Kumbukumbu: Mada moto zilizowasha moto na kuzua tafrani.

A JUSTMAN

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
439
555
Wadadisi na wachanganuzi wa mambo wametudokeza kuwa lile sekeseke la polisi kutaka taarifa za baadhi ya member humu ndani kumbe lilitokana na mada nne zilizoletwa humu ndani na mijadala yake kuwa mikali sana.

Eti kumbe ukali wa hizi mada haukuishia tu humuhumu wapi, ulikwenda na kukita mpaka kunako na wahusika walipozipata walijawa na ghadhabu kubwa isiyomithirika wakaapa kuwatafuta wale wote waliozileta humu na kusababisha ziwe hadharani inaezekana kabisa wanataka kulipa kisasi kwa gharama yoyote ile sababu wao wanawachukulia hawa waloleta mada hizi ni kama wabaya wao au maadui.
Wanawachukulia hivyo bila kujali kuhusu ukweli wa kilichomo ndani ya mada hizi, au waleta mada hizi wanajaribu kutaka kusahihisha madudu yanayofanyika katika sekta mbalimbali nchini na hatimaye wahusika wajirebishe na kufanya kazi ipasavyo kwa kujali maslahi ya jamii na taifa zima kwa ujumla.

Ni heri niwakumbushe kuwa daima mtenda udhalimu/muovu yu upande wa hasara zaidi ya yule mtendewa udhalimu.

Nilipotazama mada hizi nikaona ni vema sana nikaziweka pamoja ili iwe kumbukumbu kwa wapendwa sana member wote wa forum hii wanaotumia muda wao kujikita kwenye mijadala yenye kujenga, kukosoa bila kuvunja sheria na kufichua maovu(whistleblower) ili kupata taifa lililo na maendeleo yanayolingana na rasilimali zetu na utajiri wote wa asili tuliojaliwa na Mungu kwa ustawi wa Watanzania pasi kujali matabaka yao, itikadi zao, dini, rangi zao na makabila yao.

Nimezipata mada 3 ile moja nimeshindwa kuipata.

Charles Kimei (CRDB) jiuzulu, kashfa ya kontena, tiketi TFF, wanafunzi na ujambazi CRDB

USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Waziri Charles Kitwanga & Vicky Kamata wanahusika kwenye ufisadi wa kulipwa BOT kwa miaka 6 (Hii mada ilikanushwa na wahusika)

Kampuni ya CUSNA Investment na Madai ya Ukwepaji Kodi (Nimeshindwa kuipata hii mada kulikoni?)


ZAWADI YA WASEMA KWELI KATIKA TAWALA DHALIMU MARA NYINGI HUWA NI KIFO.
 
Back
Top Bottom