Kumbukumbu yenye huzuni ya dereva Mtanzania aliyefia na kuzikwa Congo

Explainer

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
516
504
Natumai wengi wetu tu wazima wa afya tele, maana bado naona thread zenu na post kibao toka kwenu wakuu.Acha nisiwe mchoyo wa mambo mazuri yenye kufundisha jamii yetu, nachukua nafasi hii kufanya kama kumbukumbu na ukumbusho wa tukio la kifo cha ghafla cha ndugu yetu mtanzania mwenzetu kilichotokea nchi jirani ya kongo akiwa safarini, hakika popote ulipo ikiwa ughaibuni au nchi za mashariki ya mbali, basi kama ukikutana na MTZ mwenzako jua kwamba angalau umepata ndugu mpya uko, maana nimeamini tuna upendo wa kweli kabisa, tukio hili lilitokea nchini kongo miaka kama miwili sasa imepita baada ya dereva mmoja raia wa TZ kuugua ghafla na kufariki akiwa njiani.

IMG_20150418_054216.jpg
Na hilo ndilo lililokuwa gari lake akiendesa, kwa msaada mkubwa wa madereva wengine wa TZ, ambao wao pia walikuwa njiani, waliweza kujichangisha na kupata walau pesa kidogo kwaajiri ya kuustili mwili wa dereva huyo alietokea TZ, hawakuweza kumrudisha nyumbani kwa kukosa pesa zaidi na kukosa nafasi pia,

IMG_20150418_054243.jpg
Hayo ni baadhi ya magari kutokea TZ yakiwa yamepaki pamoja na gari la marehemu, na madereva wakiwa wanashughulikia kibali cha mazishi, pamoja na kutoa taarifa polisi

IMG_20150418_102057.jpg
Hapa ni sehemu mojawapo ya pori kubwa lililopo pembezoni kidogo mwa barabara ambapo serikari ya kijiji ilikubali kuwaruhusu madereva hao kufanya taratibu za mazishi wakisaidiwa na kiongozi mmoja wa dini tokea kijijini hapo,

IMG_20150418_091009.jpg
Madereva wakichimba kabuli, kwa umoja na ushirikiano,''hapakuwa mahari sahihi sana, lakini ilibidi ndugu yetu apumzikie hapo'

IMG_20150418_112152.jpg
Na hapo ndipo ulipokuwa mwisho wa safari ya ndugu yetu huko ugenini, idadi ndogo ya watu wenye uchungu nae, uchungu wa kitaifa tu na wala sio kuwa ndugu wala jamaa wa karibu na marehemu, lakini ilitosha waziwazi kuonesha ni jinsi gani tumekuwa na upendo na kusaidiana na kuwa mfano bora wa kuigwa na jamii nyingine.'' watu wachache sana walitosha kuwakilisha idadi kubwa ya ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa TZ.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake, ameni.
 
waliohusika wengi
So sad, ila mkuu mbona Congo karibu tu na TZ!! Kwanini msingemleta ndugu yetu akazikwa tu huku?
ingekuwa vigumu sana, kwasababu watu wote walikuwa bado wakiwa safarini, pia kukosa fedha za kutosha kwa wakati kutokana na tatizo la mawasiliano na taratibu za dini tena.. maana kiutaratibu ingechukua muda zaidi kupata vibari na usafirishaji kuanza.
 
Natumai wengi wetu tu wazima wa afya tele, maana bado naona thread zenu na post kibao toka kwenu wakuu.Acha nisiwe mchoyo wa mambo mazuri yenye kufundisha jamii yetu, nachukua nafasi hii kufanya kama kumbukumbu na ukumbusho wa tukio la kifo cha ghafla cha ndugu yetu mtanzania mwenzetu kilichotokea nchi jirani ya kongo akiwa safarini, hakika popote ulipo ikiwa ughaibuni au nchi za mashariki ya mbali, basi kama ukikutana na MTZ mwenzako jua kwamba angalau umepata ndugu mpya uko, maana nimeamini tuna upendo wa kweli kabisa, tukio hili lilitokea nchini kongo miaka kama miwili sasa imepita baada ya dereva mmoja raia wa TZ kuugua ghafla na kufariki akiwa njiani.

View attachment 367574 na hilo ndilo lililokuwa gari lake akiendesa, kwa msaada mkubwa wa madereva wengine wa TZ, ambao wao pia walikuwa njiani, waliweza kujichangisha na kupata walau pesa kidogo kwaajiri ya kuustili mwili wa dereva huyo alietokea TZ, hawakuweza kumrudisha nyumbani kwa kukosa pesa zaidi na kukosa nafasi pia,View attachment 367578 hayo ni baadhi ya magari kutokea TZ yakiwa yamepaki pamoja na gari la marehemu, na madereva wakiwa wanashughulikia kibali cha mazishi, pamoja na kutoa taarifa polisiView attachment 367583hapa ni sehemu mojawapo ya pori kubwa lililopo pembezoni kidogo mwa barabara ambapo serikari ya kijiji ilikubali kuwaruhusu madereva hao kufanya taratibu za mazishi wakisaidiwa na kiongozi mmoja wa dini tokea kijijini hapo,View attachment 367587madereva wakichimba kabuli, kwa umoja na ushirikiano,''hapakuwa mahari sahihi sana, lakini ilibidi ndugu yetu apumzikie hapo'View attachment 367588na hapo ndipo ulipokuwa mwisho wa safari ya ndugu yetu huko ugenini, idadi ndogo ya watu wenye uchungu nae, uchungu wa kitaifa tu na wala sio kuwa ndugu wala jamaa wa karibu na marehemu, lakini ilitosha waziwazi kuonesha ni jinsi gani tumekuwa na upendo na kusaidiana na kuwa mfano bora wa kuigwa na jamii nyingine.'' watu wachache sana walitosha kuwakirisha idadi kubwa ya ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa TZ,.. Mungu ibariki tanzania na watu wake, ameni.
Poleni sana,ila kwa nn msiwasiliane na tajiri wake aweze kusaidia, maiti ya mfanyakazi wake irejeshwe nyumbani?? baada ya hapo hili gari lake lilichukuliwa na nani
 
Nahisi kutoka machozi.
Jamani njoeni Tz muwataarifu mabosi zake nao watawatafuta ndugu zao waende kufukua mwili wausitiri huku Tz.
Jamani porini sana mmemuweka.

Namkumbuka dereva wetu aliyekuwa anaitwa Kisungura...alidondoka na gari Sekenke gari ikawaka moto na kufa.
Kwa ushirikiano wa madereva wenzake tulipata gari ilipo, tukachukua maiti pamoja na ndugu zake tukamzika.
Taarifa tu
 
Pole Sana Wote Walioguswa Na Huo Msiba Ingawa Kweli Tunawajibu Wa Kujiandaa Kwa Safari Ya Mwisho!!
Job 1:21
 
Back
Top Bottom