Kumbukumbu za Mfanyakazi: Pale Kikwete alipowashushia neema Wafanyakazi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,090
Wakati JK anaingia madarakani mwaka 2005, Kodi ya mapato kwa mfanyakszi ilikuwa ni asilimia 18, Yaani alikuwa akikatwa asilimia 18 ya mshahara wake.
Lakini hadi kufikia mwaka 2015 serikali ya JK ilifanikiwa kuishusha kodi hiyo hadi asilimia 12 na hivyo kuleta unafuu mkubwa sana wa maisha kwa mfanyakazi.

JK alisema kwenye mei mosi ya mwaka 2015 kuwa plan mwaka huo ilikuwa ni kuishusha zaidi hadi asilimia 9. Siku hiyo JK alijoke kuwa mipango yote itawekwa sawa kisha Ujiko yaani sifa atapewa huyo rais atakeyemfuatia.

Hata hivyo leo hii mambo yamegeuka, Miaka mirano ya huyo rais mpya hakuna nafuu ya punguzo la kodi, hakuna nyongeza za mishahara, upandaji madaraja ni shida na hata ajira mpya zimekuwa ni manati.

Laiti tungekuwa na uvhaguzi huru na haki kwa kweli serikali hii ilipaswa kung'olewa madarakani.

Tujikumbushe speech ya kihistoria ya JK kwa wafanyakazi

 
na bado,mtakumbuka kuwa na akiba ya maneno,hata huyu ni swala la muda tu.
 
  • Thanks
Reactions: sab
Tuacheni masihara hali ya mtumishi wa umma Tanzania ni mbaya sana,mbaya zaidi huu ugonjwa wa covid 19 umezidi kuchagiza hii hali,hakuna mwenye nafuu.. sekta binafsi ndio usiseme! Maisha yanatutia adabu sio kawaida!

Serikali nayo ndio kama hivi kimyaa..unataka kazi fanya hutaki acha! Nani anajali? Tatizo la ajira nalo limefanya watu kufanya kazi hata sizizo na maslahi angalau tu siku ziende,kazi hakuna! Unatoka asubuhi ushahidi tu angalau uonekane una kazi lakini mwisho wa mwezi hakuna kitu.. kwenye biashara nako ndio Dah... mitaji imekata bank nao wanadai...

No wonder wanaume tunakufa mapema,halafu fikiria na kuparangana kote huku ukirudi nyumbani mwanamke hakuelewi anakuita "msanii" hawajui kama zama zimebadilika sio kila homa ni marelia!
 
Sasa ukisikia kuhusu maendeleo ya watu ndiyo haya!
Nilitegemea wataalamu wa social science waje na utafiti kuonyesha kitendo cha JK kushusha hiyo kodi kutoka 18% hadi 12% life span ya Watanzania iliongezeka kwa miaka mingapi na kiwango cha furaha cha Watanzania (Happy index) iliongezeka kwa kiwango gani?
 
Huyu mwamba alituaidi maisha bora kwa kila mtanzania watu tukawa tunamdis ooooh ooooh katoka ndio tunakumbuka kumbe yale ndio yalikuwa maisha bora kwa kila mtanzania kamanda alikuwa bora twiga ipande Ndege watu wake wale vizur saiz mpak upate buku 10 mmmmm
Alikuwa rais mpole sana, ilitupasa tuone upande mwingine wa rais mkali .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha Ankoli atunyooshe. Tulizidi kukebehi utawala wa JK kana kwamba si lolote wala chochote..!

Ankoli ashikilie hapo hapo ili akili itukae sawa.
 
Chadema mkishashiba mnaaanza porojo

Yaani wafanyakazi laki tano Ndio muiondoe Ccm madarakani

Nyie mpo laki tano Kwahiyo msiwe wabnafsi Watanzania wanaohitaji huduma wapo wengi
 
Huyu wa sasa anachowaza ni kujenga miundombinu tu na kununua ndege! Neno MAENDELEO kwake ni VITU tu! Hataki kabisa kuhusisha na WATU.

Na ndiyo maana mpaka sasa anatoa ajira za wahitimu wa vyuo kwa kusuasua, amejigeuza kuwa SHETANI/IZRAEL MTOA ROHO kwa Wafanyakazi wa nchi hii, nk.
 
Acha Ankoli atunyooshe. Tulizidi kukebehi utawala wa JK kana kwamba si lolote wala chochote..!

Ankoli ashikilie hapo hapo ili akili itukae sawa.

Wakati JK anawakata wafanyakazi 8% kwenye mishahara yao ya Mkopo wa Elimu ya Juu na kupunguza PAYE kwa wafanyakazi hadi 12%, Huyu wa sasa kapandisha makato ya Elimu ya juu hadi 15% na hajapunguza makato yoyote kwenye PAYE. Matokeo yake maisha kwa mfanyakazi yamekuwa magumu sana.
Kiufupi ukiwa ni mfanyakazi katika awamu hii kama hukujenga nyumba katika awamu iliyopita basi awamu hii ya miaka kumi ya JPM kujenga nyumba ni ndoto!. Utadunduliza fedha, fedha zenyewe ziko wapi?, bili za maji zimeongezeka, gharama za mawasiliano (vifurushi) zineongezeka, bei ya gesi ya kupikia imeongezeka, gharama za vyakula kama unga vineongezeka etc
 
Hata mm naonaga sawa tu MWAMBA WA CHATO anavotunyoosha! Enzi za JK wananchi tulijigeuza JINI KISIRANI! Kidogo utaskia MGOMO WA MADAKTARI.... haujakaa sawa utaskia na DARUSO wametangaza MGOMO... ukirudi huku unaskia CHAHEMA wanaandamana.... Huyu twendeni naye tu ili tujifunze kuwaheshimu Viongozi wanyenyekevu wenye upole!
Acha Ankoli atunyooshe. Tulizidi kukebehi utawala wa JK kana kwamba si lolote wala chochote..!

Ankoli ashikilie hapo hapo ili akili itukae sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema mkishashiba mnaaanza porojo

Yaani wafanyakazi laki tano Ndio muiondoe Ccm madarakani

Nyie mpo laki tano Kwahiyo msiwe wabnafsi Watanzania wanaohitaji huduma wapo wengi
Kuna muda unaropoka pumba Sasa Chadema inatoka wapi kwenye swala la kuongeza maslai ya watumishi umesahau Kama hao ndio wanaomuwakilisha Rais uko maofisin iwe shuleni hospital na sehem nyingine hujui hao wakiharibu inaonekana Rais ndio kafanya vibaya sio kila kitu lazma ukoment umekuwa kama nyumbu Sasa unaoboa
 
Kuna muda unaropoka pumba Sasa Chadema inatoka wapi kwenye swala la kuongeza maslai ya watumishi umesahau Kama hao ndio wanaomuwakilisha Rais uko maofisin iwe shuleni hospital na sehem nyingine hujui hao wakiharibu inaonekana Rais ndio kafanya vibaya sio kila kitu lazma ukoment umekuwa kama nyumbu Sasa unaoboa

Huyo ana Chadema phobia
 
Back
Top Bottom