Kumekucha: Mawakili wa Mbowe waweka pingamizi kesi ya Ugaidi

Weka picha nyingine. Hii moja haitoshi.

A105075F-F7F1-4CDA-8C1C-7943E556BB59.jpeg
 
Hakuna Kesi hapo ni kufunika upuuzi wa walkia JUMONG tu , mtu hana substance haonekani kama nchi anaiongoza yeye, kiukweli tumepigwa pale tena pakubwa sana, Rais Hajawahi kutoa statement ya maana hata moja , maagizo anatoa watu hawafuati na bado anajichekesha tu eti MImi Rais ila Umbo la Kike , THubutuuuuuuu Sirro anakuangalia tu na timu yake na wala huna la kumfanya, tatizo aliambiwa tangu mwanzo ondoa takataka zooote za Mwendazake weka watunwako wanaokutii, hakusikia ndio madhara yake haya , apambane na hali yake
 
Mawakili wa Gaidi tayari wameona ngoma nzito hivyo wameanza kukata tamaa mapema, nia yao aibu za mbowe zisiwekwe hadharani hivyo wanatamani afutiwe tu kesi, isisikilizwe.
 
Mawakili wa Freeman Mbowe ambaye ni Mwamba wa siasa za Tanzania, anayeshitakiwa na serikali ya Tanzania kwa makosa ya Ugaidi wa thamani ya hela za madafu shilingi laki 6, Wameiwekea pingamizi kesi hiyo kwa madai kwamba Mahakama ya Uhujumu uchumi na Rushwa, ambako kesi hiyo imepelekwa haina uwezo wa kusikiliza kesi ya Ugaidi.

Mahakama imepokea pingamizi hilo na inatarajia kulitolea uamuzi kesho saa 3 asubuhi.

Mungu ibariki Chadema

View attachment 1918046

=========

Mahakama kutoa uamuzi pingamizi la Mbowe na wenzake​

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kesho Jumatano Septemba 1, 2021 itaamua pingamizi la Mbowe na wenzake kama mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza kesi yao ama la.

Mbowe na wenzake wameipinga mahakama hiyo kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao kwa mashtaka ya ugaidi na kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia Ugaidi kesi yao inapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu ya kawaida na si hiyo ambayo ni Divisheni Maalum.

Serikali imepinga hoja hizo ikidai kuwa kwa mujibu wa marekebisho ya sheria mbalimbali namba 3 ya Mwaka 2016 makosa yaliyoko kwenye Sheria ya Ugaidi yaliwekwa kwenye Sheria ya Uhujumu Uchumi na kwamba kwa hali hiyo mahakama hiyo ya ufisadi ina mamlaka ya kusikiliza mashtaka yao.

Jaji Elinazer Luvanda baada ya kusikiliza hoja za pande zote ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano asubuhi atakapotoa uamuzi.

Chanzo: Mwananchi
Unajiaibisha sana. Wapi duniani ulishasikia ugaidi unasemwa ni wa thamani fulani?. Ugaidi unaelezwa kwa madhara yake na siyo thamani yake. Shame on you
 
Erythrocyte ,

..Ni kweli inachanganya Mbowe kushtakiwa kwa tuhuma za ugaidi ktk mahakama ya uhujumu uchumi.

..unadhani kwanini mawakili wa serikali wamefanya hivyo?

..Pia nini faida ya mawakili wa Mbowe kuweka pingamizi?

..Mimi nilidhani wangeiacha mahakama na mawakili wa serikali wachafuke kwa kuendesha kesi ktk mahakama isiyo na mamlaka ya kuendesha kesi husika.

Cc Petro E. Mselewa
 
Unajiaibisha sana. Wapi duniani ulichasikia ugaidi unasemwa ni wa thamani fulani?. Ugaidi unaelezwa kwa madhara yake na siyo thamani yake. Shame on you
Labda kama unamtukana Sirro aliyeleta hicho kiwango
 
Erythrocyte ,

..Ni kweli inachanganya Mbowe kushtakiwa kwa tuhuma za ugaidi ktk mahakama ya uhujumu uchumi...
Mawakili wa serikali wao ni Mbumbumbu siku zote , Lissu kishasema haya miaka na miaka , kuhusu akina Kibatala kuweka pingamizi hilo , hii ni muhimu sana, kwa vile ikiwa tunataka haki basi ni vema mchakato wa kuipata haki yenyewe upite kwenye njia sahihi
 
Back
Top Bottom