KUMBUKUMBU-siku baadhi ya wana Jf walipoamu kuwa wakimbizi wa muda,hivi ndivyo wakijifariji

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
4,981
2,000
1)Namanga hadi Holili,tunarejea nyumbani
Twarudi na zetu hali,na furaha vifuani
Safari yetu ya ghali,ila bado na imani
Tutaporudi nyumbani,tutakutana na Melo.


2)Tutapeana mikono,na kukumbuka zamani
Tulisaga visigino,kwenye kambi ya amani
Asopenda malumbano,aliitia kizani
Tutaporudi nyumbani,tutakutana na Melo.


3)Japo masaa machache,tutakuwa safarini
Tusubirini pakuche,tukaingie garini
Ugenini tupaache,maana hatupaamini
Tutaporudi nyumbani,tutakutana na Melo.


4)Tutaimba na kucheza,nyimbo zetu za nyumbani
Japo sana tutawaza,wale watu wa medani
Jinsi watavyo chunguza,ili watutie ndani
Tutaporudi nyumbani,tutakutana na Melo.


5)Tusihofu tutarudi,japo hatujui lini
Tushukuru tuna budi,na tuweke akilini
Tufanye sana juhudi,turejee salimini
Tutaporudi nyumbani,tutakutana na Melo.


6)Tutausema ukweli,kila kona duniani
Usikike hadi mbali,Arabuni na barani
Amerika na tusali,tumrudie Manani
Tutaporudi nyumbani,tutakutana na Melo.


7)Tutampa na salamu,za kule ukimbizini
Hali ilikuwa ngumu,ila tungefanya nini
Siku tukitia timu,tutaeleza kwanini
Tutaporudi nyumbani,tutakutana na Melo.


SHAIRI -TUTAKUTANA NA MELO.
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,963
2,000
afu wewe na jamaa yako ndo mlisababisha tukapigwa exile
 

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
4,981
2,000
Wengine bado wapo kile,inawezekana hawajaridhika bado na hali ya huku,ila waambieni warejee nyumbani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom