Kumekucha! Ili kwenda sawa na TRA wenye nyumba za kupanga TZ waja na kali ya mwaka!

Mmh sijui kama wao wamiliki wa nyumba wanaweza kukurupuka na bei zao tuu.. lakin poa kuna chama ambacho kinatetea walaji... pia hali ilivyo sasa kama kuna mwenyenyumba kawaza kupandisha bei imekula kwake... bora nikajenge ya udongo kuliko hzo mambo... lakin wadau kila mwenye kipato na alipe kodi... TRA ninaamini ni watu wenye weledi hawezi kuweka kodi ili kumuumiza mwananchi...
 
Baada ya sisi Watanzania kuwa na Viherehere huku tukijifanya kila mara kuwalaumu wenye Nyumba nchini Tanzania kuwa huwa wanapandisha Kodi za pango kiholela na tukataka sifa hadi kuwashtakia wenye nyumba au wamiliki hao wa nyumba kwa Waziri wa Ardhi ambaye nae pia alilifikisha hili kwa TRA ambao na wao kama kawaida yao wakakurupuka kutoa maamuzi ya kutaka kuja na Bei elekezi huku wakitarajia kuanza kuwatoza Kodi wenye Nyumba wote nchini Tanzania sasa kibao kimegeuka.

Muda mfupi tu uliopita nimetoka kumdukua mmoja wa Wajumbe mwandamizi kabisa wa Chama cha Wenye Nyumba nchini Tanzania ambapo niliweza kumtega mawili matatu na yeye akaingia pale nilipopataka na akatiririka mambo ambayo kiukweli hata Mimi Mpangaji mwenzenu nilishikwa na butwaa na hadi hivi naandika huu uzi naona maluweluwe tupu!

Ni kwamba Umoja wa Wenye Nyumba za Kupanga nchini Tanzania muda wowote kuanzia sasa na nadhani maamuzi yao haya watayatoa Mapema mwezi ujao ( January 2017 ) katika kile wanachosema ni " mwendo wa kwenda sawa na TRA " sasa na Wao wameamua kufanya mabadiliko yafutayo ya Utozaji wa Kodi ya Pango ambayo yanaweza kuanza mwakani ambapo sasa Mpangaji hatokuwa anatajiwa bei nzima ya Chumba au Nyumba na kuanzia sasa utaratibu wao wa kututoza sisi Wapangaji utakuwa kama ufuatao:

  1. Ukitaka kukodi Nyumba nzima ( Kubwa ) kwa mfano huko nyuma ilikuwa labda ni Tsh 600,000/ kwa mwezi sasa kwa mabadiliko yao mapya ni kwamba kuanzia mwakani hutotozwa hiyo Tsh 600,000/ na badala yake utaanza kupigiwa Hesabu ya kuanzia Chumbani, Jikoni, Sebuleni, Chooni na Bafuni, Kibarazani, Store na hadi katika Parking yard yako. Hapo wanamaanisha kuwa kila eneo litakuwa na tozo yake hivyo tusishangae kuambia tozo ya Jikoni ikawa Tsh 75,000/, Sebuleni Tsh 50,000/, Chumbani Tsh 150,000/, Chooni na Bafuni Tsh 200,000/ kutokana na UNYETI wake, Kibarazani Tsh 50,000/, Store Tsh 75,000/ na Parking yard Tsh 100,000/ ambapo jumla yake hapo utapata ni Tsh 700,000/.
  2. Ukitaka kupangisha Chumba lakini Self Contained ( ambao wengi Wetu ndiyo tupo humu ) ni kwamba sasa badala ya sisi kutozwa kati ya Tsh 150,000/ hadi Tsh 300,000/ kwa mwezi mambo yatageuka ambapo sasa na sisi tutatozwa Bei ya Chumba peke yake, Sebule peke yake, Bafu na Choo peke yake na jikoni ambapo kwa mujibu ya huyu Mjumbe alisema kuwa Gharama haitakuwa kama hiyo tuliyoizoea na tusishangae Kodi yetu sasa ikawa ni kati ya Tsh 275,000/ hadi 450,000/.
  3. Kwa wale Masela wenzangu tunaopanga Kijichumba tu kimoja na ambao wengi wetu tunatozwa kati ya Tsh 30,000/ hadi 40,000/ kwa mabadiliko haya mapya wanayotaka kuja nayo wenye nyumba za Kupanga kwa mujibu wa huyu Mjumbe mwandamizi ni kwamba sasa Kodi yetu ya Pango itakuwa kati ya Tsh 50,000/ hadi Tsh 70,000/.
Mwisho nitoe tu Rai kwa Watanzania wenzangu tuache kimbelembele na kukurupuka kwani nina uhakika kama kweli haya Mabadiliko yataridhiwa Wengi wetu tutakuwa tunatandika Magodoro yetu barabarani na kulala huku tukipigia miswaki yetu katika Mitaro ya City na tukijazana katika Vyoo vya Jiji kujisaidia na kuoga.

Niwaombe pia TRA kuwa kama ni kweli kuwa nanyi mna mpango wa Kuwatoza Kodi wenye Nyumba za Kupanga tafadhali achaneni na huo mpango wenu kwani nina uhakika kuwa mkifanya hivyo na hawa wenye Nyumba za Kupanga na wao watatukomoa kwa kututoza Kodi ya Pango kama nilivyoielezea hapo juu na hatimaye Watanzania tutaishi katika maisha magumu sana na tutasekea mno.

Naomba kuwasilisha.
Mkuu hicho kitu hakipo wasiitishe serikali lazima walipe kodi,Nikiwa kama mfanyakazi mbona sisi tunalipa kodi?
Kwanza naiomba serikali itunge sheria ambayo kodi ilipwe kwa kila mwezi,iweje umlipe mwenye nyumba miezi 6/12 wakati mimi nalipwa kwa mwezi,Nenda kwa jirani hapo Kenya tu,kodi ni kila mwezi
 
Ilikuwepo sheria ya bei elekezi ya kodi ya pango...Rent Restriction Act, ikafutwa kwa kupitwa na wakati..
Sasa mnairudisha kimya kimya kwa matamko..
 
We hakuna kitu hicho kwani kutakuwa na bei elekezi ya serikali mpaka hivi sasa wenye nyumba bado bei zao ziko juu hawalipi kodi wana pandisaha hovyo pango kisa kupanda kwa maisha bila kuzingatia kipato chenyewe kwa sasa

Acha walipe kodi wasikutishe kupandisha kodi kwani wao pia wananjaa wanafikia hadi kuchukua pango kabla ya mwezi husika tena walipe kabisa ........
 
But sina uhakika, hivi viwango vya kulipa kodi si vinaanzia Tsh +180,000/=? Sasa kama kwa mfano nimekupangisha kwa Tsh 50,000 labda tuvymba 3 then nitakua naingiza Tsh 150,000/= hapo si ni tax free!? Au mi ndio sijaelewa!?
Kosa kubwa Tanzania linalopeleke kukosa kodi katika eneo hili ni kutokupima ardhi na kibaya hata waliopima wanaishia kunyang'anywa! Unamtoza mtu kodi ambaye si maji, barabara wala huduma nyingine zinafika kwake!
 
Mkuu sometimes jaribu kujiheshimu basi hiki nilichokiandika hapa kama uzi wangu ndicho kilichojadiliwa katika moja ya Vikao vya Chama cha Wenye Nyumba za Kupanga nchini Tanzania na hiyo kitu nimeidukua kwa Mjumbe wao Mwandamizi mmoja ( ambaye sitoweza kumtaja jina ) sasa Wewe kama unadhani kila mara GENTAMYCINE anafanya Ukomedi humu JF utakuwa unakosea. Ulitakiwa unipongeze kwa jitihada zangu za kufanya udukuzi na kuja na hii taarifa muhimu kwa wengi wetu wenye maisha ya kati ambayo kimsingi ni magumu inavyotuhusu na kutuchanganya ila kwakuwa Wewe bado unaishi kwa Shemeji na kula yako inategemea uwajibikaji wa kutukuka wa Dada yako akiwa Chumbani Kitandani na Shemeji yako usiku huwezi kuwa na machungu kama tuliyonayo sisi Wasaka Nyoka. Umenikera sana Mkuu!

Ninakuhakikishia kuwa huyo mwenye nyumba uliye mdukua alikua amepagawa tu. Mfuate baada ya wiki tatu umkumbushie story hii...aki ya Nani tena atakuruka.
 
Eeeh mkome vimbelembele hujui Mtu hela ya Kujenga aliopataje mpaka akajenga unakuja kupangishwa wewe kutwa mdomo....mi Naona sawa Tu watu wachajiwe Kwa sehemu
 
Back
Top Bottom