Kumbukizi; Safari ya matumaini ya Mzee Lowassa alipowania Uraisi miaka 5 iliyopita

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,340
2,000
Hakika mwenyezi Mungu kaiwekea fumbo zito kesho yetu!

ILIKUWA NI ARUSHA, MKUTANO ULIOTAMBULIKA KWA JINA LA "SAFARI YA MATUMAINI" KATIKA KUWANIA TIKETI YA URAIS NDANI YA CCM
Enzi hizo hoja ilipokuwa haijibiwi kwa rungu!

Ilikuwa tarehe 30/05/2015;
Mafuriko ya lowassa yalivyoitikisa ARUSHA.
Viongozi mbalimbali wakiwemo wachungaji walihudhulia kumuunga mkono.

Alikuwepo Marehemu mzee Kingunge ngombare, Mashekh, Maaskof na Mapadree bila kumsahau swahiba kindakindaki wa lowassa mzee wa kanisa la uzima na ufufuo JOSEPHAT GWAJIMA.

Uwanja ulijaa kwelikweli, Ilikuwa Ukinyanyua mguu tu mwenzako anakanyaga...watu walikuwa full shangwe vaibu Kama lote, walishiba vizuri, kila mmoja alitabasamu kimoyomoyo kwa mtonyo na mavumba ya kutosha,
Shangwe na ndelemo Ziligharamiwa; walioweza kushangilia zaidi waliongezewa zaidi mtonyo,

Wanaofanikiwa kuzimia kwa shangwe walipatiwa laki tano zaidi, Nakumbuka nilikuwa jilani na jamaa yeye alifanikiwa kuzimia mara tatu maana ake alibeba milioni moja na nusu... Ambulance ilikuwepo kuhesabu wanaozimia kwa Shangwe!

AMA KWELI KISICHOKUWA RIZIKI HAKILIKI HATA UFANYAJE!
FB_IMG_1590822794332.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom