Kumbukumbu murua: Tujikumbushe watangazaji mahiri wa mpira nchini

py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,476
4,447
Hawa ni watangazaji mahiri waliowahi kutangaza mpira nchini na wengine bado wanaendelea kutangaza.

Yupi alikuwa anaugonga moyo wako kati ya hawa

1. Ezekiel Malongo(R.I.P)
2. Ahmed Jongo
3. Swedi Mwinyi
4. Charles Hillary
5. Dominic Chilambo (R.I.P)
6. Ahmed Kipozi
7. Sekione Kitojo
8. Jesse John
9. Abubakari Liongo
10. Halima Mchuka (R.I.P Sport Lady)
11. Juma Nkamia
12. Tom Chilala
13. Shaaban kisu
14. Nadhiri Mayoka
15. Mickdad Mahmud
16. Sarah Dumba
17. Enock Bwigane
19. Abdallah Majura
20. Efrahim Kibonde
21. Maulid Kitenge
22. Omar Jongo
23.Salim mbonde
 
Ahmed Jongo,Swedi Mwinyi,Abubakari Liongo,Juma Nkamia hao jamaa achana nao
sijaona kama hao, hawa vijana wanajaribu tu ila bado sana
 
Du, nilikua sijui kama ezekiel malongo alishafariki. Alikua ananifurahisha sana. . RIP
 
Baraka Mpenja anakuja vizuri, akikazana huyu bwana mdogo atakuwa poa sana.
 
Baraka Mpenja anakuja vizuri, akikazana huyu bwana mdogo atakuwa poa sana.
Huyu Ezekiel Malongo alinitangazia World cup 2002 kipindi kile mashindano yamefanyika Japan na Korea kusini gemu zinachezwa saa NNE asubuhi,

Dah jamaa alikua anajua background ya kila mchezaji............
 
Ahmed Jongo,Sued Mwinyi Ramadhani,Juma Nkamia,Jesse John
Ahmed Jongo hakuwa akinifurahisha akitangaza
Hata marehemu Malongo hakunifurahisha,alikuwa mapepe sana.
Waliokuwa na sauti nzuri ya kutangazia mpira ni Nkamia,Jesse John,Sued Mwinyi ,Marehemu Iddi Rashidi Mchata na hata Bwigane.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom