mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,307
- 6,514
Leo ni siku ya kumbukumbu ya kuungana kwa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar, ambapo wazee wawili wenye hekima walikubaliana na kutekeleza jambo hili.
Katika utawala wa JMK lilifanyika jambo kubwa la kubadili katiba ya 1977 na kutengeneza mpya ambayo kwa kiasi kikubwa ingeshirikisha wananchi wenyewe katika kuiunda.
Katika kuijadili rasimu ya katiba iliyoandaliwa kwa ueledi mkubwa na tume iliyokuwa chini ya mzee Warioba, BMK liliundwa na hakika lilikuwa na mvutano mkubwa wa kihoja hasa katika suala la muundo wa jamhuri ya muungano.
Washindani wa siasa wa CCM wakipendelea muungano wa serikali tatu, na CCM wakitaka muungano wa serikali mbili. Jambo hili liliwaunganisha wapinzani na wakaamua kuunda UKAWA jambo lililofurahiwa na wananchi wengi wa Tanzania.
Bahati mbaya UKAWA wakasusia bunge, kwa sababu ya faulo za waziwazi za CCM, hali iliyopelekea CCM kujiundia katiba inayopendekezwa wao wenyewe.
Tumefikia hapa kwa sasa, mchakato wa katiba umekwama, baadhi ya wa mbili wamehamia kwa wa tatu........ilhali walipinga kipindi kile cha BMK.....na thamani ya UKAWA haionekani tena.....
Je katika kuadhimisha siku hii wewe unakumbuka nini?
Heri ya muungano