Kumbukumbu ya miaka 40 kifo cha Steve Biko na hali ya kisiasa nchini

Aug 29, 2017
90
154
Tarehe 12/9/1977, kijana Steve Biko aliyekuwa akipingana na sera za kibaguzi wa rangi aliuawa nchini Afrika Kusini.

Biko aliuawa akiwa kijana mdogo tu wa miaka 30 na ushee ingawa alikuwa amefanya makubwa na yakukumbukwa sana nchini mwake na ulimwenguni kote hadi hii leo.

Kifo cha Biko kilipokelewa kwa simanzi na masikitiko makubwa na wapenda haki na uhuru duniani, ndo maana hata hii leo kila ifikapo 12/9 kizazi cha wapenda haki humuwashia mishumaa ya kumtakia amani huko aliko.

Tanzania ilikuwa ni mmoja ya mataifa yaliyokuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wa mataifa ya kusini mwa jangwa wa Afrika na bila shaka ililaani vikali kuuawa kwa kijana Steve Biko.

Miaka arobaini toka kifo cha Biko, dunia imeshuhudia mabadiliko makubwa ikiwemo kukoma kwa utawala wa weupe wachache na sera za kibaguzi nchini Afrika Kusini.

Nchini Tanzania nako mambo sasa yamegeuka, ule uharamia aliokuwa akiupinga Biko huko kwao Afrika Kusini na kupata uungwaji mkono wa Tanzania umeota mizizi nchini.

Hivi karibuni, hasa toka awamu ya tano iingie madarakani, kumetokea matukio mengi yasiyo ya afya kwa ustawi wa haki na uhuru wa taifa letu.

Matukio ya utekaji na utesaji, mauaji na uvamizi wenye mlengo wa tofauti za kiitikadi na kisiasa hapa nchini pamekuwa pahala pake.

Tukio la kukumbukwa zaidi ni la kuuawa kikatili kwa aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Busanda uchaguzi mkuu 2015 na mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita Kamanda Alphonce Mawazo ambaye alikatwa katwa mapanga mchana kweupe hali ilyopelekea umauti wake.

Mwaka mmoja baada ya kifo cha Mawazo aliyekuwa rafiki yake wa karibu Ben Rabiu Saanane, msaidizi binafsi wa Mwenyekiti wa CHADEMA taifa mheshimiwa Freeman Mbowe alitoweka na hadi sasa hajapatikana.

Tarehe 7/9 mwaka huu Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, mbunge wa jimbo la Singida mashariki na Rais wa chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) huko Dodoma alimiminiwa risasi thelathini na mbili na kuachiwa majeraha makubwa.

Mheshimiwa Tindu Lissu amekuwa mkosoaji mkuu wa serikali ya rais Magufuli akiituhumu kuwa inaendeshwa katika misingi ya kidikteta, kikabila, kidugu na usiginaji wa katiba.

Hadi sasa mheshimiwa Lissu amelazwa katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako anapatiwa matibabu ya risasi tano zilizompata.

Haya ni matukio machache ukiachia kesi zinazofunguliwa kila kukicha dhidi ya wafuasi ya vyama vya upinzani nchini hasa CHADEMA na uvamizi endelevu wa ofisi za mawakili nchini.

STEVE BIKO ULIPIGANA VITA ILIYOSALAMA, PUMZIKA KWA AMANI.
 
Kizuri hakidumu sijui kwasababu wengi hukihitaji hivyo huwazi kuchakaa na kufikia mwisho au ni kutokana na kuhitajika Sana hivyo wenye wivu huamua kukiteketeza mapema..... Siko katika mood nzuri ila Lisu akirudi nitakuwa vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom