Kumbukumbu: prof. kighoma ali malima (15 december 1938 - 6 august 1995)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,908
30,252
1565100779837.png


Nimemjua Prof. Kighoma Ali Malima katika siku zake za mwisho wa maisha yake na nilijifunza mengi kutoka kwake kuhusu hali ya Waislam toka tupate uhuru mwaka wa 1961.

Nilipoandika kitabu cha Abdul Sykes kitabu hiki katika utangulizi nilikitoa kama tabaruku na kumbukumbu kwa Prof. Malima.

Inafaa siku kama ya leo kutafakari ingekuwaje iwapo kama Prof. Malima angeishi na akawa ni mmoja wa viongozi wa vyama vya siasa vilivyopo hivi sasa na Prof. Malima akiwa na agenda ya kuleta usawa wa kweli katika jamii hii yetu.

Prof. Malima aliamini kuwa njia pekee ya kuleta haki na usawa kwa wote ni kwake kupigania hili nje ya CCM na kwa ajili hii alijitoa kwenye chama hicho.

Mkutano wake wa kwanza wa hadhara na ndiyo alioutumia kujitoa CCM aliufanya Tabora Viwanja Vya Uyui.

Kishindo chake kilikuwa kikubwa.

Mkasa mkubwa ulitokea pale vyombo vya habari ambavyo vyote kwa sababu za wazi vilikuwa vikimpiga vita Prof. Malima toka akiwa CCM na katika Baraza la Mawaziri vilipoandika kuwa Prof. Malima atajitoa CCM ndani ya msikiti Tabora.

Sheikh Issa Mavumbi sheikh wa BAKWATA alitumika bila kujijua katika propaganda hizi na alipata fedheha kubwa kutoka kwa umma wa Waislam wa Tabora pale alipoletwa na polisi msikitini Tabora kuja kutahadharisha kuwa msikiti ule usimruhusu Prof. Malima kufanya siasa msikitini na kujitoa CCM akiwa ndani ya msikiti.

Vurugu kubwa ilitokea msikitini pale na msikiti siku ile ya Ijumaa ulikuwa umejaa hadi nje kwa ile propaganda iliyokuwa imezagaa kote kuwa Prof. Malima atajitoa CCM ndani ya msikiti ule.

Ilikuwa katika taharuki hii hapo ndipo aliposimama mwanasiasa mkongwe na muasisi wa TANU na harakati za kudai uhuru Mzee Bilal Rehani Waikela kutuliza hali ile.

Mzee Waikela akamuuliza Sheikh Mavumbi habari za Prof. Malima kuja msikitini kujitoa CCM yeye kapewa na nani?

Sheikh Mavumbi hakuwa na majibu.

Mzee Waikela akawauliza Waislam kama kuna mtu yeyote mle ndani ameomuona Prof. Malima ndani ya msikiti ule.

Prof. Malima hakuwapo Tabora siku ile achilia mbali kuwa ndani ya msikiti ule.

Sheikh Mavumbi alitolewa kwa haraka pale msikitini na polisi wale wale waliomleta mara ya kwanza huku kivumo cha, ''Takbir,'' kikitanda ndani na nje ya msikiti.

Sheikh Mavumbi ilimdhihirikia kuwa kasababisha vurugu ndani ya msikiti pasi na sababu yoyote.

Hii ilikuwa katika sala ya Ijumaa na baada ya Sheikh Mavumbi na askari kuondoka khutba ya Ijumaa ikaanza na Waislam wakakamilisha ibada kwa utulivu.

Hii ndiyo ilikuwa fungua pazia la Prof. Malima pale alipojitoa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uyui.

Ghafla joto la siasa nchi nzima lilipanda vibaya sana.

Harakati za chinichini za miaka mingi zilikuwa zimewatayarisha Waislam kusimama na kuuliza nini kimetokea kuwafanya wao juu ya mchango wao mkubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika leo wamekuwa raia daraja la pili?

Waislam walitegemea Prof. Malima sasa akiwa nje ya CCM ataiweka agenda hii uwanjani peupe ijadiliwe na ufumbuzi upatikane.

Inatosha kwa Prof. Malima akakumbukwa kwa hili.
 
Mie namfahamu yule mtoto wake alieibiwa mibinduki na mchepuko hotelini morogoro. Nlipata kuskia kisa kimoja kuhusu huyu profesa wakati akitetea elimu dunia kwa waislam alipambana sana.
Nasikia ndio muasisi wa kuweka mfumo wa namba badala ya majina katika mitihani, majina yalikuwa yanakuja kujulikana baada ya matokeo kuwa tayari na kutolewa public.
 
Alishafariki tumuache apumzike ila hata wahudumu wa Mipango enzi hizo walokuwa siyo waislamu aliwabadilisha! Vivyo hivyo hazina. Hebu tuyaache hayo
Hayo yepi tuyaache?

Nimeuliza neno uliloandika. "Mdini" maana yake nini?
 
Alikuwa mdini sana kiasi ofisini alileta maji katika thermos na Mhudumu alikoroga chai mbele yake. Aliweka chumba maalum cha kuswalia! Mengine tumsitiri ila
Hilo sio tatizo kusali kwenye chumba.ukenda ofisi fulan unakuta katibu mkuu kilabada ya dakika 20 anaingia kusali ,kashasfaafu naye islamiki sijui kwaaliyeteuliwa sasa
 
Nasikia ndio muasisi wa kuweka mfumo wa namba badala ya majina katika mitihani, majina yalikuwa yanakuja kujulikana baada ya matokeo kuwa tayari na kutolewa public.
Hili si kweli.
Namba zilianza hata kabla hajawa Waziri wa elimu, na mmoja wa Kaka zangu alitumia namba katika Mtihani.
 
Alikuwa mdini sana kiasi ofisini alileta maji katika thermos na Mhudumu alikoroga chai mbele yake. Aliweka chumba maalum cha kuswalia! Mengine tumsitiri ila
Njinjo,
Prof. Malima
hakuwa mdini ila alitahadharisha athar za udini uliokuwapo.

Ukitaka kusoma kuhusu tatizo hili soma kitabu cha Maisha ya Abdul Sykes
sehemu ya tatu ya kitabu na ndiyo ya mwisho nimeipa jina ''Njama Dhidi ya
Uislam.''

Katika sehemu hiyo nimeeleza kila kitu.
Sasa kama unataka kujua ukweli tuanze hapo.

Hili suala la tatizo ubaguzi ni nyeti sana na tumepata kujadili hapa Majlis
na mimi nimetoa ushahidi mwingi kwa kutumia rejea za kuaminika.

Huna wewe cha kumsitiri Prof. Malima ila wapo watu kwa kufanya staha
wanajizuia kusema mengi wayajuayo kwani zipo ''legacy,'' za baadhi ya
viongozi hakuna anaetaka zivunjike.

Lakini kama wewe unautaka mjadala huu fungua uzi wako mpya nami
nitakuja kutoa darsa.

Kuswali ndani ya ofisi hakujakuwa udini.

Mimi maisha yangu yote ya kazi nikiswali ofisini kwangu na nilikuwa na
msala kila ofisi niliyofanyakazi na wakubwa zangu walilijua hili na hata
siku moja hawakunikataza na wako wengi wanafanya hivi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom