Kumekucha: Maalim Seif amuomba CAG kufanya Ukaguzi Maalum kwa fedha za ruzuku ya CUF alizolipwa Lipumba na bodi yake feki

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,441
215,227
Hebu msikilize hapa

MAHAKAMA KUU YAIFUTA BODI FEKI YA WADHAMINI YA LIPUMBA ILIYOSAJILIWA NA RITA KWA SHINIKIZO LA MSAJILI JAJI MUTUNGI:

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)
OFFICE OF THE SECRETARY GENERAL


MAELEZO YA KATIBU MKUU WA CUF, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI, LEO TAREHE 18/2/2019 ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA OFISI YA WABUNGE WA CUF MAGOMENI, DAR ES SALAAM;

THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi) kimepokea kwa furaha uamuzi wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Masjala Kuu ya Dar es Salaam) chini ya Mheshimiwa Jaji Benhajj Masoud uliotolewa leo hii kuhusiana na Shauri Na. 13/2017 lililofunguliwa na Mbunge wetu, Mhe. Ally Saleh dhidi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Registration, Insolvency and Trusteeship Agency - RITA) na Wadaiwa wengine 17 ambapo kimsingi imetoa Tamko la Kisheria (Declaratory Decree) kwamba RITA haikufuata taratibu katika kusajili wale waliodaiwa kuwa ni Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CUF waliosajiliwa na RITA tarehe 12 Juni, 2017 ambao waliwasilishwa na Prof. Ibrahim Lipumba na Magdalena Sakaya na kudhaminiwa na Msajili wa vyama vya siasa.

Uamuzi wa Mahakama Kuu chini ya Mheshimiwa Jaji Benhajj Masoud kueleza kwamba RITA haikuzingatia matakwa ya kifungu cha 17 cha Sheria ya Muunganisho wa Wadhamini (Trustees Incorporation Act – Cap 318 RE 2002) umekata mzizi wa fitina kuhusiana na madai yetu tuliyokuwa tukiyasema tokea awali kwamba RITA haikuwa sahihi kusajili watu waliopitishwa na kikundi kilichojiita Baraza Kuu la Uongozi la Taifa bila ya kujiridhisha iwapo kweli kikundi hicho kilikuwa ni Baraza Kuu halali la Uongozi la Taifa la CUF.
Mahakama Kuu imetamka wazi kwamba mbali ya kwamba ni masharti ya kifugu cha 17 cha Sheria ya Muunganisho wa Wadhamini (Trustees Incorporation Act – Cap 318 RE 2002) kwamba RITA inapaswa isimamie (monitor) kikao kinachopitisha Wadhamini wa taasisi yoyote lakini kwa mazingira ya CUF ambapo kuna kambi mbili zinazokinzana, walipaswa kujiridhisha zaidi kuhusu uhalali wa chombo kilichopitisha Wadhamini . Kwa ufupi Mahakama Kuu imetamka kuifuta rasmi Bodi feki ya Lipumba na kikundi chake na kuitanabahisha RITA kwamba ifanye kazi zake kwa kuzingatia sheria.

CUF tumezingatia pia maelezo aliyotoa Jaji Benhajj Masoud kwamba pamoja na kutotakiwa kujielekeza kuhusu hadhi (status) ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya CUF lakini kupitia ushahidi uliotolewa alielewa kwamba muda wa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini waliokuwepo kabla ya tarehe 12 Juni, 2017 ulikuwa haujamalizika na kwamba unamalizika mwaka huu wa 2019.

Kufuatia uamuzi huu wa leo wa Mahakama Kuu, CUF tunamuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum wa fedha za ruzuku (ambazo ni fedha za walipa kodi wa Tanzania) zilizotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kwa Lipumba na genge lake kupitia Bodi yao feki ya Wadhamini katika kipindi chote ambacho Msajili huyo na RITA waliipa uhalali Bodi hiyo wakitambua kwamba haikuwa halali.
Kwa hatua ya sasa itoshe kusema haya kuhusiana na uamuzi huo. Maelezo zaidi yatataolewa katika siku zinazofuata.
Nikiwa Katibu Mkuu wa CUF napenda kumpongeza kwa namna ya pekee Mhe. Ally Saleh (Mbunge wa Malindi – CUF) kwa kuchukua hatua ya kufungua shauri hili ambalo limeondosha utata uliokuwepo kuhusu Bodi ya Wadhamini ya Chama chetu. Mhe. Ally Saleh amekifanyia Chama kazi kubwa sana na ya kuheshimika na kuthaminika. Tunamwambia Ahsante sana.

Pia tunawashukuru kwa dhati Timu ya Mawakili wetu waliosimamia Shauri hili ambao ni Mhe. Mpare Kaba Mpoki, Mhe. Fatma Amani Karume, Mhe. Juma Nassoro Dovutwa, Mhe. Daimu Halfani, na Mhe. Loveness Denis kwa uweledi, umahiri na umakini mkubwa waliouonesha hadi kufikia mafanikio haya.

Shukrani nyengine zimwendee Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Chama chetu, Mhe. Joran Bashange, kwa kujitolea kwa nguvu zake zote kusimamia bila ya kuchoka shauri hili na mashauri mengine yaliyofunguliwa na Chama. Tunawashukuru pia mashahidi wote waliosimama upande wa Chama kutoa ushahidi katika shauri hili. Kwa wote hao tunawaambia

Ahsante sana.

Napenda pia kuwapongeza sana wanachama wa CUF kwa uamuzi huu muhimu wa leo. Kwa niaba ya viongozi wenzangu nawataka waendelee kuwa watulivu wakisubiri uamuzi wa Shauri Na. 23/2016 ambao utatolewa siku ya Ijumaa ya tarehe 22 Februari, 2019.

Nilisema tokea awali kwamba tutaheshimu uamuzi wowote utakaotolewa na Mahakama na kwamba tumejiandaa kwa maamuzi yoyote. Bado tunasimamia msimamo wetu huo.

HAKI SAWA KWA WOTE


SEIF SHARIF HAMAD
KATIBU MKUU – CUF

Imetolewa leo tarehe 18 Februari, 2019
 

Attachments

  • Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad ameitaka ofisi ya Mdhibiti na Mkagu ( 422 X 750 ).mp4
    3.6 MB · Views: 38
Ni Tanzania tu, labda kuwe na muujiza lakini Bosi wa RITA na JAJI Mutungi walitakiwa wajiuzuru wao wenyewe au wafyekelewe mbali. "Maendeleo hayana Chama" Ha Ha Ha LoL. Kuna watu hupenda kuwafanya watanzania wenzao wapumbavu. Bado yule wa mhimili dhaifu nae aibu itamkumba kuhusu haya ya CUF.
 
Ni Tanzania tu, labda kuwe na muujiza lakini Bosi wa RITA na JAJI Mutungi walitakiwa wajiuzuru wao wenyewe au wafyekelewe mbali. "Maendeleo hayana Chama" Ha Ha Ha LoL. Kuna watu hupenda kuwafanya watanzania wenzao wapumbavu. Bado yule wa mhimili dhaifu nae aibu itamkumba kuhusu haya ya CUF.
wabunge wa viti maalum wa ndugai na Lipumba wajiandae
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom