Kumekucha! Magurudumu yaanza kung'oka kwenye gari la JK

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Ninavyofahamu mimi, gazeti la kila wiki la Changamoto linamilikiwa na shushushu mmoja wa ngazi ya juu mstaafu (jina nafunika kwanza kwa sababu hawa huwa hawastaafu) hivyo habri zinazoandikwa humo kuhusu ya ndani ya serikali ya JK huwa yana ukweli kwa takriban asilimia 100.

Isitoshe gazeti hili lilikuwa ni anti-upinzani katika kipindi cha kampeni mwaka jana.

Leo hii katika stori yake kubwa ‘Maswahiba wamuasi Rais Kikwete’ linaeleza jinsi rafiki zake wa karibu wanavyomuasi, hali ambayo itamuweka pagumu katika kipindi chake cha pili cha utawala ambacho ndiyo amekianza tu.

Pamoja na mambo mengine, gazeti limesema kwamba hata katika vurugu za Arusha, kuna mkono wa baadhi ya maswahiba hao wa JK.

Swali: Hii si ndiyo dalili inayoonyesha kwamba magurudumu yaanza kunyofoka katika gari la JK?
 
Yaani natabiri tutayapata yale waliyoyapata majirani zetu kenya....lazima yatatokea kama tu mambo yataendelea kua hivi!
 
Ndio vizuri mpaka atie adabu,teh teh teh...sasa kila mtu na lwake,makamba kasema hivi,msekwa malecela wanasema vingine;ngeleja kaja na hili,sitta analeta lile,full mkorogo...mkulu mwenyewe aanh kimya kama b*e*ge kudadadeek!
 
inawezekana kuna ukweli maana hata magazeti ya FISADI PAPA naona yanaandika tofauti na hapo mwanzo
 
bado nchi nzima itamgeuka

Magurudumu yalianza kunyofoka tangu wakati wa uteuzi wa wagombea katika CCM. Huyu mjamaa anachekesha saaaana!

Hivi sasa serikali yake haina umoja, mawaziri na viongozi wake wakuu kila mmoja yuko kivyake -- wanapingana katika kauli zao kuhusu masuala makuu ya kitaifa!

Hawezi hata kuwaambia: "Jamani tuwe na msimamo mmoja katika masuala haya."

Hawezi, badala yake anakenua meno tu.
 
Jk hana cha kupoteza, hategemei kugombea tena kiti cha uraisi. lakini historia inatuambia awamu ya pili siku zote ni yakukusanya kilicho bakia ili kuongezea pension yake. Hao wabaya wake imekula kwao
 
Ninavyofahamu mimi, gazeti la kila wiki la Changamoto linamilikiwa na shushushu mmoja wa ngazi ya juu mstaafu (jina nafunika kwanza kwa sababu hawa huwa hawastaafu) hivyo habri zinazoandikwa humo kuhusu ya ndani ya serikali ya JK huwa yana ukweli kwa takriban asilimia 100.

Isitoshe gazeti hili lilikuwa ni anti-upinzani katika kipindi cha kampeni mwaka jana.

Leo hii katika stori yake kubwa ‘Maswahiba wamuasi Rais Kikwete' linaeleza jinsi rafiki zake wa karibu wanavyomuasi, hali ambayo itamuweka pagumu katika kipindi chake cha pili cha utawala ambacho ndiyo amekianza tu.

Pamoja na mambo mengine, gazeti limesema kwamba hata katika vurugu za Arusha, kuna mkono wa baadhi ya maswahiba hao wa JK.

Swali: Hii si ndiyo dalili inayoonyesha kwamba magurudumu yaanza kunyofoka katika gari la JK?

Mwaka huu wameanza mapema na jinsi JK alivyo na visasi na alivyo wa kukurupuka hadi 2015 tutasikia mengi na kuona mengi.

Adui muuombee njaa
 
Ni dalili mbaya kwa uongozi wake, Kila kukicha maandamano tutaona mengi mwaka huu. Tuiombee nchi yetu mambo yasije yakafika pabaya jamani.
 
-Katiba inamkosesha usingizi,

-Mauaji aliyofanya Arusha yanamtesa,

-Vyuo vikuu ndio kwanza vimepamba moto,

-Mafisadi wanamshinikiza afumbe mdomo,

-Balali ndio huyo imejulikana wazi kuwa yuko hai,

-Mawaziri wake wanahoji kauli zake na kupishana kimitizamo,

-ahadi zake zinazokaribia thamani ya bil.100 hazitekelezeki,

-Nchi ipo gizani, uzalishaji viwandani unashuka,

-Inflation inazidi kila kukicha,

-Kauli za maaskofu zinamnyima hata kusogelea hafla zao, tumbo moto!


Total confusion...ni wa kumhurumia!...Akina Rizwani na Salma walimsukumiza
kwenye madaraka na kumsaidia kuchakachua, sasa hivi wamemwacha achanganye na zake!

Pole weee!...
 
Familia ishaandaliwa makazi maalum katika nchi moja ya Ki-Arabu. Prof Mutharika kusaidia kufaulisha uondokaji wake. Ndio maana katembelewa mara mbili ndani ya wiki mbili hapo nyuma kidogo.

Makamu wa rais na mtaalam wa NUCLEAR naye kwa sasa yuko kwenye kukamilisha kazi nyeti mno huko mbugani Serengeti. Sio matairi tu kunyofoka bali na sentabolti nayo iko pabaya kupita kiasi.
 
Hii nchi anaye tusumbua ni mmoja tu mpaka sasa ni Lowasasa ..... na bado Bwana huyu ana amini atakuja kuwa raisi wa nchi hii one day.
 
Jk hana cha kupoteza, hategemei kugombea tena kiti cha uraisi. lakini historia inatuambia awamu ya pili siku zote ni yakukusanya kilicho bakia ili kuongezea pension yake. Hao wabaya wake imekula kwao

Anacho cha kupoteza sana kuliko wewe na mimi kama ulikua hujui.

Marais wenzake wamestaafia hapa hapa nchi na tunapishana nao mitaani kila kukicha bila shida yoyote sasa yeye kwa damu hizi za Watanzania wenzetu, atastaafia wapi kama si mtindo wa SAMUEL DOE?

Uliwahi kuona wapi mtu umuibie chake tena umgeuze litaaira na mwisho kuanza kuwaua hadharani baada ya kutoshiba na yale mauaji ya gizani?
 
Kinachomtesa JK ni kimoja tu -- anajuta kwa nini alijishirikisha na mafisadi kuwania urais. Angweza kuupata urais bila ya hao kwani alikuwa ni kipenzi kikubwa cha wananchi tangu jaribio lake la 1995.

Angewaambia kama mnanipenda -- basi kaeni mbali nami. Hakufanya hivyo, akawakumbatia jumla jumla -- a la 'line, hook and sinker' -- kama wasemavyo wenzetu.

Sasa hivi anaona hata haya kuwatazama machoni mafisadi waliojiingiza na kumuweka. Anaogopa, yeye anajua, na wao wanajua, kwamba akienda kinyume cha matakwa yao (kama vile kutolipa Dowans) watamlipua, kwani mtu kama RA ana ushahidi wa kimaandishi ya kumzamisha JK moja kwa moja. Muirani huyo hawezi kujiamini kiasi hicho bila ya kuwa na 'kitu' mbaya kimaandishi cha kuhusu JK.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom