Kumbukumbu ya kushambuliwa kwa Lissu: Mitandao inaweza kukutoa machozi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Leo hii ukipita mitandaoni na kuona picha na matukio ya kushambuliwa kwa Lissu hakika unaweza kutokwa na machozi hasa kama ulikuwa ni mmoja wa watu uliomshuhidia Lissu kwa macho akiwa katika hali ile.

Binafsi nilikuwa pale Airport Dodoma siku ile usiku wakati Lissu anapakizwa kwenye ndege kabla ya kupelekwa Nairobi kwa matibabu.Kwa hakika sikutarajia kama Lissu angepona.

Nakumbuka kumuona Lissu akikwa hajitambui huku ametundikiwa ndripu ya maji(dawa),dripu ya damu huku akiwa na kifaa ambacho naamini ilikuwa ni mashine ya kumsaidia kupumua.Hakika lile tukio lilikuwa baya na la kikatila sana.

Waalaniwe waliopanga unyama ule mbingunui na duniani kwani hawataki kutubu bali wanaendeleza uovu wao bila woga na bila kumuogopa Mungu hivyo walaniwe.



 
Ni tukio lililonifanya niwachukie baadhi ya wanaJF kwa roho mbaya waliyoonesha wakati wa shambulizi hilo. Ni tukio lililosababisha nibadili msimamo kuhusu Barbarosa na Jingalao kwa tabia ya utu waliyoonesha wakati wa tukio hilo. Ni tukio lililonisaidia kutofautisha baadhi ya wanasiasa wa JF na ubora wao kisiasa. Ilinisaidia YEHODAYA ni miongoni mwao, nikajua pia Tumainiel ni WAO. Ni tukio lililoniletea rafiki GENTAMYCIN japo tulikuwa na tunaendelea kuwa na misimamo tofauti katika baadhi ya mambo. Ni tukio lililobadilisha utu na msimamo wa Imhotep, kijana machachari wa Lumumba aliyekataa kuwa mnafiki na kuamua kusimama katikati ya ubinadamu na kuchukia unyama. Ni tukio lililoiacha nchi ikiwa kimya na kwa hakika wengi tulidhani imetangazwa hali ya hatari. Kila mahali walionesha kuchukizwa na tukio hili, isipokuwa wachache wanaoamini maslahi yao binafsi yalikuwa yanaguswa na kutikiswa na misimamo ya Lissu. Najikumbuka siku hiyo na siku mbili baadaye yaani tarehe 7, 8 na 9 kila nilipokuwa nasoma habari za uzushi za kina YEHODAYA na kundi lake zikiongelea kifo cha Lissu nilitokwa machozi. Kwangu vifo pekee vya wanasiasa wa ndani vilivyonigusa ni kifo cha Sokoine, na Nyerere. Kwa nje ya nchi ni Rajiv Gandhi na mwanaharakati Princess Diana. Hivyo tukio la mtetezi halisi wa haki za watu Lissu kujeruhiwa halikuniacha salama. Waliofanya hivyo, wapatikane au wasipatikane kwangu wanaendelea kuwa maadui wa mpaka kifo changu, na wote wanaoshabikia upuuzi na unyama wa Sept7 wanabaki maadui zangu forever. Endeleeni kujifariji kwa maneno ya kejeli na kashfa lakini Mungu hajawahi kuchekea uovu na hakika mtalipa sasa au baadaye.
Lissu umepona ili kuonesha uwepo na uwezo wa Mungu, na kwamba bila ruhusa yake hakuna binadamu anayeweza kumdhuru mwenzake. Tunaoamini uwepo wake tunaamini amejidhihirisha kupitia tukio lako, hivyo muamini na kumtumikia yeye siku zote kwa vile ukuu wake umeonekana kupitia kwako.
 
Lakini tujikumbushe Jambo moja muhimu Sana katika tukio hili la kushambuliwa kwa Lisu. Huko Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam kulikuwa na tukio kubwa la kupokea ripoti ya Makinikia, tukio lililoongozwa na Rais Magufuli. Kwa maajabu ambayo hayajawahi kutolewa maelezo na yeyote, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hakuwepo Ikulu.
Kitendawili ni kuwa alikuwa wapi!!!? Wana JF hebu mwenye kufahamu atuambie siku Lisu anapigwa risasi Area D Dodoma saa 7/8 mchana, Daud Albert Bashite alikuwa wapi na akifanya
nilni!.!!?
 
Point Lini Atarudi Sasa Au Zito Ameshamwambia Asirudi Nyumbani Kwa Sasa Huko Hali Ni Mbaya Ndege Kukamatwa S A Na Kuachiwa Na Korosho Kukubari Kushindwa Kwa Sababu Anamjua Ni Mtu Wa Kuongea Sana Kwa Hofu Na Mapenzi Ya Urafik Wao Inawezekana Wasiojurikana Waka Mripua Tena Maana Kashasema Juzi Juzi Alienda Kumcheki Zito Mwambie Arudi Mkuu Sasa Akuna Noma Watu Wameshajijenga Kisiasa Na Wako Vizuri Kwa Hoja
 
Ile damu ya tundu lissu inazidi kuwatafuta kila wanalofanya linaangukia pua Ile miradi yote aliyokuwa anaitegemea imekufa kifo cha mende...
Huyo ndiyo MUNGU Bana huwa hadhihakiwi akisema NO hakuna wa kupinga
Nani chadema hao?
 
Back
Top Bottom