Kumchagua Kinana Katibu Mkuu kunadhihirisha CCM inasimamia maslahi ya nani!

Umslpogaaz

Member
Joined
Apr 14, 2008
Messages
94
Points
0

Umslpogaaz

Member
Joined Apr 14, 2008
94 0
Kwa Kinana kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa ccm, kimetudhihirishia wazi kuwa kwa sasa chama hicho kipo kwa maslahi ya nani. Ni kwa muda mrefu Watanzania wamekuwa wamekistukia chama hicho kuwa hakipo upande wao. Viongozi wake wamekuja na maneno mengi matamu ya kuwalaghai wananchi kuwa watajirekebisha, kwa mfano usemi wa kujivua gamba. Mpaka leo hivi wengi tumeona kuwa maneno hayo yote yalikuwa ni kiini macho na hakuna aliyevuliwa gamba. Ni Rostam pekee ambaye kwa hiari yake aliachia ngazi kutokana na sababu zake mwenyewe kama alivyozieleza.

Viongozi wa chama hicho wote, kuanzia ngazi za juu kabisa, wamegubikwa na kashfa mbalimbali za ufisadi, lakini hata hivyo bado wanaendelea kushika nyadhfa mbalimbali, si kwa kupenda wananchi, bali waweze kupata nafasi za kufisadi zaidi. Sio siri kuwa Kinana ameshutumiwa mara nyingi kwa kujishughulisha na mambo ya kifisadi na kihalifu. Hata hivyo, kutokana na mfumo wa ccm wa kifisadi, amechaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa chama hicho.

Waswahili wanasema, 'Mungu si Athumani'. Siku chache tu baada ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa ccm, amekumbwa tena na kashfa ya meli zake kukamatwa zikiwa zimebeba meno ya ndovu, TENA! Siku zote tunasema Mungu mkubwa! Mungu amesikia sala za wanyonge wa Tanzania kwa kuwaumbua watu hawa wanaotufisha sisi na mali asili zetu. Ametuonyesha tena hadharani kabisa, KIMATAIFA kuwa hawa watu ni maharamia na hawapaswi kuiongoza nchi hii tena.

Naongelea haya kama MTANZANIA ambaye si mwanachama wa chochote cha siasa. Nina uchungu na nchi hii jinsi inavyonajisiwa huku wote tunatazama. Labda nisingeyasema haya kwa hisia kali kama ccm isingekuwa chama kinachotawala. Lakini ubaya ni kuwa ccm ni chama ambacho kwa sasa kinatawala, na kama kinaendeshwa na majangili wa kimataifa, basi usalama wa taifa zima, wewe na mimi na watoto wetu upo hatarini.

Mwenye macho haambiwi tazama. Tumeona sote kuwa ccm ni chama cha aina gani. Tufanye hima kuwaonyesha wote, hata wale wasio na macho, au wana macho lakini wanaangalia kupitia matumbo yao, kuwa kuzidi kuichagua ccm ni kuendele kujitakia maafa. Narudia tena, tutoke kila mmoja wetu, aende kwa kila mtu wake wa karibu na kusambaza ujumbe huu.

Tanzania ina wenyewe, na wenyewe ni wananchi wa Tanzania na sio wachache waliopo ccm.
 

Kiwi

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2009
Messages
1,045
Points
1,500

Kiwi

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2009
1,045 1,500
Umesema kweli mkuu.
Ile dhana iliyokuwepo awali wakati CCM inaanzishwa kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi haipo tena. Ni bora hata zile alama za jembe na nyundo ziondolewe kwenye bendera ya ccm. Kumweka fisadi anayejulikana wazi kuwa katibu mkuu ni tusi kwa wakulima na wafanyakazi wa Tanzania.

Lakini tujikumbushe, ile ilikuwa CCM ya Mwalimu, siyo hii ccm ya jk. ccm imepoteza dira, inapelekwa na mkondo wa maji... mbele hakuna anguko tena bali ni kuzama kwenye miisho ya bahari!

Pengine ndiyo itakuwa salama ya watanzania walio wengi maana kwa mwendo huu tunaopelekwa na ccm hakuna tumaini.

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!
 

Savannah

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
239
Points
0

Savannah

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
239 0
Kwa bahati mbaya, waTZ walio wengi hawaoni hivyo. Usije ukashangaa CCM wakiendelea dunda baada ya 2015. Kwakweli CCM histahili kuwa madarakani.
 

Mkirindi

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2011
Messages
5,418
Points
2,000

Mkirindi

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2011
5,418 2,000
Umslpogaaz hebu tafautisha, a clearing n forwardin company and a ship owner. hivu ukipana basi la MTEI LA KWENDA AUSHA NA KWENYE BEGI UNA UNGA WA DRUGS KILO, JEE WEWE NDIYE MHALIFU, AU NI AKINA MTEI WENE HAYO MABASI NDIO WAUZA UNGA. KUROPOKA OVYO NI SUMU YA BONGO.
 
Last edited by a moderator:

PhD

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2009
Messages
3,922
Points
2,000

PhD

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2009
3,922 2,000
Ndugu zangu, huyu bwana Kinana amekuwa kwenye serikali kwa muda mrefu sana, amewahi kuwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa kipindi ambacho ujangili wa tembo katika mbuga zetu ulishamiri. kumekuwa na allegations za ndugu bwana kinana either kwa baadhi ya mali, jina lake au kampuni zake kujihusisha na ujangili wa tembo. Rejea Taarifa ya Kamati teule ya bunge iliyoundwa mwaka 1992 kuchunguza masuala ya mali asili, ujangili na vitalu ilikuwa chini ya mbunge profesa kwa sasa jina nimelisahau (Philip marmo alikuwa mjumbe katika kamati hiyo walau nakumbuka, na alhaji ndolanga alikuwa mkurugenzi wa idara ya wanyama pori) amabyo ilibainisha ushiriki wa kampuni za bwana kinana katika uuzaji wa maeneo ya loliondo na ujangili wa tembo hasa kwa yeye kutumika kama deal maker wa waarabu kupewa maeneo hayo, rejea kufutwa kazi kwa manufaa ya umma kwa yule bwana wa TANAPA/NGORONGORO aliyekataa ujenzi wa hotel ya SOPA katika eneo la hifadhi miaka ya 90( alifukuzwa na mzee mwinyi).

Tatizo kubwa naloliona sasa ni kushamiri kwa ujangili wa tembo, uhusiano wa ujangili huo na kundi la alshabab, kushamiri kwa ugaidi na fikra kuwa wasomali na raia wenye asili ya kisomali wenye madaraka mbali mbali katika nchi za afrika mashariki wanatumika kama daraja la kutakatisha fedha haramu kwa ajili ya alshababu.

Na mwisho kwa uchunguzi wa serikali ya marekani kupitia vyombo vyake kuna taarifa zikiwaainisha raia hao ambapo wapo watanzania ( kuna uwezekano mkubwa kinana yumo) wamo pia viongozi wa kenya akiwamo kiongozi mmoja katika muhimili wa bunge la kenya. Hivyo basi Taarifa hiyo ikitoka kuna uwezekano CCM kutangazwa ni kundi la kigaidi, ni suala la muda tu ila ukweli utajulikana nuda si mrefu.
 

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
4,836
Points
2,000

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
4,836 2,000
Mafisadi, wezi, majangili, majambazi, mateja, misukule, mashangingi, washirkina, popo, waasherati, wanafiki,wauwaji, bundi, amfibia (hao kwa uchache) wote wanapatikana CCM.CCM ni kichaka hatari sana kwa kiumbe hai yeyeto yule.

"I have a dream......" CCM ikitolewa madarakani na baadaye kujifia pamoja na mambo mengine itabidi ufanyike mpango Lumumba iwe makubusho. Ili angalau tujaribu kurudisha sehemu kiduchu sana ya uporaji walioifanyia Tanzania.
 

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Messages
4,023
Points
1,250

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined May 26, 2009
4,023 1,250
Si jambo la kupingwa kuwa CCM kwa sasa inahusishwa kwa ufisadi. Ni jambo ambalo si la busara kwa wakati huu ambapo chama hio kilichonekana kuwa kimejijenga upya, kuweka viongozi ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi. Kuna wanaosema kuwa si yeye aliyekamatwa na pembe hizo, lakini hata meli zake kuhusishwa na uhalifu huo ni janga kubwa. Mimi binafsi nashangaa kwa nini wanaoshabikia CCM hawalioni hilo. Kwetu sisi ambao ni wananchi wa kawaida, meli hizo kukamatwa mara ya pili na shehena za pembe ni jambo ambalo linatutia mashaka na kuthibitisha ukweli wa aina ya safu ya viongozi wa CCM. Hata hivyo ni heri tu, maana tunazidi kuonyeshwa na kuamshwa hata kama tulikuwa tumelala. Tunasubiri kwa hamu sana 2015 kukiondoa chama hicho kilichojaa majangili!

PS:

Rejea zaidi kwenye hii post: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/356329-uteuzi-wa-kinana-ccm-unaweza-hatarisha-hatma-ya-chama-hicho.html
 

PhD

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2009
Messages
3,922
Points
2,000

PhD

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2009
3,922 2,000
Ukisoma between the lines na hali tete ya alshabab na uchunguzi wa marekani kuhusu wafadhili wa kundi hilo hatari ni wazi CCM wamekosea sana kumteua KINANA mtu ambaye hadi leo hajaweza kujisafisha na tuhuma nzito za pembe za ndovu, ujangili na ufadhili wa alshababu.

Hii inaweza kuwa credit kwa vyama vya upinzani na asasi za kiraia kupata support ya marekani sasa kuiondoa CCM , kwa taarifa za ndani KINANA amehushwa sana na matukio ya loliondo, mahusiano yake na matajiri wa kiarabu NK.
 

Lambardi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Messages
10,507
Points
2,000

Lambardi

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2008
10,507 2,000
Hizi allegation mbona zinatisha sana?inabidi aje mbele ajisafishe kama kweli anaweza!kashfa hii nzito sana jamani!meno ya tembo na mzigo umekamatwa hong kong na ulisafirishwa na kampuni yake huyo bwana Kinana!
 

politiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2010
Messages
2,376
Points
1,250

politiki

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2010
2,376 1,250
Umslpogaaz hebu tafautisha, a clearing n forwardin company and a ship owner. hivu ukipana basi la MTEI LA KWENDA AUSHA NA KWENYE BEGI UNA UNGA WA DRUGS KILO, JEE WEWE NDIYE MHALIFU, AU NI AKINA MTEI WENE HAYO MABASI NDIO WAUZA UNGA. KUROPOKA OVYO NI SUMU YA BONGO.
maneno yako yangekuwa na msingi mzuri kama ingekuwa ndiye mara yake ya kwanza kuhusishwa na kashfa na nyara kumbuka kamati ya bunge ya mwaka 1992 kampuni za huyu bwana ziliusishwa na ujangili. mfano wako ni mzuri endapo tu kama ingekuwa mara yake ya kwanza anayo track record ya miaka karibu 20 ndani ya biashara hiyo. kama nchi tungekuwa na mfumo wa check and balance mtu angekuwa ameshakamatwa siku nyingi lakini ndiyo hivyo tena kesi za nyani zote wanapewa ngedele.
 

mtumishidc

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2012
Messages
511
Points
225

mtumishidc

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2012
511 225
kama rostam ni king maker, kinana ni meneja wa kampeni(chafu na safi) na ndio waliotupa rais 2005 na 2010, kinana amerudi kuja kumsimika nani(hajalishi kihalali au kiharamu)?
kama jk alisimamiwa na hawa watu wawili na akawa rais, je jk hawezi kuwa na sifa za hao wawili?(nifahamishe rafiki zako na nitazijua tabia zako!)
na kama sifa za kinana ndizo hizo zilizotajwa na Umslpogaaz na Daudi mchambuzi rais wangu na ccm yake wapo salama kiasi gani?
 
Last edited by a moderator:

Tom

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2007
Messages
472
Points
0

Tom

JF-Expert Member
Joined May 14, 2007
472 0
Umslpogaaz hebu tafautisha, a clearing n forwardin company and a ship owner. hivu ukipana basi la MTEI LA KWENDA AUSHA NA KWENYE BEGI UNA UNGA WA DRUGS KILO, JEE WEWE NDIYE MHALIFU, AU NI AKINA MTEI WENE HAYO MABASI NDIO WAUZA UNGA. KUROPOKA OVYO NI SUMU YA BONGO.
Kuna utofauti. Clearing and forwarding company ana document na ku-clear mzigo bandarini ili kuu-forward uendako. Lkn anaye book container tupu toka kwa shipper, stuff and ku-seal kabla ya CLEARING agent kukutana container lenye mzigo ndie mhalifu.

Sasa aliye book container tupu toka kwa shipper, kuli-stuff and kuli-seal ndiye pia aliyemwomba Clearing and forwarding agent asafirishe huo mzigo. Hivyo ni wazi Kinana ana maelezo ya kutoa kwa Polisi, ama aseme nani mwenye mzigo ama sivyo ni wa kwake mwenyewe. Hivi Dar Harbour si pana X-ray ya containers? hawakuona meno.
 

Forum statistics

Threads 1,344,531
Members 515,863
Posts 32,824,470
Top