Kumbukumbu ya Nyerere iwe siku ya kuzaliwa na sio kufa; Kingunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbukumbu ya Nyerere iwe siku ya kuzaliwa na sio kufa; Kingunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by iron finger, Oct 14, 2011.

 1. iron finger

  iron finger JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  akichangia katika mdahalo wa leo mzee kingunge alisema mashujaa duniani kote hukumbukwa kwa siku zao kuzaliwa na sio kufa akatoa mifano kwa george washnton.karl max,lenin,na komrade mao.amesemema ameshajaribu kupeleka swala ilo kwenye vikao vikubwa lakini akasema majibu ni busness as usually!
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  na yeye asubili kukumbukwa kwa uasisi wa chipukizi..
   
 3. M

  Mzee Madoshi Senior Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hili limenikuna sana, tunasherehekea siku ya vifo vya watu wabaya kama kumbukumbu nzuri ya kuondoka kwa duniani, kwamba dunia sasa imekuwa bora zaidi kwa kifo cha mshenzi huyu. Kwa waliokufa kwa matukio maalumu, kusherehekea siku ya kifo ni kama kumbukumbu na fundisho kwa wengine kuwa yaliyotokea ni mabaya na yasirudiwe.

  Na tunasherehekea siku za kuzaliwa kwa watu wazuri kama shukrani kwa mungu kwa kuweza kumleta kiumbe huyu duniani ambaye amekuwa mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya wanadamu. Sasa labda kwa kusherehekea siku za kufa kwa Nyerere na Karume ni sherehe kwa baadhi ya watu, au vifo vyao ni ndio mwanzo wa mchango wao wa ukombozi kama ilivyokuwa kwa Yesu bin Mariam
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hapa Mzee kasema kweli. Tatizo litakuwa kwa mwenzetu wa Zanzibar sijui kama wanajua alizaliwa tarehe ngapi!!
   
 5. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Navyoona hata mimi kauli ya kingunge ina make sense. Mengine huwa anachemsha lakini kwa hili naona amewaza mbali .
   
 6. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  It doesn't make difference. Suala ni kumuenzi kwa matendo yake tu. Hizi zingine ni bwebwe tu zisizokuwa na tija. Kama ni hivyo, mbona siku nyingi tu tunazoweza kuzichukulia kama za matukio muhimu ya mwalimu. Mimi ningeshauri siku Nyerere, Uhuru na Masujaa iwe siku moja tu. Huwezi kumkumba Nyerere au mashujaa wa nchi hii kwa kuwatenga na Uhuru.
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  MKuu umenichekesha na hii .Itabidi tuanze kuwachapa darasa kaka wajue nini tunafanya .Kingunge kusema maneno yale ina ana kiri kwamba ma CCM si masikivu au yalifanya hivi makusudi ili kuhakikisha Mwalimu harudi maana wana sherehekea .
   
 8. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Siyo lazima, hivi Yesu na Nyerere nani maarufu? tunaadhimisha krismas na Pasaka pia (Ijumaa kuu wote hatuendi kazini), hata sisi watu binafsi tuna sherehekea siku ya kuzaliwa tukiwa hai, ukishakuwa marehemu watu wanaadhimisha kifo chako. hayo mambo yalikuwa ya wana socialist na Kingunge ndo socialist aliyekubuhu.
   
 9. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Megawatt, tatizo watu wanachanganya kumbukumbu ya tukio; na shughuli, mawazo, mtazamo na malengo ya tarehe husika. Wengine wanaona kila unapokumbuka tukio, maana yake unasherekea. hapo ni NO!. Utakapoelewa maana ya kuiadhimisha siku husika, ndipo utaona matukio yote yanafundisha siyo kusherekea tu. Tatizo watu wanawaza sherehe tu ndo maana wanafanya starehe za ajabu hata katika sikukuu za dini kama Krismas, Pasaka na Idd bila kujua malengo ya siku hizo. Sioni sababu ya watu kuanza kujadili siku baadala ya ujumbe wa siku. Huku ni kuishiwa sera na maneno ya kujadili.
   
 10. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Jf imeharibika.yaani hakuna anyejua falsafa ya kuadhimisha siku mtu alipokufa badala ya kuzaliwa? Msipomchunga kingunge atasema xsmass ni bora kuliko pasaka.hana dini yule.siku ya kufa ina maana kwenye historia ya mtu kuliko kuzaliwa
   
Loading...