GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Baada ya sisi Watanzania kuwa na Viherehere huku tukijifanya kila mara kuwalaumu wenye Nyumba nchini Tanzania kuwa huwa wanapandisha Kodi za pango kiholela na tukataka sifa hadi kuwashtakia wenye nyumba au wamiliki hao wa nyumba kwa Waziri wa Ardhi ambaye nae pia alilifikisha hili kwa TRA ambao na wao kama kawaida yao wakakurupuka kutoa maamuzi ya kutaka kuja na Bei elekezi huku wakitarajia kuanza kuwatoza Kodi wenye Nyumba wote nchini Tanzania sasa kibao kimegeuka.
Muda mfupi tu uliopita nimetoka kumdukua mmoja wa Wajumbe mwandamizi kabisa wa Chama cha Wenye Nyumba nchini Tanzania ambapo niliweza kumtega mawili matatu na yeye akaingia pale nilipopataka na akatiririka mambo ambayo kiukweli hata Mimi Mpangaji mwenzenu nilishikwa na butwaa na hadi hivi naandika huu uzi naona maluweluwe tupu!
Ni kwamba Umoja wa Wenye Nyumba za Kupanga nchini Tanzania muda wowote kuanzia sasa na nadhani maamuzi yao haya watayatoa Mapema mwezi ujao ( January 2017 ) katika kile wanachosema ni " mwendo wa kwenda sawa na TRA " sasa na Wao wameamua kufanya mabadiliko yafutayo ya Utozaji wa Kodi ya Pango ambayo yanaweza kuanza mwakani ambapo sasa Mpangaji hatokuwa anatajiwa bei nzima ya Chumba au Nyumba na kuanzia sasa utaratibu wao wa kututoza sisi Wapangaji utakuwa kama ufuatao:
Niwaombe pia TRA kuwa kama ni kweli kuwa nanyi mna mpango wa Kuwatoza Kodi wenye Nyumba za Kupanga tafadhali achaneni na huo mpango wenu kwani nina uhakika kuwa mkifanya hivyo na hawa wenye Nyumba za Kupanga na wao watatukomoa kwa kututoza Kodi ya Pango kama nilivyoielezea hapo juu na hatimaye Watanzania tutaishi katika maisha magumu sana na tutasekea mno.
Naomba kuwasilisha.

- Ukitaka kukodi Nyumba nzima ( Kubwa ) kwa mfano huko nyuma ilikuwa labda ni Tsh 600,000/ kwa mwezi sasa kwa mabadiliko yao mapya ni kwamba kuanzia mwakani hutotozwa hiyo Tsh 600,000/ na badala yake utaanza kupigiwa Hesabu ya kuanzia Chumbani, Jikoni, Sebuleni, Chooni na Bafuni, Kibarazani, Store na hadi katika Parking yard yako. Hapo wanamaanisha kuwa kila eneo litakuwa na tozo yake hivyo tusishangae kuambia tozo ya Jikoni ikawa Tsh 75,000/, Sebuleni Tsh 50,000/, Chumbani Tsh 150,000/, Chooni na Bafuni Tsh 200,000/ kutokana na UNYETI wake, Kibarazani Tsh 50,000/, Store Tsh 75,000/ na Parking yard Tsh 100,000/ ambapo jumla yake hapo utapata ni Tsh 700,000/.
- Ukitaka kupangisha Chumba lakini Self Contained ( ambao wengi Wetu ndiyo tupo humu ) ni kwamba sasa badala ya sisi kutozwa kati ya Tsh 150,000/ hadi Tsh 300,000/ kwa mwezi mambo yatageuka ambapo sasa na sisi tutatozwa Bei ya Chumba peke yake, Sebule peke yake, Bafu na Choo peke yake na jikoni ambapo kwa mujibu ya huyu Mjumbe alisema kuwa Gharama haitakuwa kama hiyo tuliyoizoea na tusishangae Kodi yetu sasa ikawa ni kati ya Tsh 275,000/ hadi 450,000/.
- Kwa wale Masela wenzangu tunaopanga Kijichumba tu kimoja na ambao wengi wetu tunatozwa kati ya Tsh 30,000/ hadi 40,000/ kwa mabadiliko haya mapya wanayotaka kuja nayo wenye nyumba za Kupanga kwa mujibu wa huyu Mjumbe mwandamizi ni kwamba sasa Kodi yetu ya Pango itakuwa kati ya Tsh 50,000/ hadi Tsh 70,000/.