Mu7
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 1,559
- 1,821
Heshima zenu WanaJF wote. Niende kwenye mada:
Tarehe 7 April kila mwaka ni siku ambayo ndugu zetu Wanyarwanda huadhimisha kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari ambamo wapendwa wao karibia milioni 1 waliuawa. Siku hiyo kuna ibada na hotuba za viongozi mbalimbali wakikumbuka tukio hilo lililoacha makovu kama sio madonda ya kudumu mioyoni mwa Wanyarwanda wengi. Siku hiyo tumekuwa tukishuhudia kwenye vyombo vya habari jinsi machungu yanavyoamka upya na kupelekea baadhi yao kuzimia wakikumbuka matukio ya kutisha waliyoyashuhudia wakati wa mauaji yale ya 1994.
MAONI YANGU:
Kwa kuwa machungu ya tukio lile bado ni makali mioyoni mwa Wanyarwanda wengi na nchi hiyo bado inaendeleza juhudi za kuleta maelewano, maridhiano na msamaha miongoni mwa wananchi wake waliotendeana vibaya, nashauri maadhisho hayo yasitishwe kwa kuwa kibinadamu ni vigumu sana kumsamehe mtu uliyemshuhudia akimuua kikatili mzazi wako, dada yako, kaka yako, mtoto wako au mme/ mke wako kumbukumbu ya tukio inapokuwa bado kali. Ni maoni yangu tu.
Karibuni kwa michango yenu.