Kumekucha CCM! ...na Bado!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumekucha CCM! ...na Bado!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jul 19, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,761
  Trophy Points: 280
  CCM wamtimua Shibuda


  *Atupiwa virago kwenye Kamati ya Siasa
  *Adai ni kundi la wanaojifanya watu wa JK


  Na Suleiman Abeid, Shinyanga

  MBUNGE wa Maswa mkoani hapa, Bw. John Shibuda, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutimuliwa kwenye kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM ya wilaya ya Maswa, akidaiwa kutokuwa mjumbe halali.

  Hali hiyo ilijitokeza jana muda mfupi kabla kikao hicho hakijaanza katika ofisi za CCM wilayani hapa, ambapo Bw. Shibuda alionekana akitoka nje ya ofisi hizo, huku akihangaika kufanya mawasiliano na viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho.

  Akizungumza na Majira baada ya kutimuliwa katika kikao hicho, Bw. Shibuda alisema kitendo hicho kilichofanywa na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo, Bw. Peter Bunyongoli na Katibu Mwenezi na Itikadi, Bw. Jeremiah Makondeko, ni cha kumdhalilisha na kumvunjia heshima ndani ya Chama.

  Bw. Shibuda alisema anavyofahamu yeye ni mjumbe halali wa Kamati hiyo ya Siasa kwa mujibu wa Katiba ya CCM Ibara ya 81(1)(f) ambayo inaonesha wazi kuwa wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na wabunge wa majimbo, wenyeviti wa halmashauri za majiji, manispaa, miji na wilaya.

  Ibara hiyo inasomeka: “Mbunge, au wabunge wanaotokana na CCM wanaowakilisha wilaya hiyo au wabunge wa aina nyingine wanaoishi katika wilaya hiyo,” ni wajumbe halali wa kamati ya siasa ya CCM wilaya.

  Bw. Shibuda alielezea kushangazwa kwake na hatua hiyo ndani ya kikao hicho, ambapo siku zote amekuwa akialikwa kuhudhuria vikao vya kamati hiyo akiwa mjumbe na kuonesha ushahidi wa baadhi ya barua za mialiko kwa vikao hivyo alizokuwa akipelekewa.

  Baadhi ya barua hizo za mialiko zilikuwa ni zenye kumbukumbu namba CCM/KS/28/46 ikiwa ni ya mwaliko wa kikao cha dharura cha Julai 16 mwaka huu; Kumbukumbu namba
  CCM/MSW/KS.15/VOL.III/47 ya Juni 28 mwaka huu na kumbukumbu namba CCM/MSW/K.50/13/3/50 ya Julai 12, mwaka huu, ikiwa ni mwaliko wa kikao ambacho alitimuliwa kwa kuelezwa kuwa si mjumbe.

  Alisema pamoja na juhudi za kumweleza Mwenyekiti wake asome Katiba vizuri, alikataa kwa kueleza kuwa toleo la Katiba chapisho la hivi karibuni halioneshi kuwa wabunge ni wajumbe wa kamati za siasa za wilaya.

  Bw. Shibuda alisema Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Wilaya hiyo na kwamba uamuzi wake ni wa mwisho na kuendelea kumtaka atoke nje ya kikao mara moja ili wao waweze kuendelea na kikao.

  “Kwa kweli nimesikitishwa sana na kitendo hiki cha kufukuzwa ndani ya kikao kama mbwa, tena mbele ya kadamnasi, sijui Mwenyekiti huyu anajivunia kitu gani, nahisi ni kile ambacho amekuwa akitamba nacho kila siku kuwa yeye ana uhusiano binafsi na Rais Jakaya Kikwete, wakati Rais alishasema hana makundi,” alidai Bw. Shibuda.

  Hata hivyo, alisema hali hiyo imeanza kumpa wasiwasi iwapo atatendewa haki atakapoamua kugombea nafasi yoyote ya uongozi ambayo inahitaji kuthibitishwa na vikao vya chama, na kusema kuwa ni wazi hawezi kutendewa haki.

  Akizungumza na Majira kwa njia ya simu, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Gustav Muba, alisema wabunge wote wa majimbo ya uchaguzi ni wajumbe halali wa kamati za siasa za wilaya.

  Bw. Muba alisema iwapo kweli viongozi wa CCM wa wilaya ya Maswa watakuwa wamemfukuza ndani ya kikao Bw. Shibuda, watakuwa wamefanya makosa, na pia aliahidi kufuatilia hali hiyo mara baada ya kupokea taarifa rasmi.

  “Wabunge wote wa majimbo kwa tiketi ya CCM ni wajumbe halali wa vikao vya kamati ya siasa ya wilaya, inawezekana viongozi wa Maswa watakuwa wameitafsiri vibaya Katiba, au kuna kosa fulani limefanyika katika uchapishaji, nitafuatilia hali hiyo, baada ya kupewa taarifa rasmi,” alieleza Bw. Muba.

  Kwa kipindi kirefu sasa, uongozi wa CCM wilayani Maswa, umekuwa na mgogoro mkubwa unaotokana na kambi wakati wa uchaguzi wa kura za maoni za uteuzi wa wagombea ubunge ndani ya chama hicho, hali ambayo inaonekana kukithiri kadri siku zinavyokwenda.

  Juzi Makamu wa Rais, Dkt. Ali Mohemmed Shein, aliwataka viongozi wa wilaya hiyo kuwa na mshikamamo wa pamoja, ili kutekeleza kikamilifu Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005, ili kulinda imani ya wananchi kwa chama hicho, lakini hata kabla hajamaliza ziara yake mkoani hapa, malumbano yameanza kujitokeza.
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...waandishi wengine bwana, kichwa cha habari na habari yenyewe wala haviwiani, au ndio kuuza magazeti?

  hovyoo!
   
 3. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mchongoma angalia joke nyingine ya Saed Kubenea, the most talked about newsman in the country today:

   
 4. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Huyu si alikuwa mgombea urais? mbona anaonekana kama asiyekuwa na nguvu ndani ya chama hata ngazi ya wilaya?

  Ama huyu alikuwa mtandao wa Sumaye na hivyo sasa mtandao wa JK wanamshughulikia?
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,806
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  Rais apata ajali

  Nikanunua gazeti ili kujua kulikoni.

  Rais wa chama cha ngumi Tanzania Emmanuel Mlundwa (aliwahi kuwa bingwa huyu wa EA kama sikosei) amepata ajali ya gari lakini hakuumia sana.

  Nilikasirika sana. Mzee Rukhsa ndiye aliyekuwa katinga Ikulu miaka hiyo.
   
 6. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ha ha aaaaaaa ha haaaaa

  This is hilarious! LOL

  E bwana unaikumbuka toka wakati wa Mwinyi?

  Pole mwanangu. Yani wanajifanya wajanja ile mbaya ma Editor.

  Ha haaaa! Hiyo kali mwanangu!
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huko ni kuanguka kwa CCM ila wakishaona mbunge amepoteza mvuto kwa wananchi na kuna hatari ya kupigwa budi utakapowadia uchaguzi basi humfanyia njama za kumdhalilisha na halafu wanaibuka na mwengine ambae atafanyiwa mapinduzi na kuekwa kwenye Ubunge.CCM ndivyo walivyo wakishakutumia wanakupiga buti huku wanakwambia utajiju >
   
 8. Wakunyuti

  Wakunyuti JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dhambi ya ufisadi inaanza kuwatafuna taratiiibu....... na bado
   
 9. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2008
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Miaka ya 1997 niligongana na Kichwa cha Gazeti moja la kila wiki kikisema
  "Mchungaji abaka Kondoo" nililikimbilia hilo gazeti nikalinunua haraka. Hofu yangu ilikuwa huyu mtumishi wa Bwana amekuwaje hadi akafanya uharamia mkubwa namna hiyo?

  Nikanunua gazeti langu nikatafuta kibaraza, pahala patulivu nijisomee bila kusumbuliwa hadi nielewe kulikoni.
  TOBA!!! Kuingia ndani kwenye habari: Kumbe mchungaji anayezungumziwa kwanye habari ni wa mifugo.
  Nilisikitika sana.

  Waandishi angalieni kwa umakini vichwa vya Habari Mnavyouza navyo magazeti.
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Huu ni ufisadi mwingine maana wanafanya makusudi ili waweze kuuza magazeti yao lakini at the same time wametumia attractive headings ili wakushawishi kununua gazeti.
  Sijui hawajatambua kuwa huu ni ufisadi pia?
   
Loading...