuwa ni wanyama!
 
Back
Top Bottom