Kumbukizi ya maisha ya Maalim Seif imeandikwa na Profesa Ibrahim Haroun Lipumba

Elezea kidogo huo mwaka 1988 kwanin Maalim afukuzwe ccm na sababu zake za kufungwa!
 
1972 maalim alijiunga chuo kikuu alimaliza high school 1963.
"The late karume alikataa wa Zanzibar kwenda kusoma vyuo vikuu"
Walienda baada ya kifo chake.
Wazanzibar wanapolalamikia ukandamizaji hili ni muhimu kukumbuka.
1982 prof anasema kulikuwa na uhaba wa bidhaa Mzee Msuya ana majibu mwalimu alikataa nini.
Tunapo waenzi waasisi wetu tuna mengi yakukumbuka.
 
1972 maalim alijiunga chuo kikuu alimaliza high school 1963.
"The late karume alikataa wa Zanzibar kwenda kusoma vyuo vikuu"
Walienda baada ya kifo chake.
Wazanzibar wanapolalamikia ukandamizaji hili ni muhimu kukumbuka.
1982 prof anasema kulikuwa na uhaba wa bidhaa Mzee Msuya ana majibu mwalimu alikataa nini.
Tunapo waenzi waasisi wetu tuna mengi yakukumbuka.
Shukurani mkuu kwa taarifa yako
 
IMG-20210314-WA0022.jpg
 
Huyu mzee mnafiki sana maana alijiona yeye ndio CUF kumbe marehemu maalim ndio alikua CUF sasa anakula jeuri yake qmaamae chama kimekufa njaa kali ,alitakiwa amuombe msamaha kabla hajafa lakini too late
 
Mtwara wanasema hi ni 'Kuntumia ntu maalufu kuelezea histolia yako ya usomi kidogo'
Kwani mengi yanayoelezwa ni ya Ibra.
 
BURIAN KAKA YANGU MAALIM SEIF
SHARIIF HAMAD

SEHEMU YA TATU.
MAALIM SEIF ALIVYOSHINDA UCHA GUZI MKUU WA ZANZIBAR 1995.

Uchaguzi wa Zanzibar ulifanyika trh 22 Oktoba 1995,Kwa kuwa wapiga kura wote walikuwa chini ya 350000 matokeo yalitarajiwa kutangazwa usiku wa tarehe 22 au asubuhi ya trh 23 oktoba 1995
Baada ya kimya kirefu hatimaye trh 24 Oktoba 1995 ktk milango ya saa 8.00 mchana,mkurugenzi wa uchagu zi aliwaita mawakala wa Wagombea urais,Bwana Mwinyi Mzee, aliyekuwa wakala wa Dr. Salmin Amour, mgombea urais wa CCM, na Bwana Nassor Seif Amour, aliyekuwa wakal a wa Maalim Seif Shariff Hamad,mg ombea Urais wa CUF,Pia alikuwepo Bi Judith Thompson,raia wa Canada, aliyekuwa mshauri wa mambo ya uchaguzi wa ZEC.

Mkurugenzi wa Uchaguzi aliwapa nakala ya matokeo ya uchaguzi huo mawakala yaliyoonyesha Mgombea wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, ameshinda kwa kupata kura 166,522 sawa na asilimia 51.4 ya kura zote halali zilizopigwa,ukilinganisha na kura 157,351 alizopata mgombea wa CCM Dr Salmin Amour Juma.

Kituo cha televisheni cha DTV kiliya pata matokeo hayo na kuyatangaza,
Baada ya taarifa ya Mkurugenzi wa zec kupokelewa na ccm,Naibu katibu mkuu wa CCM upande wa Zanzibar, Bwana Ali Ameir Mohamed aliandika barua zec kupinga matokeo na kudai uchaguzi urudiwe kwa sababu hauku wa huru na wa haki.
Kabla ya ZEC kutoa majibu yoyote kwa barua iliyoandikiwa,ZEC ilipokea shinikizo jipya kutoka ccm na vyombo vya dola kumtangaza Dr. Salmin Amour Juma kuwa ndio mshindi wa uchaguzi wa Rais Zanz na ilifanya hivyo.

Alhamisi trh 26 oktoba barozi Kari
Karanko wa Finland aliyekuwa anaon goza Tume ya Waangalizi wa uchagu zi wa Umoja wa Mataifa (United Nations Election Observation Team) aliieleza ZEC kuwa kulikuwa kuna makosa ya wazi kati ya matokeo toka kwenye vituo vya kupigia na kuhesabia kura,na yale yaliyotanga zwa na ZEC,Alishauri uapishaji wa Rais usifanyike mpaka hapo hitilafu hii itakaporekebishwa.
Na ZEC waliukataa kata kata ushauri wake.

Ripoti ya Jopo la Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa International (Election Observation Team,Zanzibar Observation Report) iliweka bayana wizi wa kura uliofanywa na CCM.
Kwa mfano jimbo la Kwahani wataza maji wa Kimataifa walishuhudia kuhesabiwa upya kwa kura za Rais, uwakilishi na udiwani,kwa upande wa Rais,Mgombea wa CUF alipata kura 2792, na Mgombea wa CCM alipata kura 2775, na kura 61 ziliharibika,Matokea haya yalifanana na yale ya aliyekuwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Mlandege.

Hata hivyo ZEC ilitangaza kuwa Mgombea wa CUF amepata kura 2319 na mgombea wa ccm amepata kura 3248.
Taarifa ya Zanzibar Election Monitoring Group (ZEMOG) iliainisha mapungufu makubwa ya mchakato wote wa uchaguzi wa Zanzibar wa 1995. Baada ya kupokea Taarifa mbalimbali,mabolizi 14 toka nchi zinazoendeshwa kwa kufuata mising ya demokrasia walitoa taarifa yao trh 21 Novemba 1995 ambayo nainukuu:-

“The International Observation team has found serious discrepancies in the compilation of the votes for the Presidency. The figures announced by the Zanzibar Electoral Commission do not always correspond with the figures recorded at the polling stations. A reconciliation could alter the outcome of the Presidential Elections”
Kwa kiswahili kisicho rasmi, taarifa ya mabalozi hao ilikuwa kama ufuatavyo:

Watazamaji wa Kimataifa wamebaini mapungufu makubwa ya ujumlishaji wa kura za Rais,Kura zilizotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar hazifanani kabisa na kura zilizohesabiwa kwenye vituo vya kura,Uhakiki na uthibitishaji wa kura hizi unaweza ukabadilisha matokeo ya Uchaguzi wa Rais’.
Hii ilikuwa lugha ya kidemokrasia kueleza kuwa CCM wameiba kura. Kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imemtangaza aliyeshindwa kuwa ndiye mshindi wa Uchaguzi katika

Uchaguzi wa 1995, CUF ilitangazwa mshindi katika majimbo ya uwakilishi 24 yakiwemo majimbo yote 21 ya Pemba,na majimbo 3 ya Unguja.CCM walitangazwa wameshi nda majimbo 26 yote yakiwa yako Unguja.
Kwa sababu ya Chama kudhulumiw a kiti cha Urais wa Zanzibar,wawakili shi wa CUF waliamua kutoingia na kushiriki shughuli za Baraza la wawa kilishi.

Kwa kuzingatia mazingira yaliyokuw epo,Mwalimu Nyerere alishauri kuwa kwa matokeo yaliyotangazwa ya uchaguzi wa Zanzibar,ni vyema ikau ndwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
CCM na Dr Salmin Amour hawakuu kubali ushauri huo,katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Chief Anyaoku alichukua jukumu la kusuluhisha mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar na Muwakilishi wa Chief Anyaoku alika milisha mazungumzo na pande zote na kufikia Muafaka uliowekwa saini Zanzibar Juni 9 1999.

Maalim Seif alinikaribisha nihudhurie sherehe hizo zilizofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa wakati huo,Nilistuka nilipoona kuwa Dr Salmin hashiriki sherehe hizo.
Mtia Saini wa CCM alikuwa muwakili shi mmoja mchekeshaji almaarufu Fadau ambaye hivi sasa ni marehem,
haikuwa dalili nzuri.
Muafaka huo uliitaka CUF imtambue rasmi Dr Salmin Amour kuwa Rais halali wa Zanzibar, na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CUF washiriki kikamilifu katika shughuli za Baraza.

CUF ilikamilisha masharti yote ya Muafaka wa Jumuiya ya Madola.
Kwa upande wao CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilitakiwa kufanya marekebisho ya sheria ili kuhakikisha kuwa Uchaguzi wa 2000 unakuwa huru na wa haki.
Marekebisho hayo yalikuwa ni pamo ja na kuanzishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi, na kurekebisha sheria za Mahakama ili kuhakikisha kuwa mahakama zinakuwa huru katika utendaji na utoaji wa maamuzi.
Aidha vyombo vya habari vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar vilitakiwa visipendelee chama chochote katika kurusha habari za kisiasa.

Kwa upande wake vyombo vya usalama vya dola na hasa Polisi, vilitakiwa kutenda haki kwa vyama vyote bila upendeleo.
Katika sherehe ya kuweka saini Muafaka baina ya CCM na CUF, Maalim Seif wakati huo akiwa Makamu Mwenyekiti wa CUF, alitoa hotuba nzuri iliyoonyesha kuwa yeye ni Mzanzibari Mzalendo yuko tayari kusamehe yaliyopita. Pamoja na kumshukuru Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola alisema,napenda pia kutoa shukrani maalum kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi.

Hekima na mwelekeo wa kisiasa ulioonyeshwa na Kamati Kuu ya CCM katika kuonyesha njia iliyofikia mwafaka huu ni jambo linalostahiki pongezi za dhati. Naiomba Kamati Kuu ya CCM ipokee salamu zetu hizo. .... Utiaji saini wa mwafaka huu ni kielelezo halisi chenye kudhihirisha wazi sifa nzuri za watu wetu; na pia kuweka bayana nia ya kumaliza mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar, kwa njia ya amani.

''Hali hii inatoa fundisho zuri katika hali nzima ya umalizaji migogoro kwa njia za amani. Nchi nyengine katika Bara la Afrika zinaweza kujifunza kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaweza kuepushwa, endapo vyama vinavyopingana vitaonyesha uvumilivu wakati wa machungu makubwa ya kuitafuta suluhu kwa njia ya majadiliano.
CCM na serikali ya Mapinduzi Zanzibar hawakutekeleza kabisa makubaliano ya Muafaka wa Jumuiya ya Madola. Hali hiyo ilijenga mazingira ya mgogoro mkubwa zaidi kwenye Uchaguzi wa mwaka 2000.
 
SEHEMU YA NNE:
KUCHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA TAIFA NA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KUWA KATIBU MKUU - CUF

Niliporejea nchini mwaka 1998 kutoka Helsinki niliendelea na shugh uli za utafiti na ushauri wa mambo ya uchumi nchi za nje.
Miongoni mwa shughuli nilizofanya ilikuwa ni pamoja na kwenda nchini Swaziland kuishauri Wizara ya Fedha ya nchi hiyo namna ya kuimarisha sera zake,kwa lengo la kukuza uchumi na kuwa na utulivu katika uchumi mpana. Aidha nilifanya ushauri kama huo kwa Wizara ya Fedha nchini Namibia.

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa lina kitengo kinachoandaa taarifa ya kila mwaka ya Maendeleo ya Watu (Human Development Report). Niliteuliwa kushiriki katika maandalizi ya taarifa ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 1999 iliyojikita katika suala la Utandawazi na Maendeleo ya Watu–Globalization With a Human Face. Nilifanya utafiti na kuandaa mada kuhusu Utandawazi na Maendeleo ya nchi za Kiafrika – Globalization and Economic Development of African Countries.
Na nilikwenda New York kushiriki katika vikao vya kuandaa taarifa hii.

Sikupata fursa ya kufanya shughuli za kiushauri nchini Tanzania. Hali ya kisiasa ilikuwa ya kuwaona Viongozi wa Vyama vya Upinzani kama maadui. Mazingira yaliyokuwepo yalisababisha pia kupoteza marafiki zangu wa Chuo Kikuu. Nakumbuka kuna wakati nilikuwa nakwenda kufanya utafiti Maktaba ya Repoa (Research for Poverty Alleviation), wakati huo ikiwa karibu na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi wake ambaye tulikuwa pamoja Chuo Kikuu alinikaribisha vizuri. Kwa kuwa nilikuwa nafanya utafiti, karibu kila siku nilikuwa nakwenda kwenye maktaba hiyo.

Katika hali ya kushangaza sana Mkurugenzi wa Repoa aliwekwa ‘kiti moto’ na Mwenyekiti wa Bodi yake kwa hoja kwamba alikuwa anaigeuza Repoa kuwa ofisi ya CUF. Ilinibidi niache kutumia Maktaba ya Repoa.
Profesa Helleiner ambaye mwaka 1995 aliongoza timu ya Wataalam walioishauri serikali kuhusu sera za kuimarisha uchumi na kuwa na mahusiano mema na Washirika wa Maendeleo, alikaribishwa nchini mwaka 1998 kuja kuendelea kutoa ushauri. Shirika la Maendeleo la Denmark liligharamia ziara yake. Kwa kuwa mimi nilishiriki katika timu hiyo mwaka 1995, Profesa Helleiner aliniomba niungane naye alau nimpe ushauri wangu. Balozi wa Denmark wa wakati huo alimfahamisha Prof. Helleiner kuwa Serikali haitafurahia jambo hilo. Pamoja na hayo Profesa Helleiner alikuja kunitembelea nyumbani kwangu Sinza, tukashiriki wote chakula cha jioni.

Kufukuzwa kwangu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutopewa fursa za kufanya kazi za ushauri nchini Tanzania hakukuniathiri kitaaluma. Nilipata fursa nyingi nje ya nchi. Katikati ya mwaka 1999 kulifanyika chaguzi ndogo katika majimbo ya Temeke na Ubungo. CUF iliingia katika chaguzi hizo ndogo na mimi nikapewa jukumu la kuongoza kampeni za Ubungo na Temeke. Kila siku tulifungua matawi ya CUF asubuhi, na kufanya mikutano ya hadhara jioni.

Katika Uchaguzi mdogo huo, Tambwe Hiza alikuwa Mgombea wa CUF jimbo la Temeke, Hussein Mmasy alikuwa Mgombea wa CUF katika jimbo la Ubungo. Kampeni zilifana sana. Vijana walijitolea na kukodi malori (Fusso) kwenda kwenye mikutano ya hadhara iliyokuwa na hamasa kubwa. Marehemu Tambwe Hiza alikuwa na kipaji cha kuhutubia na kuchekesha. Salama Masoud, wakati huo bado kijana mdogo - nadhani alikuwa bado anasoma - alikuwa mshehereshaji wa jukwaa katika kampeni za Temeke. CUF ilikuwa tishio kubwa. Kila siku ya kampeni, Wananchi – wafuasi wa CUF - walikamatwa na kuwekwa ndani. Naamini tulishinda chaguzi ndogo za Ubungo na Temeke, lakini kama kawaida CCM na dola walicheza rafu. Nadhani hofu kubwa ya CCM ilikuwa kuitangaza CUF kuwa imeshinda uchaguzi wa majimbo mawili ya Dar es Salaam, wakati tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2000. Vyombo vya Dola vilitumiwa kuhakikisha Wagombea wetu hawatangazwi kuwa wameshinda.

Nakumbuka baada ya kumalizika kwa chaguzi hizi ndogo niliondoka kwenda Uganda kushiriki Kongamano la Wachumi. Tukiwa Uganda tulipata fursa ya kutembelea Jinja kwenye chanzo cha mto Nile. Katika ziara hiyo nilikutana na Jaji Agostino Ramadhan, wakati huo akiwa Makamo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Nadhani alikuwa amekwenda kwenye Mkutano wa Majaji nchini Uganda. Aliponiona alistuka. Aliniambia ‘wewe unatusumbua sana Dar es Salaam, lakini bado unapata muda wa kufanya shughuli nyingine, na Uganda upo?
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF wakati huo, Mzee Musobi Mageni, aliamua kustaafu na akaniomba nigombee Uenyekiti. Makamo Mwenyekiti Maalim Seif na Katibu Mkuu, Mzee Shaabani Khamis Mloo, waliunga mkono pendekezo hilo kwa kuzingatia hamasa kubwa ya vijana wakati wa mikutano yangu. Mimi sikuwa na shauku kubwa lakini nilikubali.

Mkutano Mkuu wa Chama wa kuchagua viongozi wa kitaifa wa CUF uliandaliwa kufanyika mwishoni mwa Novemba 1999. Kabla ya Mkutano Mkuu niliomba orodha ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tanzania Bara. Nilibaini hakukuwa vijana wowote wa Profesa Malima katika hiyo orodha. Walionishawishi nigombee Urais hawakuwa wamejitokeza kushiriki waziwazi ktk siasa za CUF. Hakuna hata mmoja aliyekuwa mjumbe wa mkutano Mkuu wa Chama. Baadhi yao walikuwa wanafanya kazi Serikalini au kwenye Mashirika ya Umma. Nilielewa kuwa wasingeweza kushiriki kwenye siasa moja kwa moja. Kilichonipa tabu ni kwamba hata hivyo hawakuhangaika kuhakikisha kuwa CUF inapata wajumbe wengi wa mkutano mkuu wenye uwezo wa kushika nafasi za kiutendaji ndani ya Chama, na kuzifanya vizuri.

Katika hali hii niliamua bora nisigombee nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, na badala yake niendelee na shughuli zangu za utafiti na ushauri. Niliandika barua kwa Katibu Mkuu kuwa sintagombea nafasi ya uenyekiti wa Taifa. Chama kilituma ujumbe wa watu watatu kuja kuzungumza na mimi, ukiongozwa na Marehemu Ali Haji Pandu. Wajumbe wengine walikuwa Wilfred Lwakatare na Mzee Mbelwa. Walikuja nyumbani kwangu Sinza kunisihi nigombee nafasi ya Uenyekiti. Nakumbuka Lwakatare alitumia ‘gia’ ya kuwa ‘alau ukae kwa miezi sita ili tujipange’. Niliwaomba wanipe muda ili niweze kutafakari.

Hatimaye nilikubali kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa. Mzee Mloo na Maalim Seif walibadilishana nafasi. Mzee Mloo aligombea wadhifa wa Makamo Mwenyekiti, na Maalim Seif wadhifa wa Katibu Mkuu.
Baada ya Uchaguzi wa Chama wa mwaka 1999, nilianza ziara ya kutembelea mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar. Mzee Mloo alishauri nianze ziara mikoa ya kusini. Nilianza ziara Mkoa wa Lindi. Hata hivyo mikutano yangu ya hadhara iliwekewa vizingiti vingi. Tarehe 31 Desemba 1999 nilipokuwa Lindi Mkutano wangu wa hadhara uliokuwa umepangwa kufanyika jioni ulizuiliwa na polisi kwa kisingizio kuwa wananchi wa Lindi walikuwa wanajiandaa na sherehe za mwaka mpya na kuipokea karne ya 21! Tulipoteza siku nzima katika mazungumzo na hatimaye aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, mtani wangu,Marehemu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, aliwaeleza Polisi wasizuie mkutano.tulianza kutangaza mkutan huo saa 09:00 alasiri na kufanya mkutano saa 11 jioni.

Newala tulizuiliwa kufanya Mkutano wa hadhara kwa kisingizio kuwa Taarifa ya mkutano imewafikia Polisi chini ya saa 48 kabla ya tukio. Tuliamua tufanye mkutano wa ndani. Tulikodi Ukumbi wa Chuo. Gari ya matangazo ilipoanza kutangaza mkutano wa ndani, ilizuiwa na polisi na kuelezwa kuwa mkutano wa ndani hautangazwi kwa kipaza sauti! Afisa Mfawidhi (OCD) wa Polisi alitueleza kuwa taarifa ya mkutano wa ndani inapaswa kupelekwa kwa wahusika kwa barua na siyo kwa kuwatangazia kwa kipaza sauti. Kwa sababu ya hivyo visingizio hatukuweza kufanya huo mkutano wa ndani.
Mkutano wetu Mtwara mjini ulikuwa ufanyike trh 10 Januari 2000 ulizuiw a na Polisi kwa kisingizio kuwa ktk wiki ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, majeshi yote yalikuwa 'standby.

Nilipomuona Mkuu wa Mkoa,Nsa Kaisi anisaidie alinijibu kuwa yeye hana madaraka juu ya Polisi Mkoani kwake.
Alinieleza kwamba mtu anayeweza kuingilia kati ni IGP na maafisa wa juu wa makao makuu ya polisi. Alinieleza kuwa Mtwara ilikuwa na matatizo ya kiusalama kwani haikuwa inawezekana kutofautisha kati ya Mmakonde au Mmakua wa Msumbiji, na Mmakonde au Mmakua wa Tanzania! Utadhani Msumbiji na Tanzania hazikuwa nchi marafiki.
Wakati tunazuiwa kufanya mikutano ya hadhara mkoani Mtwara, Mzee John Malecela, Makamo Mwenyekiti wa CCM, alikuwa anafanya mikutano ya hadhara mkoani Tabora.

Nilitembelea mikoa yote ya Tanzania isipokuwa Rukwa. Sikuweza kutembelea Rukwa kwani nilipofika Kigoma Julai 2000, Polisi walianza kuzuia mikutano ya hadhara kwa kisingizio kuwa kampeni hazijaanza pamoja na kwamba sheria namba 5 ya Vyama vya Siasa ya 1992, haizuwii kufanyika mikutano ya vyama muda wowote ule, kwa ajili ya kuelezea sera za chama na kusaka wanachama wapya. Nadhani hofu kuu ya CCM ilikuwa ni kuona jinsi Wananchi wa Tanzania walivyokuwa wanaitikia kaulimbiu ya CUF ya Haki Sawa kwa Wananchi wote,Na nia yetu ya dhati ya kujenga uchumi imara utakaoleta neema kwa wote, CUF ilikuwa tishio katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000.
 
SEHEMU YA TANO
UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2000 ZANZIBAR.
Baada ya Uchaguzi wa 1995, hali ya kisiasa Zanzibar ilikuwa tete sana Wanachama wa cuf na viongozi 18 walikamatwa mwishoni mwa 1997 na mwanzoni mwa1998 na kufunguliwa kesi ya uhaini ya kutaka kuipindua serikali ya Zanzibar.
Kati ya hao waliokamatwa ni pamoja na Mzee Machano Khamisi Ali, Juma Duni Haji, Hamadi Rashid Mohamed, Hamadi Masoud Hamadi, Nassor Seif Amour, Hamad Mmanga, Bi Zulekha Ahmed Mohamed, na Bi Zeina Juma Mohamed.
Mwaka 1999 na 2000 nilijitahidi kwenda kuwatazama watuhumiwa wakiwa Mahabusu kila Zanzibar.

Pamoja na muafaka wa CCM na CUF uliofikiwa chini ya upatanishi wa Jumuiya ya Madola, na kuwekwa saini Juni 1999, Mzee Machano na wenzake hawakuachiwa kwa kisingizio kuwa hilo ni suala la kuamuliwa na Mahakama,mara tu
baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 waaliachiwa huru.
Katika hukumu yake,Jaji Agostino Ramadhan alieleza kuwa washitakiwa hawawezi kufanya kosa la uhaini wa kupindua serikali kwa kuwa Zanzibar haikuwa dola huru (Sovereign State) inayoweza kupinduliwa.

Katika kipindi chote hicho tangu baada ya Uchaguzi wa 1995 Maalim Seif aliishi zaidi Dar es Salaam, makazi yake yakiwa Hoteli ya Star Light. Hata hivyo alifanya ziara za mara kwa mara Pemba na Unguja, kuhamasisha umma.
Ndani ya CCM kulikuwa na mvutano. Dr Salmin Amour alitaka agombee tena Urais. Mara ya kwanza alichaguliwa kuwa Rais mwaka 1990 wakati wa mfumo wa Chama kimoja.

Katika mfumo wa Vyama vingi alikuwa amekuwa Rais kwa kipindi kimoja tu. Kwa sababu hiyo aliona ana haki ya kugombea kipindi cha pili. CCM na Mwalimu Nyerere walipinga wazo la Dr Salmin kugombea mara ya tatu, kwa hoja kwamba ilikuwa ni uvunjaji wa Katiba. Dr Salmin aliukejeli msimamo wa Mwalimu Nyerere kwa kusema “Hakuna cha Baba wa Taifa, wala Babu wa Taifa.” Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dr Omari Ali Juma, naye alimpiga kijembe Dr Salmin kwa kusema: “usisubiri mpaka upigwe mawe ndiyo ujue hupendwi.”

Hatimaye CCM waliweza kumdhibiti Dr Salmin Amour na kumzuia kupata fursa ya kugombea Urais kwa mara ya tatu.
Kwa mujibu wa katiba ya CCM utaratibu wa kumteua Mgombea wa Urais wa Zanzibar unaanza kwa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Zanzibar “Kufikiria na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho, juu ya Wanachama wanaoomba nafasi ya Rais wa Zanzibar.” Uteuzi wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM inapokutana mjini Dodoma.

Kwa kuzingatia utaratibu waluojiwekea, katika kura za maoni CCM Zanzibar walimchagua Dr Mohamed Gharib Bilal, aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Dr Salmin, kwa zaidi ya theluthi mbili ya kura zote, kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Amani Abeid Karume ambaye hatimaye alikuja kuwa Mgombea wa Urais wa Zanzibar alikuwa mtu wa tatu. Alipata kura kiduchu, chini ya asilimia 13 ya kura zilizopigwa.

Pamoja na CCM Zanzibar kupiga kura za kumkataa Karume, Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma ilimteua kuwa Mgombea wa CCM. Wana CCM wa bara ndiyo waliomteua Amani Karume kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar. Dr Salmin alinuna, hakufurahia uteuzi huo. Maalim Seif alikuwa na nafasi nzuri ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa 2000. Wakati Amani Karume hakuwa chaguo la wana CCM wa Zanzibar, Maalim Seif aliaminiwa na hata baadhi ya wana CCM kuwa ni mtetezi wa Wazanzibari.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa CCM waliendelea kutoa kauli kabla ya uchaguzi kwamba hawatatoa utawala kwa vipande vya karatasi. Katika mikutano yake ya kampeni Zanzibar, Rais Mkapa aliyekuwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano, alitamka hadharani kuwa hayuko tayari kukabidhi serikali kwa chama kisichokuwa na asili ya Afro-Shirazi na TANU!
Maana ya kauli hii ilikuwa, bila kujali matakwa ya Wazanzibari walio wengi, viongozi wa CCM wangeendelea kubakia madarakani kwa sababu CCM ndio iliyokuwa na asili ya ASP na TANU.

Chama cha CUF kilifanya kampeni za kusisimua. Nilishiriki kwenye uzinduzi wa kampeni kumnadi Maalim Seif. Nilieleza nilivyokutana na Maalim msikitini Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na uwezo wake mkubwa kitaaluma na uelewa wa mambo.
Nakumbuka Ismail Jussa kuniambia kuwa nilikuwa nimemnadi vizuri sana Maalim Seif, kuliko hata walivyofanya Wazanzibari. Ismail Jussa na aliyekuwa Meneja wa Kampeni, mheshimiwa Awadhi, pia walifanya kazi nzuri ya kumuelezea Maalim Seif kwa Wazanzibari.
Mwaka 2000 tulikuwa na mtandao mzuri wa Chama Zanzibar yote na uwezo wa kulinda kura zetu.
Uchaguzi wa Zanzibar na ule wa Jamhuri ya Muungano ulifanyika siku moja; tarehe 29 Oktoba 2000. Baada ya CCM kuona inashindwa vibaya polisi waliamriwa wachukue masanduku ya kura kwa nguvu.
Utekelezaji wa zoezi hilo ulivuruga kabisa uchaguzi. Ili kuwatisha wananchi polisi walifanya ukatili mkubwa mitaani na kwenye makaazi ya watu.

Timu za Watazamaji wa Ndani na wa Kimataifa wa Uchaguzi wa Zanzibar, zilishauri uchaguzi wa Zanzibar ufutwe na uchaguzi mpya ufanyike baada ya kuifanyia marekebisho Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Jumuiya ya Madola ambayo ilikuwa mpatanishi wa CCM na CUF baada ya Uchaguzi wa 1995 ilituma timu nzito ya watazamaji wa uchaguzi iliyoongozwa na Dr. Gaositwe Chiepe, ambaye alipata kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Botswana.

Katika barua yake kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kuwasilisha Taarifa ya Watazamaji Dr. Chiepe alieleza:-
“ in our view, on the evidence of polling day, these elections should be held again, in their entirety, but not until the existing election management machinery has been reformed from top to bottom. .…
"It was a cause of great sadness to us that we had to come to such a conclusion. We would have been overjoyed should the Zanzibar Electoral Commission have been able to rise to the occasion. As it was, either because of incompetence or a deliberate wrecking attempt – we are still not sure which – this election fell far short of minimum standards.”
Kwa tafsiri isiyo rasmi, maelezo ya Dr Chiepe yalikuwa kama ifuatavyo:

“Kwa maoni yetu, kwa kuzingatia ushahidi tuliouona siku ya kupiga kura, Uchaguzi wote urudiwe, lakini iwe ni baada ya kuifanyia marekebisho Taasisi inayosimamia Uchaguzi toka juu mpaka chini. .. “Tunasikitishwa sana kufikia hitimisho hilo. Tungefurahi sana kama Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ingeweza kusimamia uchaguzi ipasavyo. Hata hivyo haikuwa hivyo. Ama kwa kukosa uwezo, au kwa sababu za maksudi za kuvuruga – hatuna uhakika ni lipi – uchaguzi huu umeshindwa kufikia viwango vya chini kabisa.”

Taarifa ya Jumuiya ya Madola ilihitimisha:-
“The people of Zanzibar turned out in large numbers to vote in their second multi-party democratic elections since independence, waiting in long queues for hours and generally remaining peaceful and orderly. We commend them for their extraordinary patience, maturity and dignity.

Unfortunately, the conduct of the elections fell far short of minimum standards. The failure to deliver ballot papers, which prevented some stations from opening until very late and disrupted voting even at those which had opened, was so serious that it led to the cancellation of the election in 16 constituencies, representing more than 40 % of the registered voters, and the suspension of election operations and removal of ballot boxes in the other 34 constituencies.

"The cause was either deliberate manipulation or gross incompetence. Since their announcement ZEC have themselves indicated that there might have been other, possibly very serious shortcomings, which are being investigated by the police.
"The Group believes that only a properly conducted and fresh poll, throughout Zanzibar, undertaken by a Commission reformed in line with international good practice, with its independence guaranteed in both law and practice, and a restructured and professional Secretariat, can create confidence in and give credibility to Zanzibar’s democracy.”

Kwa tafsiri isiyo rasmi ripoti ya Jumuiya ya Madola ilihitimisha kama ifuatavyo:
“Wananchi wa Zanzibar walijitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi wa pili wa Vyama vingi tangu kupata uhuru. Walisubiri kwenye mistari mirefu kwa saa nyingi kwa amani na utulivu.
Tunawapongeza kwa ustahamilivu wao, ukomavu wao na heshima yao.
“Kwa bahati mbaya, uendeshaji wa uchaguzi haukufikia hata viwango vya chini kabisa. Karatasi za kupigia kura hazikufikishwa kwa wakati na kusababisha baadhi ya vituo vya kupigia kura kuchelewa sana kufunguliwa, na kuvuruga upigaji kura katika vituo vilivyofunguliwa.

‘Kasoro hizi zilikuwa nyingi na kusababisha Tume kufuta Uchaguzi wa majimbo 16 yenye zaidi ya asilimia 40 ya wapiga kura walioandikishwa, na kusitisha shughuli za uchaguzi na kuondoa masanduku ya kura katika mjimbo mengine 34. Sababu ya matukio haya zilikuwa ni ama za maksudi, au kutokana kukosa uwezo kabisa wa kuendesha uchaguzi. Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imedokeza kuwepo kwa matatizo makubwa yanayochunguzwa na polisi.

"Watazamaji wote wa uchaguzi wanaamini kuwa Zanzibar yote inapaswa kuwa na uchaguzi mpya, utakaosimamiwa na Tume iliyofanyiwa marekebisho, yenye uwezo wa kusimamia uchaguzi kwa viwango vinavyokubalika kimataifa. Tume iwe huru kisheria na kwa vitendo; na iwe na Sekretariati yenye uwezo na weledi ili kurejesha imani, na kuipa uhalali demokrasia ya Zanzibar.”
Watazamaji wa uchaguzi wa ndani TEMCO, walikuwa na msimamo kama ule wa Watazamajiwa Jumuiya ya Madola.
Taarifa yao ya awali ilieleza:-

“TEMCO observers were able to monitor the campaigns, voting and vote counting in some parts of Zanzibar. The eagerness of the Zanzibar people to cast their votes on October 29, 2000 was unprecedented; most polling stations or centers were full of anxious voters by 6.00 am or earlier, and most of them remained in their queues for as long as it took for the election officials to get ready. … This showed that the ordinary people of Zanzibar are on the side of democracy.
“However, considering the events that took place on Sunday 29th and Monday 30th October, 2000, we can not but conclude that those state instruments responsible for managing the elections in Zanzibar have let down the people and the multi party democracy which we are trying to nurture in Tanzania and Africa.

“We note with concern that all …important and delicate decisions have been made by ZEC without consultation with the main stakeholders, namely the contending parties. True, ZEC has the legal authority to postpone or cancel an election, to set a new date for a cancelled election, and to make a temporary stoppage of the vote counting process. However, some legal requirements have been violated by ZEC action, for example the participating parties, candidates and their agents have been denied their legal rights to ensure that the ballots remain secure until the votes are counted. In the case of Pemba, ballot boxes were forcibly seized by police against the will of the party agents and sent to district ZEC offices which are inaccessible to party agents.

"On Monday 30th October 2000 a most shameful episode took place at Darajani area in Zanzibar. A state force consisting of ordinary police, state security people, the special field force unit (FFU), etc, descended on a group of CUF supporters who were peacefully singing songs of praise to their party and leaders following a press statement by the CUF Zanzibar Presidential candidate, Mr. Seif Shariff Hamad.

"These CUF supporters – men and women, young and old – were beaten up most mercilessly and handled in a manner which, to an observer, would suggest that the state instruments of law and order were carrying out a vengeance rather than performing ordinary arrests.

"Looking at the election process as a whole, from registration of voters to the Sunday 29th voting fiasco in the Urban West Region and other parts of the Isles; and considering the degree of distrust of state authorities (ZEC, police, state media, and the Salmin Amour administration as a whole) which currently exists in Zanzibar, TEMCO believes that the solution is to cancel the elections in Zanzibar in totality and to organize fresh elections. This would also provide an opportunity to review the weaknesses of the state instruments involved in the electoral process, to involve the political parties more closely in decision-making, and to begin a process of national healing and reconciliation. A rush solution may create more problems than it solves.”
Kwa tafsiri isiyo rasmi taarifa ya TEMCO ilikuwa kama ifuatavyo:-

“Watazamaji wa TEMCO walifuatilia kampeni, upigaji kura na kuhesabu kura maeneo mbalimbali ya Zanzibar. Kulikuwa na hamasa kubwa ambayo haijapata kutokea ya wananchi wa Zanzibar kujitokeza kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2000.
"Wananchi wengi walikuwa kwenye vituo vya kupiga kura tangu saa 12 asubuhi au mapema zaidi. Walisubiri kwenye mistari ya wapiga kura kwa muda mrefu mpaka wasimamizi wa uchaguzi walipokamilisha taratibu. Hii inaonyesja jinsi wananchi wa Zanzibar wanavyounga mkono demokrasia.

"Hata hivyo ukizingatia matukio ya jumapili tarehe 29 na Jumatatu tarehe 30 Oktoba 2000, hatuna jinsi zaidi ya kufikia hitimisho kuwa vyombo vya dola vilivyopewa jukumu la kusimamia uchaguzi Zanzibar vimewaangusha wananchi, na demokrasia ya vyama vingi tunayojaribu kuijenga Tanzania na Afrika.

“Tumeshuhudia kwa masikitiko maamuzi yote nyeti yaliyoamuliwa na ZEC bila kuwashirikisha wadau wakuu ambao ni vyama vinavyoshindana katika Uchaguzi. Ni kweli ZEC ina mamlaka ya kisheria ya kuahirisha au kufuta uchaguzi, kupanga tarehe mpya ya uchaguzi uliofutwa, na kusimamisha kwa muda mchakato wa kuhesabu kura.

“Hata hivyo ZEC imekiuka taratibu za kisheria. Kwa mfano, Vyama vya siasa vinavyoshiriki kwenye Uchaguzi, wagombea na mawakala wao wamenyimwa haki ya kuhakikisha kuwa kura zilizopigwa zinakuwa salama mpaka zitakapohesabiwa.
"Kisiwani Pemba, Polisi walichukua kwa nguvu masanduku ya kura bila mawakala kuridhia na kuyapeleka ofisi za wilaya za ZEC ambako mawakala wa vyama hawawezi kuyafikia na kuyaona.

“Jumatatu ya tarehe 30 Oktoba, tukio la aibu sana lilitokea eneo la Darajani, Zanzibar. Vikosi vya dola wakiwemo polisi wa kawaida, Usalama wa Taifa, na FFU waliwavamia na kuwapiga vibaya wanachama na wapenzi wa CUF waliokuwa wanaimba kwa amani nyimbo za Chama na kuwasifia viongozi wao, baada ya Mgombea wa Urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuzungumza na waandishi wa habari.

'Kwa mtazamaji wa kawaida, vitendo vya vyombo vya dola vilikuwa vya kulipiza kisasi na sio vya ukamataji wa kawaida wa wananchi wanaotuhumiwa kufanya makosa.
“Ukiutazama kwa ujumla mchakato wa Uchaguzi, toka uandikishaji wa wapiga kura mpaka sintofahamu iliyojitokeza kwenye uchaguzi wa tarehe 29 Oktoba katika Mkoa wa Mjini Magharibi na maeneo mengine ya Zanzibar; na ukizingatia kutoaminika kwa hali ya juu kwa mamlaka za dola (ZEC, polisi. Vyombo vya habari vya serikali, na Utawala wa Salmin Amour kwa ujumla wake), TEMCO inaamini kuwa suluhisho ni kufuta Uchaguzi wote wa Zanzibar na kuandaa uchaguzi mpya.
"Utaratibu huu utatoa fursa ya kutathmini udhaifu wa vyombo vya dola vinavyosimamia uchaguzi, kushirikisha vyama vya siasa kwa karibu katika maamuzi na kuanza mchakato wa kuponya majeraha na kuleta maridhiano ya kitaifa. Kutafuta ufumbuzi wa haraka kutasababisha matatizo makubwa zaidi.”

Chama chetu kilikubaliana na ushauri wa watazamaji wa Jumuiya ya Madola na TEMCO wa kufutwa uchaguzi wote; na kuandaliwa uchaguzi mpya ambao ungesimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na CCM waliupuuza ushauri huo. ZEC ilitangaza kurudiwa uchaguzi katika majimbo 16 ya Mkoa wa Mjini Magharibi siku ya tarehe 5, Novemba 2000.
Chama cha CUF kilikataa kushiriki katika Uchaguzi huo kwa sababu matokeo yangekuwa ya kupanga, hasa ukizingatia kuwa masanduku ya kura ya majimbo 34 yalikuwa mikononi mwa Tume bila chama chetu kujua kilichokuwa kinafanyika kwenye masanduku hayo.

ZEC ilidhihirisha wazi haina uwezo wa kusimamia uchaguzi huru na wa haki.
Baada ya uchaguzi wa Novemba 5, 2000 bila haya CCM walijitangazia ushindi wa kishindo. Haukuwa ushindi wa kishindo bali ulikuwa wizi wa kishindo.
 
Asilete ujinga huyu mnafiki.
Kuona tu imeandikwa na Lipumba sijasoma chochote.Najua hana kheri yoyote.
Magufuli ana mengi ya kukumbukwa katika kipindi chake kifupi cha uongozi kuliko huyu mjinga mjinga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom