Uchaguzi 2020 Kumchagua Tundu Lissu kuwa Rais ni kuikabidhi Tanzania kwa Mabeberu. Tusifanye kosa twende na John Pombe Magufuli

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
7,079
2,000
(System haiwezi kukabidhi nchi) sasa kama ni hivyo kura ni za nini? Si muwaambie hao system wamkabidhi wanaemtaka?
Utaelewa muda ukifika,nani alikwambia kura yako inaamua matokeo2 ya urais?,ubunge na udiwani sawa
 
zigii

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
516
250
Utaelewa muda ukifika,nani alikwambia kura yako inaamua matokeo2 ya urais?,ubunge na udiwani sawa

Ok sasa nimekuelewa kama ni hivyo kwanini kelele na kejeli zinakuwa nyingi? Wakati mnajua system ipo badala ya kura?
 
Abul Aaliyah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
4,048
2,000
Acha uongo ww
Kwa.taarifa yako watumishi wa umma wote walikwisha ongezwa mpunga kimyakimya kitambo sana ,kalagha bhaho wewe kapuku,ndio maana huwa wapo kimya na hakuna migomo ,kadhalika wanafunzi wa vyuo vikuu kuhusiana na mikopo
 
Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
11,818
2,000
Mungu hajaisahau Tz, Kama alivyotuvusha na Magu wetu kipindi Cha corona, ataendelea kutuvusha na Magu wetu kipindi Cha uchaguzi!

Kama vile Mungu alivyomponya Lissu wetu na zile Risasi za Mashetani na Shetani Mkuu aliyeagiza Lissu auawe.
Ndivyo atakavyoilinda nchi na kuwa Salama Mikononi mwa Lissu
 
Nzwangendaba

Senior Member
Nov 9, 2019
175
250
Kwani sasa hivi hao mabeberu hawapo nchini? Hujasikia boss wako akisema mabeberu tayari wameshagawana gesi yetu ya Mtwara? Hujui Mabeberu wamekamata Migodi mingi Mikubwa hapa nchini? Je hayo yamefanywa kwa vile Lissu ni kiongozi wa nchi? Ni kweli hujui ni serikali ipi iliyoingia nayo Mikataba?

Na je vipi Mabeberu walivyotutwanga Mahela kwenye Richmond, Escrow n.k, ni Kwa vile Lissu na Chama chake ndio walikabidhiwa nchi?
 
mwanateknolojia

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
766
1,000
Mkuu sasa kama tayari alishapiga kelele kwa mabeberu na kukawa hakuna impact yoyote, Je wasiwasi wako ni nini?

Tunataka rais atakayeunganisha nchi na dunia kwa manufaa ya watanzania wote, kuna faida nyingi kwa rais kujumuika na jumuiya za kimataifa yeye mwenyewe physically na sio kuwa mangimeza wa kutuma wawakilishi kwenye kila tukio la kimataifa, kwa kisingizio cha vita ya kiuchumi.

Hapa lazma CCM ikubali Candindate wao ameshindwa na hana namna! Tumweke kando na tumpe Tundu Lissu akanyooshe mambo ili tubaki na jina moja tu la wahisani na tusiwe na majina mawili kwa mtu mmoja.

kwamba akitoa msaada tunamuita muhisani, akitukosoa tunamuita Beberu ! Hizi hoja nyingine kama ndoa za jinsia moja ni vitu vidogo sana kwa mtu mwenye focus ya maendeleo.

Kwanza takwimu za kitaifa na kidunia zinaonyesha wanawake ni wengi kuliko wanaume na vivyo hivyo wanawake wasio na ndoa pia ni wengi kuliko wenye ndoa, hivyo kama kuna wanawake wenzao wengine wengi wenye uwezo wa kuwaoa na kuwatunza si kuwaruhusu tu waoane.

Hapa kikubwa sio ndoa ya jinsia moja bali ni namna gani moyo wa mtu unakubali na kuridhia mahusiano hayo. Hili likifanyika kwanza linapunguza umaskini na makundi yasiyo na dira ya maisha! Hivyo tuache kutumia hoja mbovu kuzuia mambo makubwa!
 
Bekiri

Member
Jun 30, 2013
14
75
1. Tundu Lissu sio mtu mwenye kusema ukweli akausimamia.

Kwa kinywa chake anasema, mwaka 2007 aliandika waraka ulioitwa "list of shame" wakati huo akiwa na Dokta Slaa ukasomwa pale Mwembe Yanga.

Katika waraka ule Lowassa alitajwa kama fisadi papa (ashakum). Kwa wakati huo Lissu aliamini kuwa Lowassa ni fisadi asieweza kuvumilika. Ilipofika mwaka 2015 Lissu akashiriki kikao cha kumkabidhi Lowassa urais mtu alieaminika ni fisadi. Aghalabu, Dokta Slaa aliondoka kusimamia imani yake. Lissu akalamba matapishi yake!

Hapa ndio kusema kuwa, Lissu anaweza kusema jambo moja usiku halafu kesho akalikana kwa maslahi yake binafsi. Watanzania tunataka Rais mwenye msimamo, asie kigeugeu ambae yuko tayari kusimamia imani yake hadi mwisho. Dokta John Magufuli eneo hili amethibitisha kushinda. Msimamo wake dhidi ya korona ni ushahidi wa wazi. Tuchagulieni mtu huyu asimamie nchi hii kwa miaka mitano ijayo.

2. Tundu Lissu ni mtu muongo na msariti.

Kabla ya mwaka 2013 uhusiano kati ya Tundu Lissu na Zitto Kabwe ulikua mkubwa zaidi. Mmoja akiwa Naibu Katibu Mkuu Bara na mwingine akiwa Mwanasheria wa Chama. Wote walikua vijana wazuri wenye vission na Chama chao.

Ulipofika mwaka 2013, Zitto akautaka Uenyekiti wa Chadema, Lissu akabadilika, akamtengenezea Zitto kesi ya usariti wa Chama, akamfukuza Chama. Licha ya kuwa Lissu aliufahamu ukweli kuwa Zitto hakua na hatia isipokuwa aliponzwa na Uenyekiti lkn hakujali, akamsariti rafiki yake akaitangazia Dunia kuwa Zitto ni mtu hatari zaidi ktk siasa za upinzani. Akamchafua Zitto akanuka!

Tanzania tunamtaka Rais mwenye kusema ukweli hata kama unaumiza. Lissu alishindwa kusimamia ukweli kumtetea Zitto Kabwe kwa sababu ya maslahi yake kwa Freeman Mbowe. Huu ni udhaifu ambao mtu wa nafasi ya Urais hapaswi kuwa nao. John Magufuli eneo hili amefanikiwa sana, kwake black ni black na white ni white. Tuchagulieni tena mtu mwema huyu atufikishe 2025.

3. Lissu sio mtu mwenye kupenda Muungano.

Tangu zamani hata sasa amani ya nchi yetu imeshikiliwa na Muungano. Mwalimu Nyerere alipata kusema, tukikubali kubaguana kwa kigezo cha Uzanzibar na Ubara tukimaliza tutaanza kubaguana kwa kigezo cha Uchaga, Usukuma na Uzanaki. Alisema, dhambi ya ubaguzi haina mwisho, tunahitaji kuimarisha zaidi muungano wetu kuliko kuuvunja.

Tundu Lissu hapendi Muungano, msimamo wake na chama chake uko wazi. Amethibitisha hivyo Bungeni na ktk mahojiano mbalimbali. Tafuta mahojiano yake na Salama Jabir ktk kipindi cha Mkasi mwaka 2016. Kwa msimamo wake, hatufai kuwa Rais kwa sababu atauvunja Muungano wetu na huo ndio utakua mwanzo wa kufarakana.

Katika eneo hili la Muungano, John Magufuli na Chama chake amejipambanua wazi. Msimamo wake uko wazi kuwa atausimamia, ataulinda na kuuboresha zaidi kadili ya mahitaji na wakati. Tuchagulieni tena mtu huyu alitulize Taifa letu tuimarishe Muungano wetu kwa ajili ya umoja wetu, ushirikiano wetu na usalama wa Taifa letu.

4. Tundu Lissu si mtu Mzalendo kwa Taifa lake.

Ushahidi uko wazi kuwa Tundu Lissu sio mwaminifu na Mzalendo kwa Taifa lake. Kauli zake za kichonganishi dhidi ya Taifa lake, uhusiano wake na mataifa ya nje ni ushahidi wa wazi ktk eneo hili. Kuna wakati alitofautiana na Kiongozi wa ACT Wazalendo ktk msimamo wake wa kuisimanga nchi yake mbele ya wahisani pale aliposhauri Tanzania kunyimwa msaada kwa sababu za tofauti zetu ndani.

Kwa hoja hii Tundu Lissu anathamini zaidi mataifa ya nje kuliko Taifa lake. Hii ina maana moja kubwa kuwa anaweza kutumika wakati wowote kulihujumu Taifa lake endapo atakua na madaraka makubwa ktk nchi.
Tusimchague, hatufai ktk nafasi ya urais. Eneo hili John amedhihirisha mbele ya Dunia kuwa yeye kwake Tanzania iko mbele ya kila kitu. Hajakwenda kwao kuwapigia magoti kama Lissu, John na Tanzania, Tanzania na John. Tuchagulieni John kazi iendelee!!

5. Tundu Lissu si mtu mwenye busara na hekima.

Hekima ya mtu ipo ktk kinywa chake. Kama mtu hawezi ku-control kinywa chake hekima yake ni sifuri. Kinywa cha Lissu kinasema ulongo, kinatoa maneno ya kejeri, dhihaka na majivuno wakati wote. Lissu haheshimu mamlaka yoyote ktk nchi hii, kauli zake dhidi ya Rais wa Nchi ni ushahidi unaotesa nafsi za watu wema. Kauli zake dhidi ya Mahakama mara kwa mara na sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, ni ushahidi mwingine wa kijeuri unaoumiza nafsi za mamlaka.

Nafasi ya Urais wa nchi ni nafasi ya juu kabisa ktk nchi, ni nafasi inayopaswa kukaliwa na mtu mwenye busara na hekima za juu sana. Eneo hili John Magufuli amethibitisha pasina shaka kuwa hajambo. Mazungumzo yake na Viongozi wa dini na madhehebu, wafanya biashara na makundi mbalimbali ktk nchi ni ushahidi wa kujivunia. Tuchagulieni mtu huyu atusaidie kufika salama Ka'anani.
Nawasalimu; Kampeni za kistaarabu.com,
#MitanoTena!!
MenukaJr.
 
Sep 8, 2020
67
150

900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
3,133
2,000
Lissu hafai kuwa Rais wa nchi hii, Ubunge ndio ilikuwa level yake ya juu na ya mwisho.

Kumbukeni alikuwa kwenye matibabu huko ughaibuni mara alipopata nafuu, kazi yake ilikuwa kuzungumza mambo ya hovyo sana, kutaka nchi iwekewe vikwazo, kukubali kuruhusu ndoa za jinsia moja, pindi akiwa mtawala , na ifahamike ni kinyume na mila na desturi zetu nchini ,alifanya mambo ya fedheha sana.

Wazungu walimsikiliza wakaona huyu ni bogus kabisa, ndio maana pamoja na kelele zake na maombi yake hayakuwa na impact yoyote.

Mtaji aliobakia nao kwa sasa ni kupata kura za huruma kwa risasi zilizompata

Pia system haiwezi kukabidhi nchi kwa mtu anayetetea mapenzi ya jinsia moja na msaliti kwa taifa lake,si mnakumbuka vitisho vyake na MIGA?,yako wapi?,tumeunda kampuni ya Twiga minerals Tanzania kwa ubia ambao unalinufaisha taifa, kongole Rais Magufuli.

Namuonea huruma sana, kwa maana baada ya uchaguzi atapotea kwenye ulingo wa siasa, kiki hazitakuwepo , Bunge ndio lilikuwa linampa kiki, miaka mitano sio mchezo kukaa benchi
we ndo walewale akina jinga lao.Lisu2020 president
 
The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
6,562
2,000
Umelalamika tu.

Kama Nyerere aliongoza nchi mwl kijana 39 yrs. Na alionyesha mafanikio, Mwinyi na diploma ya ualimu lakini alitupa ruksa, Mkapa toka uandishi mpaka Rais alieacha impact . Kikwete na democracy ya Kiswahili lakini alimaliza salama. Na sasa tunae Mwl mwingine tena wa sayansi lakini hajashindwa.

Ndiyo aje ashindwe advocate msomi anayetaka nchi iongozwe kwa sheria na katiba ?!

Lissu yuko vizuri kuliko team ilioko uwanjani saa hii. Hata wewe unajua. Labda figisu tu. Na ndiyo keshasema hatamuachia Mungu . Mnalo

Hatamuachia Mungu katika sehemu anayotakiwa kuifanya yeye. Hii ni kweli...

Mungu amefanya sehemu yake tayari. Kaulinda uhai wake bàada ya maharamia hawa maCCM kutaka kuuchukua kwa risasi 38 za AK47 na SMG..

Nafasi na sehemu yake ya kutenda ameitenda na anaendelea kuitenda kwa ufasaha na ufanisi Mkubwa..

Nafasi yetu na sehemu yetu ya kutenda ni kumwezesha aimalize kazi hii kufikia hitimisho la uharamia wa CCM na Magufuli hapo trh 28/10/2020 kwa kumpigia kura za KIMBUNGA na kulinda kura zetu...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom