Kumbukumbu Je huu ni ungwana? Mzee Leonard "Mambo“ Mbotela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbukumbu Je huu ni ungwana? Mzee Leonard "Mambo“ Mbotela

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by X-PASTER, Jun 18, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Leo nimemkumbuka Mtangazaji wa enzi hizo kutoka KBC (Kenya) Leonard "Mambo“ Mbotela ni mtangazaji mashuhuri wa redio nchini Kenya. Tulimjua haswa kupitia kipindi chake mashuhuri cha "Je, hii ni ungwana?".


  Na hii ni moja ya clip yake:   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Vile vile alikuwa mtangazaji mzuri sana wa soka michezo wa mpira wa miguu, nikimfananisha na magwiji wa RTD, kama vile Hamed Jongo na Dominic Chilambo.

  Msome hapa moja ya kazi zake enzi hizo, akitangaza soka.

  Kadenge na mpira, Kadenge na mpira, anachenga, moja, anachenga mbili, anakuja katikati, anaenda upande huu, anarudi upande mwingine, anakimbia, anatembea, anatambaa, anamvisha kanzu, anapepeta mpira, amemchenga mchezaji wa kwanza, amempita swipa, anamhepa fullback, mtizame, ndiye huyo, ndiye huyo, anaenda, anaenda, anaangilia huko, anaangalia kule, anatizama kushoto haoni mtu, anatazima kulia, zii mtu, atafanya nini, sasa mwangalie, anaajiitayarisha, anavuta, anapiga teke, anapiga shoot! anapiga shoot! anapiga shoot! mpira umepita moja kwa moja katikati ya miguu ya golkipa maarufu James Siang'a umeiingia ndani na kupasua wavu... wasikilizaji, wananchi, mashabiki, ni....gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooaaaallllllll!!!! gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooaaaallllllll!!!! gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooaaaallllllll!!!! gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooaaaallllllll!!!!

  Tatu Bila!! Mayowe!! Kelele! Mashabiki wa Gor Mahia wamefurahi! Mashabiki wa Abaluhyia wamezirai!  Ah ah ah huyo ndio alikuwa Mzee Leonard "Mambo" Mbotela
   
 3. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #3
  Jun 19, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  X-PASTER ama sijakuelewa ama valuu imekaa mahala pake. Leonard bado nimtangazaji na kipindi chake bado kipo cha Je huu ni ugwana??? Huwa anaingia kati wakati wa kipindi cha "Zinga la Asubhi" wakati Bony Msambi na Cyncia Anyango wakitangaza may be sijaelewa sory but he is still mtangazaji wa Radio Taifa "KBC"
   
Loading...