Kumbukizi: Putin na wenzake wakiwa Bagamoyo Tanzania

Uchina ana bandari nchini Djibouti ambayo itamsaidia kulinda meli zake kwenye mfereji wa Suezi lakini ili kulinda njia yote ya bahari ya Hindi wataalamu wanasema itabidi atengeneze kambi nchini Tanzania , Sri Lanka na Maldives.
Mkuu hao Djibouti wanaangukia alikopita Sri Lanka kwa madeni maana kakopa hela zaidi ya mapato sasa hapo mchina ancheza huu mchezo kwa kila anapotia mguu
Na sisi tujiangalie sana kwa small prints maana tukipewa page 50 huwa tunaanguka saini tu
Naomba isiwe hivyo
 
Djibouti siyo rahisi kwasababu pale kuna kambi kubwa ya Marekani chini ya jangwa la Sahara inaitwa Camp Lamonier. Hivyo Uchina lazima acheze kwa hatua. Upande wa pili hapo hapo Djibouti kuna kambi kubwa ya Saudi Arabia ambayo anaitumia kurusha ndege zisizo na rubani kupambana na wanamgambo wa Kihouthi kule Yemeni. Ukiangalia vizuri ramani utagundua Yemeni na Djibouti ni jirani sana hivyo Marekani na Saudi Arabia hawawezi kumwachia Uchina ashikilie serikali ya Djibouti kirahisi kama alivyofanya Sri-Lanka.

Marekani hawezi kuondoka pale kwasababu panampa nguvu ya kimkakati kuwepo bandari ya Hindi kupambana na nguvu ya Uchina. Marekani hapa Afrika hana kambi kubwa ya majini (Naval Force) ya kupambana na ushawishi wa Uchina kwenye bandari ya Hindi zaidi ya Camp Lemonier nchini Djibouti.

Upande mwingine Camp Lemonier inampa Marekani urahisi wa kupambana na ushawishi wa Iran kwenye nchi za kiislamu za Afrika kama Sudan na Somalia.

Uwepo wa mataifa makubwa mawili hasimu ndani ya nchi moja kunasaidia sana kuhakikisha mzani wa nguvu "Balance of Power" hautingishwi. Nadhani Uchina kama atacheza vibaya itakula kwake.

Tanzania tunatakiwa tuweke uwazi kwenye hii mikataba badala ya kuwaachia watu wachache tu. Pia upande mwingine tusiliachie taifa moja miradi yote mikubwa nchini. Kama Uchiba kapata gesi ya Mtwara, ile gesi ya Helium kule Rukwa tusimpe kabisa. Pia hata kwenye mikopo hatutakiwi tukope sana kwake. Twende na nchi za Magharibi.
 
Djibouti siyo rahisi kwasababu pale kuna kambi kubwa ya Marekani chini ya jangwa la Sahara inaitwa Camp Lamonier. Hivyo Uchina lazima acheze kwa hatua. Upande wa pili hapo hapo Djibouti kuna kambi kubwa ya Saudi Arabia ambayo anaitumia kurusha ndege zisizo na rubani kupambana na wanamgambo wa Kihouthi kule Yemeni. Ukiangalia vizuri ramani utagundua Yemeni na Djibouti ni jirani sana hivyo Marekani na Saudi Arabia hawawezi kumwachia Uchina ashikilie serikali ya Djibouti kirahisi kama alivyofanya Sri-Lanka.

Marekani hawezi kuondoka pale kwasababu panampa nguvu ya kimkakati kuwepo bandari ya Hindi kupambana na nguvu ya Uchina. Marekani hapa Afrika hana kambi kubwa ya majini (Naval Force) ya kupambana na ushawishi wa Uchina kwenye bandari ya Hindi zaidi ya Camp Lemonier nchini Djibouti.

Upande mwingine Camp Lemonier inampa Marekani urahisi wa kupambana na ushawishi wa Iran kwenye nchi za kiislamu za Afrika kama Sudan na Somalia.

Uwepo wa mataifa makubwa mawili hasimu ndani ya nchi moja kunasaidia sana kuhakikisha mzani wa nguvu "Balance of Power" hautingishwi. Nadhani Uchina kama atacheza vibaya itakula kwake.
Hapo umenena,
Lakini ameweka mguu pia hapo ingawa USA yupo hapo na pia Saudia na UAE pia,
yaani Djibouti anakula kuku kwa mrija hapo ingawa hawana kitu zaidi ya hiyo ardhi.
Mkuu nilienda hapo lakini kuna humidity sijawahi kuiona sehemu yoyote katika nchi zote nilizotembelea.
Kweli mmarekani hawezi kuacha hapo kwani inampa fursa za kuzilinda gulf states
Ila sasa kama Djibouti kakopa $8b kwa infrastructure atazilipa leo kweli au mchina atambana akatie kipande cha ardhi maana port ni kazi kuiachia labda wakusanye mapato tu
Kwa kweli mchina eti hana masharti, hii lugha ngumu kwangu mkuu utanisaidia
 
Nusu au karibia Afrika yote ilitekwa na Urusi mbona ilikuwa karibia kila nchi ya kijamaa na inafuata misingi za Urusi ukiiondoa south Africa.sasa huko kabla hawakuwa wabaguzi?

Sema baada ya kuanguka kwa ujamaa na viongozi wa nchi za Africa kukimbilia ubepari na sera za USA na EU ndio Urusi ilipopoteza ushawishi Afrika

Hata hivyo nchi za Afrika ni makoloni ya US na EU hivyo hawawezi kukaa karibu na Urusi tena nchi inayopigwa vita na mabwana zetu ndio maana huoni movements kwenye balozi zao..hivi mko radhi mkose misaada za mabwana zetu USA na EU kwa kufanya allignment na Urusi?

Urusi miaka yote imekuwa rafiki ya wanaharakati saizi wapo Syria kumsaidia Assad na pia ni rafiki wa Iran na china pamoja na North korea,Cuba,Uturuki

Zamani akina Sankara,Abdurahmani Babu,late nyerere,Nkurumah,Gamal Abdenasser na viongozi wa MPLA,Frelimo na wanaharakati wote wa Afrika walikuwa marafiki wa Russia.So si ajabu nao wametukaushia siku hizi huenda sababu hatuna uharakati
Ni kweli kabisa. Africa kipindi cha vita baridi nchi nyingi zilikuwa zimetekwa na mrusi. Mpaka shirika lao la ndege lilikuwa linafanya safari za DAR
 
View attachment 957917
Pichani wa Tatu Kutoka Kushoto ni Rais wa Russia-Urusi Sasa Hivi Vladimir Putin,Aliyekuwa Rais wa Msumbiji Samora Machael na Rais wa Sasa wa Zimbabwe Emmerson Mnangangwa Wakiwa Bagamoyo Nchini Tanzania

Vladimir Vladimirovich Putin alizaliwa Saint Petersburg wakati huo ikijulikana kama Leningrad, October 7, 1952. Ni rais wa Urusi kwa sasa tangia May 7, 2012. Alikuwa waziri mkuu kuanzia 1999 mpaka 2000, raisi kuanzia 2000 mpaka 2008, na tena kushika nafasi ya uwaziri mkuu kutoka 2008 mpaka 2012. Katika kipindi chake cha pili cha uwaziri mkuu pia alikuwa mwenyekiti wa chama cha Umoja wa Urusi.

Baada ya anguko la Ujamaa, Ujerumani Mashariki, Vladimir alirudishwa Saint Petersburg ambako June 1991 alianza kazi katika Idara ya Mambo ya nje chuo kikuu cha Saint Ptersburg. Kazi yake kubwa hapa ilikuwa kuchunguza na kuchuja vijana wa kujiunga na KGB.
Safi sana!
 
Kiuhalisia: Winning the heart of the Government is important than winning the hearts of common people
Ni kweli! Japo serikali huweza kubadilika na kubadilika huko huenda kukaambatana na mabadiliko ya kisera za nchi kulingana na utawala uliopo madarakani. Mfano utawala wa Obama na mradi wa nyuklia wa Iran na utawala wa sasa wa Trump.
 
Mkuu Malcom Lumumba!!

Sina cha kuongeza kwenye post yako #70 ingawaje umetonesha donda langu!!! Niseme jambo moja tu...

December last year nilikutana na American Researcher mmoja ambae alikuwa anafanya utafiti kuhusu China na project yake ya One Belt One Road Initiative. Moja ya case studies zake ni Bagamoyo Mega Port Project na kwahiyo alikuwa anatafuta mtu anayeifahamu Tanzania na ABCs kuhusu Bagamoyo Port Project!

Kwa bahati mzuri, sikuwa tu nafahamu ABCs za Bagamoyo Port Project bali nilikuwa nafahamu hadi ABCDE!

Kosa alilofanya ni kuniuliza nauona vipi mradi wa Bagamoyo Mega Port... nikafunguka kama nimemeza betri!!

Ilinichukua less than 1 minute kugundua kumbe jamaa tayari alishakuwa na matokeo ya utafiti wake kichwani hata kabla ya kufanya utafiti wenyewe!!! Ikawa ananipa arguments zake ambazo karibu zote zilikuwa zinalenga ku-discredit project lakini hakuna hoja ambayo sikumjibu!!!

In short, jamaa ni critic wa harakati za China in Africa... can you blame him?!

Hapa ndipo nikaikumbuka JF na wapinzani wa Bagamoyo Mega Port Project!!!

Magu na yeye alipoingia tu madarakani akalishwa sumu kibao kuhusu Bagamoyo Port Project na hakuna sumu ya kipumbavu kuliko zote kama inayodai eti Mkwere alikuwa anataka kujenga Bagamoyo Port kwa sababu ni kwao... hii hoja ilitolewa hata na yule Mzungu hadi nilipomwambia I wish we'd similar port project in Dodoma or Arusha but geography doesn't favor any of the said cities and you can't blame KIkwete for geography to be in favor of Bagamoyo!

Narudia, umetonesha donda langu na kwahiyo acha nikusanye kila kilicho changu hapa JF na niendelee na ndoto zangu za kuisaka Hollywood!
 
Mkuu Malcom Lumumba!!
Magu na yeye alipoingia tu madarakani akalishwa sumu kibao kuhusu Bagamoyo Port Project na hakuna sumu ya kipumbavu kuliko zote kama inayodai eti Mkwere alikuwa anataka kujenga Bagamoyo Port kwa sababu ni kwao... hii hoja ilitolewa hata na yule Mzungu hadi nilipomwambia I wish we'd similar port project in Dodoma or Arusha but geography doesn't favor any of the said cities and you can't blame KIkwete for geography to be in favor of Bagamoyo!
Mkuu Chige, katika vitu ambavyo Magu alipuyanga basi ni hili suala zima la Bandari ya Bagamoyo.
Sijui hata tufanyaje aisee maana watawala wa Tanzania ni watu wa ajabu sana.
 
View attachment 957917
Pichani wa Tatu Kutoka Kushoto ni Rais wa Russia-Urusi Sasa Hivi Vladimir Putin,Aliyekuwa Rais wa Msumbiji Samora Machael na Rais wa Sasa wa Zimbabwe Emmerson Mnangangwa Wakiwa Bagamoyo Nchini Tanzania

Vladimir Vladimirovich Putin alizaliwa Saint Petersburg wakati huo ikijulikana kama Leningrad, October 7, 1952. Ni rais wa Urusi kwa sasa tangia May 7, 2012. Alikuwa waziri mkuu kuanzia 1999 mpaka 2000, raisi kuanzia 2000 mpaka 2008, na tena kushika nafasi ya uwaziri mkuu kutoka 2008 mpaka 2012. Katika kipindi chake cha pili cha uwaziri mkuu pia alikuwa mwenyekiti wa chama cha Umoja wa Urusi.

Baada ya anguko la Ujamaa, Ujerumani Mashariki, Vladimir alirudishwa Saint Petersburg ambako June 1991 alianza kazi katika Idara ya Mambo ya nje chuo kikuu cha Saint Ptersburg. Kazi yake kubwa hapa ilikuwa kuchunguza na kuchuja vijana wa kujiunga na KGB.

Hii picha imeleta utata sana dhidi ya wafuasi wa TRUMP, Nimepitiapitia vicomment yani wamejikita kwenye ubaguzi tu 😀😀 mara oh warusi ni wabaguzi,ila wazungu si wabaguzi...kuna watu humu wa ajabu sana..
 
Ubaguzi ni asili ya mwanadamu na wanyama,wote wasiofanana ubaguana hata sie twabaguana
Nakubaliana na wewe 100 na zaidi. Usipoenda mbali unakuta kwenye familia wanasema huyu mtoto mweusi kama mkaa, hili kabila mimi siwezi hata kuolewa nao, hii nchi sijui wakoje. Ubaguzi unaanzia kwenye familia hasa sisi waafrika ndo wabaguzi wakubwa.
Warusi ni wale ambao wanadhani wana ile damu ya wateule kama wale wahindi wa Brahma halafu wale weusi wanaitwa untouchable. Can you imagine?
 
Mkuu hao Djibouti wanaangukia alikopita Sri Lanka kwa madeni maana kakopa hela zaidi ya mapato sasa hapo mchina ancheza huu mchezo kwa kila anapotia mguu
Na sisi tujiangalie sana kwa small prints maana tukipewa page 50 huwa tunaanguka saini tu
Naomba isiwe hivyo
Mkuu BS,

Malcom Lumumba ameelezea vizuri sana kwenye post yake #70 kiasi kwamba sie wengine hatuna cha kuongeza labda kama tunataka kuharibu!

I can understand your concern, lakini kama alivyosema ML, suala lililoikuta Bandari ya Hambantota huko Sri Lanka lisingeweza kuikuta Bandari ya Bagamoyo kwa sababu financing plan ya bandari hizi mbili ni tofauti! Hofu yako wewe ipeleke kwenye SGR... ngoja niongee jambo moja hapa: This's not about China na ukatili wao but it's about commercial loans popote pale utakapoenda duniani!

It's not about China kwa sababu, so long as unachukua commercial loan popote pale duniani LAZIMA pawe na guarantee ya namna gani utaweza kulipa mkopo wako in case of default! Tofauti kati ya mkopeshaji mmoja na mwingine ni aina ya guarantee anayoikubali in case of default! Inavyoelekea, guarantee pendwa ya Uchina ni project husika kwamba, ukishindwa kulipa wanahodhi mradi hadi pesa yao irudi... nothing personal, nothing monster like behavior but it's business! That's how the banking lending business operate popote pale duniani!!!!

So, the question is: Wakati Wachina wanaelekea kutumia project husika kama collateral, hizi commercial loans za mabilioni ambazo JPM anachukua, Wakopeshaji wetu wanakubali collateral ipi in case of default?!

Suali hilo hapo juu linapendeza kuwa na mada inayojitegemea!!!!

Back to the business! Kwanini nasema hilo la Hambantota Port lisingeikuta Bagamoyo Mega Port?!

Kama alivyosema Malcom hapo juu, Bagamoyo Mega Port Project ilikuwa under the so called BOT... Build Operate Transfer! Kwamba, Mchina angejenga bandari na kuiendesha over specified time! Hii ndiyo staili inayotumika sehemu nyingi duniani kwa expensive infrastructure projects!

Sasa katika mazingira kama hayo, yale ya Hambantota Port yasingeweza kutokea! Jambo muhimu kwetu ilikuwa ni kuhakikisha mradi hauwi overpriced!
 
Mkuu Chige, katika vitu ambavyo Magu alipuyanga basi ni hili suala zima la Bandari ya Bagamoyo.
Sijui hata tufanyaje aisee maana watawala wa Tanzania ni watu wa ajabu sana.
Biggest mistake ever!! Pamoja na kwamba natofautiana na Magu lakini namkubali sana katika ufuatiliaji wake! Huyu jamaa endapo angewekeza nguvu kwenye mradi wa bandar ya Bagamoyo, hadi kwisha kwake Tanzania ingeweza kupiga hatua hata kama madini yote unayatupa baharini!!
 
Bwana Tatum mbona unachekesha? Hiyo picha ilipigwa mwaka 1978. By then tayari samora ashakua rais, putin mwenyewe alikua na umri wa miaka 26. Huyo kamanda hapo unaejaribu kutu convince kuwa ndio yeye haonekani kufanana na kijana mdogo wa miaka26, pili putin hakuwahi kuajiriwa kwenye Red Army Bali alikua agent wa KGB.
Factamundo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom