Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Historia ya TANU ukipenda unaweza kuanza na Kleist baba yake
Abdul miaka ya 1920 na unaweza pia kuanza na Kleist mwenyewe
miaka ya 1940 mwishoni.

Lakini pia ukipenda unaweza kwenda nyuma zaidi katika Vita Vya
Maji Maji wananchi waliponyanyua silaha dhidi ya ukoloni wa
Wajerumani.

Hapa utakutana na Chief Abdul Rauf Songea Mbano.
Aaah! stori zako zote umezi limit kwenye udini (scope ni udini), nizisome mara tatu tatu ili iweje?
 
....................
Kama jambo dogo kama hili umeshidwa to get the facts right, what about the credibility of the rest?.

Paskali

Ref:
A Modern History of Tanganyika
Google Books › books
John Iliffe - 1979 - ‎History
Its first president was Mwalimu Cecil Matola, the aristocratic Yao teacher educated at Kiungani who ...
Kleist Sykes - Wikipedia
Wikipedia, the free encyclopedia › wiki › Kleist...
Kleist Sykes (1894–1949) was a Tanganyikan political activist. ... along with friends including Mzee bin Sudi, Cecil Matola, Suleiman Mjisu and Raikes Kusi.
Mohamed Said: CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) YABOMOA ...
www.mohammedsaid.com › 2015/02 › c...
14 Feb 2015 - Historia ya CCM inaanza mwaka 1929 katika nyumba ya Cecil Matola (sasa mali ya marehemu ...
A Place in the World: New Local Historiographies from Africa and ...
Google Books › books
Axel Harneit-Sievers - 2002 - ‎History
Matola, Cecil 1929. Cecil Matola Anatuhadithi Habari za Maisha Yake [ Cecil Matola tells us from his life]. Illambo Leo ...
Generations Past: Youth in East African History
Google Books › books
Andrew Burton, ‎Andrew Ross Burton, ‎Helene Charton-Bigot - 2010 - ‎History
March 1930], Kisarawe District Book, TNA). 16. Cecil Matola to Chief Secretary (CS), 22 April 1930, TNA 61/ 207/I/12.
Nyerere: The Early Years - Ukurasa 245 - Matokeo ya Google Books
Google Books › books
Thomas Molony - 2014 - ‎Biography & Autobiography
... Ujuzi Educational Publishers, 2006, pp.47–8 on the role of Martin Kayamba, Cecil Matola, Ramadhani Ali and Kleist ...
Miaka 48 bado tunaficha ukweli, kwa nini? – Raia Mwema
www.raiamwema.co.tz › miaka-48-bado-...
19 Mei 2012 - AA ilizaliwa Dar es Salaam 1927 chini ya uongozi wa Cecil Matola akiwa Rais na Kleist P. Sykes ...

I love rigorous scholarship. Big up Sir.
 
Uko serious? kama kiingereza hamkimudu tumieni kiswahili. Pia hii ungepeleka Jukwaa la biashara au historia.
Wakudadavua,
Huyu ndugu yangu ana mambo.

Kitabu hakina publisher, hakina ISBN hakina chochote wala huko
Amazon hakipo.

Nimempa darsa zima vipi mambo ya uchapaji wa vitabu ulivyo yeye
kabakia na jeuri na ubishi ambao haumsaidii lolote ila kuzidi kumtia
katika kundi la wachekeshaji.

Angalia hapo chini ''blarb,'' kama ilivyoandikwa na Yericko:
Mohamed Said Salum Angalia ''kitabu,'' cha Yericko hicho anasema
kipo Amazon na Amazon hawana hicho, ''kitabu.''

 
Aaah! stori zako zote umezi limit kwenye udini (scope ni udini), nizisome mara tatu tatu ili iweje?
Automato,
Hivyo ndivyo unavyoona wewe lakini mimi nilichoandika ni historia ya Waislam
walivyopambana na ukoloni.

Ikiwa huo ni udini sina la kusema na ibaki nimeandika, ''udini,'' maana sina njia
ya kuibadili historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Sijakuita kuja kunisoma.

Umekuja kwa khiyari yako ukipenda unaweza ukawa unayapita tu mabandiko yangu
hakuna shida.
 
Dah!
Huyo mzee kyaruzi nikikuwa namfahamu sana kabla hajafariki, makazi yake yalikuwa pale maeneo ya uwanja wa ndege manispaa ya bukoba,alikuwa ananipa historia nabaki nimeduwaa!
Mungu amlaze mahari pema.

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
M2...
Soma hapo chini ni bandiko langu la ziku za nyuma hapa Majlis:

Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki
grey10.gif
By Mohamed Said
Pondamali,
Hilo usemalo wala halina wasiwasi umesema kweli.

Abdul Sykes alikuwa katibu na kaimu rais wa TAA toka Dk. Kyaruzi alipopewa
uhamisho.

Wala sina haja ya kuweka sawa ninayoandika hilo mie nikilijua siku zote.
Kwani pamezuka nini?

Vipi kuhusu habari za Mzee Kasella Bantu.

Ungependa nikuwekee hapa habari zake zaidi au umetosheka basi na zile za
mwanzo?

Pondamali,
Historia Abdul Sykes inakuhangaisha wewe kama ilivyowahangaisha
wengi kabla yako.

Kwa mara ya kwanza nilipoandika habari zake katika gazeti la Africa
Events lililokuwa linachapwa London, toleo zima lilikusanywa likapigwa
moto.

Jiulize amri ya kuyakusanya magazeti yale ilitoka wapi na nini sababu
yake?

Huenda usiamini lakini ndivyo ilivyokuwa.

Kwa yale machache ambayo yaliwafikia watu habari ile ilikuwa gumzo
kubwa.

Watu wengi walivurugikiwa akili kama wewe hii leo akili yako
inavyovurugika.

Unajiuliza,''Hii kweli au ni uongo na porojo za Mohamed Said?''

Watu wengi hapa jamvini husema naandika porojo.
Wengi walikuwa hawajamsikia Abdul Sykes kuwa ndiye aliyeunda
TANU.

Sasa gazeti lile lilikuwa na makala,‘'In Praise of Ancestors’' Africa
Events,
London, March/April 1988, (uk. 37-41) nilitaja mchango wa
Waislam na nikamtaja Abdul Sykes.

Kwa wengi historia hii ilikuwa ngeni kabisa.

Pondamali sasa nakurudisha kwa Dk. Kyaruzi na dhana kuwa yeye
ndiye aliyemwachia chama Nyerere.

Nakuambia kwa kinywa kipana kabisa.
Huo ni uongo.

Haya ninayoweka hapo chini nimetoa katika kitabu changu:

''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold
Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,''
Minerva Press, London 1998.

''In June, TAA headquarters announced its executive committee
with J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President;
J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias
and
Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer
and Ally K. Sykes as Assistant Treasurer. Committee members were
Dr. Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z.
James, Dome Okochi, C. Ongalo
and Patrick Aoko.[1] The composition
of the TAA leadership showed East African solidarity that existed
during the struggle for independence. Kenyan patriots were elected
as office bearers side by side with Tanganyikans. It is said that it
was about that time, in the last months of 1953, that Abdulwahid
talked to Nyerere seriously about forming an open political party to
replace TAA.''



[1]Tanganyika Standard, 19 th June 1953.

Pondamali,

Nimekuwekea hapa juu uongozi wa TAA wa 1953 na gazeti ambalo
lilitaarifu habari hiyo.

Umeomuona Mzee Kasella Bantu katika mabadiliko hayo ya kihistoria?

Uongozi huu mpya ulitokea baasa ya uchaguzi wa tarehe 17 Aprili
katika Ukumbi wa Arnautoglo ambako Nyerere alichaguliwa kuwa rais
wa TAA na Abdul Sykes makamu wake.

Katika hali kama hii vipi Dr. Kyaruzi iwe kamuachia chama Nyerere?

Achilia mbali kuwa yeye alipata uhamisho kwenda Kingolwira na kisha
Nzega mwaka 1951.

Mimi nawapeni sana pole kwa kuwa kwa kweli mnaziviza akili zenu
pasi na sababu ya maana.

Hakuna mwanahistoria ambae ataweza kuandika historia ya TANU
au ya Nyerere bila ya kwenda kwenye Nyaraka za Sykes.

Hii ni hazina ya kipekee kabisa.
Ukiwa hujaridhika rejea tena na maswali mengine.

Insha Allah utanikuta mie bado nabariz hapa jamvini nakusubiri.

Tuagane kwa swali hili langu moja.

Pondamali,

Mzee Kasella Bantu hakupata kukuhadithia ile ''drama,'' siku ile
ya uchaguzi kati ya mwalimu wa shule Nyerere ambae hakuna
aliyekuwa anamfahamu na Abdul Sykes kijana maarufu wa mjini?

Mimi ''movie'' nzima ninayo kanihadithia Dossa Aziz nyumbani kwake
Mlandizi.

Mzee Kasella Bantu hakupata kukuhadithia kwa nini yeye na
Nyerere walikuwa maadui wakubwa kufikia Kasella Bantu kutoroka
nchi kwenda Ujerumani hali kapitishwa uwanja wa ndege kavaa
mavazi ya kipadri?
 
Juvenile...
Hana kitabu ndugu yangu...
Mauzauza...

Ili kiwe kitabu kuna vigezo vya kukidhi.
Hamna hata kimoja.

Hana ''publisher,'' wala ISBN.
Lakini mwenyewe anasema kitabu kipo Amazon.

Ukienda Amazon hamna hicho kitabu.
Namsubili Yericko aje kujibu hizi hoja.
 
Automato,
Hivyo ndivyo unavyoona wewe lakini mimi nilichoandika ni historia ya Waislam
walivyopambana na ukoloni.

Ikiwa huo ni udini sina la kusema na ibaki nimeandika, ''udini,'' maana sina njia
ya kuibadili historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Sijakuita kuja kunisoma.

Umekuja kwa kjiyari yako ukipenda unaweza ukawa unazipita tu mabandiko yangu
hakuna shida.
Mzee mo shikamoo sasa mzee wangu kwani kunaanae kataa kuwa waislam hawakupigania uhuru wapo sema kuna wale wasaliti ambao walikua wanataka tusipate uhuru mapema mpaka level ya wakristo na waislam ziwe sawa kielimu mfano chama cha (AMNUT)Kilikua cha waislam Kilikua kinapinga kuwahi kupata uhuru mapema kwa sababu hiyo. Kwa hiyo hizi zana za kuonyesha waislam wanaonewa au wataonewa hazijaanza leo.Unajua mtu unapochukulia unaonewa hata usipoonewa utasema unaonewa ukiwa unawapa lecture wajamaa waambie bwana na hili swala.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mzee mo shikamoo sasa mzee wangu kwani kunaanae kataa kuwa waislam hawakupigania uhuru wapo sema kuna wale wasaliti ambao walikua wanataka tusipate uhuru mapema mpaka level ya wakristo na waislam ziwe sawa kielimu mfano chama cha (AMNUT)Kilikua cha waislam Kilikua kinapinga kuwahi kupata uhuru mapema kwa sababu hiyo. Kwa hiyo hizi zana za kuonyesha waislam wanaonewa au wataonewa hazijaanza leo.Unajua mtu unapochukulia unaonewa hata usipoonewa utasema unaonewa ukiwa unawapa lecture wajamaa waambie bwana na hili swala.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Madrid Boy,
Kisa cha AMNUT umekianza katikati kwa hiyo kuna mengi huyajui kwa nini
palitokea kukosana ndani ya TANU na hii inasababishwa na kutoijua historia
ya uhuru wa Tanganyika.

Inataka uanze kwanza na mkutano wa 1955 alioitisha Sheikh Hassan bin Amir
agenda ilikuwa moja tu na ilikuwa kuweka indhar ya suala la Uislam katika
TANU.

Kisha uje Uchaguzi wa Kura Tatu 1958na kile kilichotokea katika yale masharti
ya kibaguzi ya kupiga kura.

Ukitoka hapo uje katika ugomvi uliotokea mwaka huo huo wa 1958 kati ya
Sheikh Suleiman Takadir na Mwalimu Julius Nyerere.

Sasa usikimbilie kushutumu kuhusu unakokuita, ''kuonewa,'' kwa Waislam.

Siwezi hapa nikaeleza kila kitu hadi uelewe historia yenyewe na nchi yetu
kufika hapa tulipo kwa jamii moja na ndiyo iliyopigania uhuru kusema kuwa
haitendewi haki.

Ukweli ni kuwa tatizo lipo na nimeeleza kila kitu katika kitabu cha Abdul Sykes
kitafute kitabu usome hata kama hutakubaliana na mimi lakini utajua hisia za
Waislam.

Unaweza pia kumsoma P van Bergen, ''Religion and Development,'' (1981) na
Hamza Njozi, ''Mwembechai Killings,'' (2002) kuna mengi ya kujifunza.

Unaweza pia ukaingia katika blog yangu www.mohammedsaid.com na fanya
''search,'' kwa majina mathalan, ''Sheikh Suleiman Takadir,'' au kwa matukio
kama ''Kura Tatu,'' nk. utaelewa kwa nini historia ya uhuru wa Tanganyika imekuwa
na shida ya kufahamika na kwa nini walioandika waliogopa kutaja baadhi ya majina
ya wazalendo kama Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Abdul
Sykes
nk.
 
Dah!
Huyo mzee kyaruzi nikikuwa namfahamu sana kabla hajafariki, makazi yake yalikuwa pale maeneo ya uwanja wa ndege manispaa ya bukoba,alikuwa ananipa historia nabaki nimeduwaa!
Mungu amlaze mahari pema.

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Huyu mzee ndie hasa mpigania uhuru wa Tanganyika na ndie aliyemwachia kijiti cha uongozi Nyerere, sio hawa wazee wa Mohamed anaotembea nao dunia nzima akiwanadi
 
Juvenile...
Hana kitabu ndugu yangu...
Mauzauza...

Ili kiwe kitabu kuna vigezo vya kukidhi.
Hamna hata kimoja.

Hana ''publisher,'' wala ISBN.
Lakini mwenyewe anasema kitabu kipo Amazon.

Ukienda Amazon hamna hicho kitabu.
Mbona unahangaika sana mzee?
 
Mbona unahangaika sana mzee?
Yericko,
Kipi kitanihangaisha mie?
Kama Amazon nimekuwepo huko sasa karibu miaka 20.

Kitabu changu kimeuzwa WH Smith katika maduka yake yote Uingereza.
Ukenda Africa Centre, London nipo.

SOAS nipo.

Ukienda Marekani Barnes and Nobles...
Library of Congress, Washington niko..

Ukiingia Harvard ndiyo nilikuwa katika mradi wao wa Dictionary of African
Dictionary (DAB)...

Ukitaka kuwajua hawa wote ni nani katika duru ya usomi muulize Prof. Google.

Kama kuandika hilo wala usiseme hapa JF wakijua nimeingia barzani
nyote mnakuja jamvini kunisikiliza.

Kualikwa kwenye vyuo na ''research centres,'' usiseme.
Wewe ndiyo unaehangaika kaka yangu juu haupo chini kuna moto.

Amazon unaitaka lakini hujui utafikaje.

Nakupa darsa la uchapaji wa vitabu na historia ya TANU na rejea zake
huna moja...

Ahangaikae ni wewe kaka.
Jitazame utapata jibu.
 
Huyu mzee ndie hasa mpigania uhuru wa Tanganyika na ndie aliyemwachia kijiti cha uongozi Nyerere, sio hawa wazee wa Mohamed anaotembea nao dunia nzima akiwanadi
Yericko,
Dr. Kyaruzi
ana mchango wake na hawa madaktari katika historia
ya African Association wako watano: Dr. Luciano Tsere, Dr. Wilbard
Mwanjisi, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Joseph Mutahangarwa
na Dr.
Michael Lugazia.

Wewe unawajua hawa?
Ukweli ni kuwa hawakutajwa popote.

Nakupa changamoto hebu lieleze jamvi historia zao.

Historia ya TANU ya Kivukoni imewataja popote wazalendo hawa?
Mimi wote hawa nimewataja katika kitabu cha Abdul Sykes.

Mimi si ninaewanadi wazee wangu.

Wazee wangu wamo katika Dictionary of African Biography, Oxford
University Press, New York 2011.

Sasa anaeweza kuwafika watu kwa haraka na siku zote ni mimi au
ni hii dictionary?

Anaenadi nani?
Mohamed Said au DAB?
 
Yericko,
Dr. Kyaruzi
ana mchango wake na hawa madaktari katika historia
ya African Association wake watano: Dr. Luciano Tsere, Dr. Wilbard
Mwanjisi, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Joseph Mutahangarwa
na Dr.
Michael Lugazia.

Wewe unawajua hawa?
Nakupa changamoto hebu lieleze jamvi historia zao.

Historia ya TANU ya Kivukoni imewataja popote wazalendo hawa?
Mimi wote hawa nimewataja katika kitabu cha Abdul Sykes.

Mimi si ninaewanadi wazee wangu.

Wazee wangu wamo katika Dictionary of African Biography, Oxford
University Press, New York 2011.

Sasa anaeweza kuwafika watu kwa haraka na siku zote ni mimi au
ni hii dictionary?

Anaenadi nani?
Mohamed Said au DAB?

Yericko,
Jamaa hapo chini anaomba umpe majibu:

Haki MadhubutiSenior Member
#29
Yesterday at 10:32 PM

Makosa mengi ya kiuandishi, alafu kama una haraka ya "kufika kusikojulikana". Wewe sio writer/author aliyekamilika, jaribu masuala mengine. Unazidi kujiaibisha na kuonekana just a mere clown.
 
Juvenile...
Hana kitabu ndugu yangu...
Mauzauza...

Ili kiwe kitabu kuna vigezo vya kukidhi.
Hamna hata kimoja.

Hana ''publisher,'' wala ISBN.
Lakini mwenyewe anasema kitabu kipo Amazon.

Ukienda Amazon hamna hicho kitabu.
Hahaa hadi niende Amazon ndipo ntatoa conclusion
 
Yericko,
Wewe huna kisomo cha kupambana na mimi.

Nakupa changamoto nyingine.
Kitabu cha Abdul Sykes kimefanyiwa review na John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan.

Review ya Iliffe na Glassman zimechapwa katika Cambridge Journal of African History.

Sasa fanya utafiti uone hapa Tanzania ni wangapi wamepata kuandika na vitabu vyao vikapata review katika hii journal.

Yawezekana kabisa kwa kuwa huna ulijualo katika utafiti na uandishi ikawa huoni kabisa uzito wa jambo hili.

Lakini kukusaidia hebu nenda British Council Library katizame mna nini katika hii journal na usiishie kutazama muulize mkutubi hadhi ya hiyo journal.

Ati utaamka na mimi.
Uamke na mimi ndiyo iwe nini.

Amka kamwagie dawa bamia zako utakuwa umefanya kazi ya maana sana kuliko kutaka kuweka mjadala na Mohamed Said.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom