Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,791
- 31,803
Wanamajlis,
Naona kumekuwa na hamu mpya ya kusoma historia ya nchi yetu.
Pamoja na kitabu cha Abdul Sykes kipo kitabu kingine kimeandikwa
na Ali Muhsin Barwani aliyekuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist
Party (Hizbu) ''Conflicts and Harmony in Zanzibar.''
Ali Muhsin alikuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wakati mapi.nduzi
yalipotokea mwaka wa 1964 na alifungwa jela za Bara kwa miaka 10.
Katika kitabu hiki Ali Muhsin anaeleza siasa za Zanzibar wakati wa
kupigania uhuru wa Zanzibar yeye akiwa kiongozi wa Hizbu.
Ali Muhsin anaeleza mchango wa Nyerere katika kuunda Afro-Shirazi
Party (ASP) na jinsi kuundwa kwa chama hiki kilivyobadili muelekeo
wa siasa visiwani kutoka ''utaifa'' kuelekea ''ukabila.''
Ali Muhsin atakushika pale anapoeleza maisha yake ya jela kwa miaka
kumi akianzia Ukonga, Isanga hadi Butimba na Bukoba hadi kuachiwa
mwaka wa 1974 na jinsi alivyotoroka nchini kupitia mpaka wa Horohoro
kwa msaada wa mfungwa mwenzake waliojuana jela.
Ukikianza hukiweki chini.
Kitabu hiki kinapatikana maduka ya vitabu Ibn Hazm Media Centre
Msikiti wa Mtoro na Manyema kwa bei ya shs: 10,000.00.
Pia kinapatikana Tanzania Publishing House (TPH) Samora Avenue kwa
bei ya shs: 13,000.00