Kumekucha!! CCM yapora madaraka ya vyombo vya sheria -- yaanza kusafisha mafisadi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumekucha!! CCM yapora madaraka ya vyombo vya sheria -- yaanza kusafisha mafisadi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Apr 30, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wajumbe wenzangu JF:


  Hivi kweli CCM wataweza kumaliza ufisadi hapa nchini? Inakuwaje tuhuma za ufisadi zachunguzwa na kumalizwa na vikao vya CCM badala ya vyombo rasmi vya sheria?
  Someni hii:  *************  CCM yamsafisha kada wake kwa ufisadi

  Na Debora Sanja, Dodoma

  KAMATI ya watu watatu iliyoundwa kuchunguza tuhuma za ufisadi zilizomkabili Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Kapteni John Barongo imebaini kutokuwepo kwa ufisadi wowote uliofanywa na katibu huyo.

  Akisoma taarifa ya kamati hiyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma William Kusila alisema kamati imeshamaliza kazi yake na kuwa hakuna ufisadi.

  Kwa mujibu wa Kusila, kamati hiyo iliyoundwa kuchunguza tuhuma hizo wajumbe wake walikuwa ni Haidery Gulamali, Peter Mavunde na Wales Lusingu ambao wote ni wajumbe wa kamati ya siasa ya Chama ya Mkoa.

  Alisema kamati hiyo ilipewa muda wa wiki mbili kukamilisha kazi yake na kutoa taarifa yake kwa kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa.

  "Kamati imebaini kuwa madai hayo yaliyotolewa na katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Dodoma Donald Mejetii hayana ukweli wote kwa kuwa hakuna wizi wa fedha uliofanywa na Katibu"

  Kutokana na taarifa hiyo ya kamati uongozi wa ngazi ya juu kimkoa inafanya taratibu ili kikao maalumu cha kamati ya siasa kiweze kuona adhabu ya kuumpa Mejitii." alisema Barongo.

  Awali katika tuhuma alizozitoa Mejetii alidai katibu huyo wa Mkoa amekula fedha za mradi wa ujenzi wa Jengo la Hosteli ya chama zaidi ya sh. milioni 373.

  Pamoja na tuhuma hizo pia alidai katibu Barongo alikodisha gari ya Chama kwa Manispaa ya Dodoma ili liweze kusambaza mitihani ya darasa la saba mwaka jana kwa gharama ya sh, milioni tisa na kula fedha hizo.

  Aidha, alidai pia jumla ya Sh milioni nne zililiwa na katibu huyo kutoka Manispaa ya Dodoma ikiwa ni fedha za matengenezo ya gari hilo kabla ya kuchukuliwa kufanya kazi hiyo.

  Kusila alisema mara baada ya kupata tuhuma hizo ndipo ilipoundwa kamati maalumu kuchunguza madai hayo.

  Mwisho.

  Chanzo: MtanzaniaA
   
 2. M

  Mkono JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nilitegemea majibu ya aina hiyo
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni chama cha wachekeshaji! Na M'kiti wao JK anakubali makada wake kujigeuza polisi na mahakama kuchunguza na kusafisha majizi!
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi CCM imebakiwa na wanachama wangapi vile????
   
 5. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Huyo anaechunguzwa ni Katibu CCM mkoa, wanaomchunguza ni wajumbe wa kamati ya siasa CCM mkoa!! Hata kwa akili ya graduate wa darasa la nne hakuwezi kuwa na fair investigation hapo.. maana wote ni wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa kama kula pesa wamekula wote!!!

  Angalau wangetafuta independent investigator angalau tungeweza sadiki.. MAGAMBA haya..
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii kitu inahusu chama hivyo ni mambo yao ya chama chao cha magamba wakiamua kifichiana siri sawa sisi hayatuhusu tunacho taka... EPA, RICHMOND, MEREMETA nk
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu umesoma issue yenyewe
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kama ni hivyo kwa nini Hosea na PCCB yake huingilia vitendo vya ufisadi katika michakato ya ndani ya CCM kutafuta wagombea wa nafasi katika chaguzi za chama chao? (Tuwache kwanza michakato ya kutafuta wagombea katika uchaguzi wa wabunge/madiwani).
   
 9. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Tunaanza kuoneshwa trailer ya movie itakayotoka baada ya siku 90 kuisha
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kumjibu kilaza huyo wa sheria. Hajui kwamba chini ya Penal Code wizi wowote ule ni wizi. Isingekuwa hivyo basi polisi hawapaswi kuingilia masuala ya mtu akiibiwa mali yake na mtu mwingine.
   
Loading...