Kumbukumbu kutoka Ikulu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,909
30,253
LEO KATIKA KUMBUKUMBU KUTOKA IKULU

Naangalia picha hiyo hapo chini iliyowekwa na Ikulu kama kumbukumbu na kwa hakika imenirudisha nyuma.

Ninapogeuza shingo kuangalia nyuma mimi hupenda kuingia Maktaba kwani humo hupata mengi.

Katika picha hiyo yupo Julius Nyerere, Abeid Amani Karume, Sheikh Thabit Kombo na Rashid Mfaume Kawawa.

Nina kumbukumbu gani za viongozi hawa?

Julius Nyerere, Sheikh Thabit Kombo, Rashid Kawawa maisha yao yanaweza yakasomwa katika kitabu ila Abeid Karume.

Kitabu ndipo mahali pa kusoma kumbukumbu za mtu hata kama zitakuwa hazina ukweli.

Sijapata kuona kitabu cha maisha ya Karume na sijui kwa nini.

Kumbukumbu zangu zinanieleza kuwa Nyerere hakutaka kuandika maisha yake juu ya shinikizo alizokuwa akipata toka kwa watu wake wa karibu.

Lakini zikatokea sababu ikamlazimu Mwalimu aruhusu maisha yake yatiwe katika maandishi watu wasome na mwenyewe alikubali kutoa ushirikiano katika kazi hiyo ya uandishi.

Kitabu cha maisha ya Mwalimu Nyerere kikaandikwa baada ya yeye kufariki.

Kwa bahati waandishi walinihoji kuhusu siku za kwanza za Mwalimu Nyerere alipofika Dar es Salaam na kupokelewa na wazee wangu.

Niliyosoma katika kitabu kilipotoka yamepishana na niliyowaeleza waandishi.

Kwa nini iwe hivi?

Kwa nini Mwalimu hakupenda kuandika historia ya maisha yake na kwa nini baadae akaja kukubali maisha yake yaandikwe?

Kwa nini iwe hivi?

Rashid Kawawa yeye waandishi wawili wameandika maisha yake.

Kwa nini iwe hivi?

Waandishi hawa ni Abeid Hassan Sakara na John Magotti.

Nimesoma vitabu vyote lakini hakuna hata mwandishi mmoja aliyemweleza Simba wa Vita kama anavyostahili.

Kwa nini iwe hivi?

Thabit Kombo ana kitabu lakini kuna mengi ya kutatiza.
Kwa nini iwe hivi?

Karume hajaandikiwa kitabu.
Kwa nini iwe hivi?

Hizi ndizo kumbukumbu zangu ninapoangalia picha hii ya viongozi wetu.

Kumbukumbu kutoka Ikulu imeniingiza katika vitabu vya maisha yao na kunikumbusha historia za hawa viongozi wetu.

MASAHIHISHO
Nimefahamishwa kuwa kipo kitabu cha maisha y Abeid Amani Karume.






Screenshot_20210916-191720_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom