Kumbukumbu Muhimu: Andrei Sakharov mwanafizikia mashuhuri wa nyuklia nchini Russia. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbukumbu Muhimu: Andrei Sakharov mwanafizikia mashuhuri wa nyuklia nchini Russia.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, May 21, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Leo ni Jumatatu tarehe 29 Jamadul Thani mwaka 1433 Hijiria, inayosadifiana na tarehe 21 Mei 2012 Miladia.

  Siku kama ya leo miaka 14 iliyopita, Jenerali Muhammad Suharto alilazimika kujiuzulu baada ya kuiongoza Indonesia kimabavu kwa miaka 33.

  Aliingia madarakani mwaka 1965 baada ya kufanya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Ahmad Sukarno muasisi wa wa Indonesia huru na rais aliyechaguliwa na wananchi wa nchi hiyo.
  Katika kipindi cha utawala wa Suharto nchini Indonesia, uhuru wa kisiasa ulidhibitiwa. Hata hivyo nchi hiyo ilipiga hatua kubwa kiuchumi hasa katika muongo wa 80 na 90.

  Mgogoro wa kiuchumi Mashariki mwa Asia mwaka 1997, mbali na kuleta pigo kwa uchumi wa nchi hiyo, ulipelekea pia kuzuka uasi wa wanachuo na taratibu matakwa ya kiuchumi yakachukua muelekeo wa kisiasa na wanachuo hao kuanza kupiga nara za kutaka kujiuzulu Rais Suharto.

  Mwishowe ubadhirifu wa mali ya umma wa kiongozi huyo na familia yake uliandaa uwanja wa kuondolewa kwake madarakani na kwa utaratibu huo Suharto akalazimika kujiuzulu.

  Siku kama ya leo miaka 1397 iliyopita sawa na tarehe 29 Jamadu Thani mwaka 36 Hijria kwa mujibu wa baadhi ya wanahistoria akiwemo Ibn Masoudi, vilianza vita vya Jamal kati ya jeshi la Imam Ali AS na kundi la uasi lililokuwa likiongozwa na Talha na Zubeir.

  Kundi hilo lilianzisha uasi huo baada ya kushindwa kustahamili msimamo uliyoonyeshwa na Imam Ali AS wa kutekelezwa uadilifu katika jamii. Kundi hilo hapo awali lilikuwa limekula kiapo cha utiifu kwa Imam Ali AS, lakini likaamua kuasi baada ya kushindwa kufikia malengo yao batili, na kuanzisha vita kwa kisingizo cha kulipiza kisasi cha damu ya Othman bin Affan.

  Na miaka 91 iliyopita katika siku kama ya leo alizaliwa Andrei Sakharov mwanafizikia mashuhuri wa nchini Russia. Sakharov alihitimu masomo yake ya chuo kikuu katika taaluma ya fizikia kwenye Chuo Kikuu cha Moscow na kuanza kujishughulisha na utafiti kuhusu nishati ya nyuklia.

  Mwaka 1975, Andrei Sakharov alitunukiwa tuzo ya Nobel. Hata hivyo miaka mitano baadaye mwanafizikia huyo mahiri alibaidishiwa katika mji wa Gorky jirani na Moscow kutokana na upinzani wake dhidi ya siasa za kikomonisti za utawala wa Umoja wa Sovieti.
   
 2. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa unaposema, "Leo ni Jumatatu tarehe 29 Jamadul Thani mwaka 1433 Hijiria, inayosadifiana na tarehe 21 Mei 2012 Miladia" yani sijakuelewa kabisa kaka naomba msaada wa ufafanuzi zaidi!
   
 3. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
   
 4. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu, lakini naamini inaeleweka vema, hiyo maranyingi hutumiwa kimashariki zaidi hasa ktk zama za kale! Ni lugha ya kiwanazuoni
   
 5. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Yaaaaap moja ya binadamu muhimu sana ktk historia ya dunia hii!
   
Loading...