Umslpogaaz
Member
- Apr 14, 2008
- 94
- 56
Kwa Kinana kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa ccm, kimetudhihirishia wazi kuwa kwa sasa chama hicho kipo kwa maslahi ya nani. Ni kwa muda mrefu Watanzania wamekuwa wamekistukia chama hicho kuwa hakipo upande wao. Viongozi wake wamekuja na maneno mengi matamu ya kuwalaghai wananchi kuwa watajirekebisha, kwa mfano usemi wa kujivua gamba. Mpaka leo hivi wengi tumeona kuwa maneno hayo yote yalikuwa ni kiini macho na hakuna aliyevuliwa gamba. Ni Rostam pekee ambaye kwa hiari yake aliachia ngazi kutokana na sababu zake mwenyewe kama alivyozieleza.
Viongozi wa chama hicho wote, kuanzia ngazi za juu kabisa, wamegubikwa na kashfa mbalimbali za ufisadi, lakini hata hivyo bado wanaendelea kushika nyadhfa mbalimbali, si kwa kupenda wananchi, bali waweze kupata nafasi za kufisadi zaidi. Sio siri kuwa Kinana ameshutumiwa mara nyingi kwa kujishughulisha na mambo ya kifisadi na kihalifu. Hata hivyo, kutokana na mfumo wa ccm wa kifisadi, amechaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa chama hicho.
Waswahili wanasema, 'Mungu si Athumani'. Siku chache tu baada ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa ccm, amekumbwa tena na kashfa ya meli zake kukamatwa zikiwa zimebeba meno ya ndovu, TENA! Siku zote tunasema Mungu mkubwa! Mungu amesikia sala za wanyonge wa Tanzania kwa kuwaumbua watu hawa wanaotufisha sisi na mali asili zetu. Ametuonyesha tena hadharani kabisa, KIMATAIFA kuwa hawa watu ni maharamia na hawapaswi kuiongoza nchi hii tena.
Naongelea haya kama MTANZANIA ambaye si mwanachama wa chochote cha siasa. Nina uchungu na nchi hii jinsi inavyonajisiwa huku wote tunatazama. Labda nisingeyasema haya kwa hisia kali kama ccm isingekuwa chama kinachotawala. Lakini ubaya ni kuwa ccm ni chama ambacho kwa sasa kinatawala, na kama kinaendeshwa na majangili wa kimataifa, basi usalama wa taifa zima, wewe na mimi na watoto wetu upo hatarini.
Mwenye macho haambiwi tazama. Tumeona sote kuwa ccm ni chama cha aina gani. Tufanye hima kuwaonyesha wote, hata wale wasio na macho, au wana macho lakini wanaangalia kupitia matumbo yao, kuwa kuzidi kuichagua ccm ni kuendele kujitakia maafa. Narudia tena, tutoke kila mmoja wetu, aende kwa kila mtu wake wa karibu na kusambaza ujumbe huu.
Tanzania ina wenyewe, na wenyewe ni wananchi wa Tanzania na sio wachache waliopo ccm.