Kumbukumbu: Kauli za Waziri Muhongo kuhusu Umeme

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,818
49,009
(Nimekopi sehemu)

1.Tanzania inakusudia kuanza kuuza umeme nchi za nje kufuatia mapinduzi yanayotazamiwa kufanyika kwenye sekta ya nishati na madini ukiwamo uendelezwaji wa mradi wa uzalishaji umeme katika eneo la Kinyerezi.
�2. Mipango yetu ni kwamba ifikapo mwaka 2014 tayari tutakuwa na umeme wa ziada kiasi cha megawati 500 ambao tutauuza nje ya nchi, ilielezwa jana.
3.Wizara ya Nishati na Madini imebainisha maeneo ambayo inatazamia kuyawekea mkazo ili kuzalisha umeme wa kutosha. Maeneo hayo ni pamoja na uendelezwaji wa nishati ya gesi inayotazamiwa kuanza kuchimbwa mkoani Mtwara pamoja na utumiaji wa makaa ya mawe.
4. shabaha ya Serikali ni kuendelea kukuza uchumi wa taifa kwa kiwango cha kuanzia asilimia 8 na kwamba kiwango hicho kitakuwa kimekuwa hadi kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2015.
�5.Hii mipango yetu itahakikisha tunaondokana na tatizo la umeme na kusema kweli tunakadiria kwamba ifikapo mwaka 2015 tutakuwa na kuwango cha kutosha cha umeme wa ziada, hatua ambayo itatufanya tuuze kiasi kikubwa umeme�
6. kutokana na mipango iliyoandaliwa na Serikali, kuanzia sasa umeme utachukuliwa kama bidhaa ambayo itatafutiwa masoko katika nchi za nje na kuuzwa.
7.Katika hatua nyingine, Shirika la Umeme nchini Tanesco limeingia katika makubaliano na kampuni ya kuzalisha umeme ya China Power Investment kwa ajili ya kuendeleza mradi wa uzalishaji wa umeme katika eneo la Kinyerezi. Mradi huo ambao unaingia hatua ya tatu kati ya nne zilizopangwa utakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme kiasi cha megawati 600.
8.Kwa mujibu wa Waziri Muhongo, kukamilika kwa miradi hiyo ikiwamo usafirishaji wa gesi kutoka mkoani Mtwara kutasaidia kufungua soko la ajira hatua ambayo itakuwa fursa njema. Source mwananchi 2013
CHANZO: NIPASHE

LEO HII

Leo anasimama Mkuu wa nchi anasema tutanunua umeme kutoka nje, anakuwa anatuchanganya.
Je, Megawati 500 za ziada zilizoahidiwa tangu 2013 ziko wapi hadi tunataka kununua Megawati 400 kutoka Ethiopia?? Gesi si tunayo au imeisha?
Kuna mtu anaelewa tunaelekea wapi?
 
Kama maji ya bonde LA kilombero limeshindwa kutunufaisha mengine sahau Muhogo ni muoga kama waogo wengine
 
Miaka mitano itakwisha bado tunatafuta kiwanja cha kujenga kiwanda.
 
Back
Top Bottom