Kumbukizi: Putin na wenzake wakiwa Bagamoyo Tanzania

Mkuu unapojibu usiwe unachagua sehemu ya kujibu
You seems unajibu zinazokupendeza tu nilikupa mfano wa central africa republic as a case study with the project of airport
Yes leaders come, leaders go but International treaties and bilateral business agreements between states do go away with leaders: And this is where the problem begins. Au nakosea hapa kiongozi unieleweshe ???

Ngoja nikuelezee kitu kirahisi kidogo. Kwenye sheria za kimataifa kuna kitu huitwa "Pacta Sunt Servanda" neno la kilatini kumaanisha kwamba nchi ikishaingia kwenye mkataba inalazimika kubaki kwenye huo mkataba mpaka pale muda wake utakuwa umeisha au malengo ya mkataba yatapokuwa yameisha.

Hujajiuliza kwamba kuna mikataba mingapi ya ilisainiwa hata kabla ya Uhuru lakini bado inatutesa sana ?
Hebu tupitiea kwa haraka kidogo hii mifano hai ya kihistoria:

1. Mkataba wa matumizi ya maji ya mto nile wa mwaka 1929
Mkataba ulisainiwa na viongozi kama Llyod na Muhammed Pasha lakini japo wamekufa leo wewe na mimi tunateseka. Kutumia maji ya ziwa Victoria mpaka tupigane mikwara na serikali ya wamisri.

2. Mkataba wa Heligoland wa mwaka 1890
Mkataba ulisainiwa na Leo Caprivi, Edward Baldwin na Henry Percy lakini umevuruga Tanganyika, Malawi na Zanzibari. Dar es salaam ilikuwa ni sehemu ya Zanzibari lakini ikaporwa na wazungu ambao walichora mipaka mipya. Leo tuna mgogoro usio na kichwa wala miguu na ndugu zetu Malawi, kisa tu wazungu waliokufa karne moja iliyopita.

Hapa utasemaje leaders come and go : Hizi nadharia unazitoa wapi wewe ndugu yangu ??
Mbona unasahau kuhusu ile mikataba ya Chenge na Mkapa ambayo itaviumiza vizazi vitatu vijavyo vya watanzania na kama nchi kujitoa hatuwezi kabisa..
 
Mrusi hana tofauti na Mhindi au mPakistani au far east countries people. They are racist to the maximum. Mrusi anaongoza na wao wanafuata au wapo level moja.
Kwa sasa naweza kupinga hoja ya Urusi kuwa taifa la wabaguzi, huko zamani huenda ilikuwa kweli ila sasa hivi Russians mingle a lot.
 
Kati ya watu waliovuna pembe za Ndovu hapa nchini ukiacha waarabu enzi za utumwa wa pili ni Wachina kwenye ujenzi wa Tazara.
Wamechukua sana mekyuli milimanu na madini kujifanya kutoboa milima na Mali za wajerumani wamezichukua sana,wamejilipa zaidi
 
Mi huwa najiuliza!

Hivi ilikuwaje mpaka russia ikawa haiivi na nchi za wazungu wenzake?

Maana karibu wazungu wote huwa wameshikamana si mchezo ila mrussi dzain km huwa anawacheki kwa dharau na kufanya yake
Mkuu mbona walio fika urusi wana sema choka mbaya tofauti na wenzie
 
That's why hawa jamaa watatoa dawa ya ukimwi hata kama ikipatikana labda Mungu awaoneshe dawa ya mti...its among their wepon in southern sahara countries
Kitu kimoja ambacho watanzania na waafrika wengi hatukielewi ni hiki:
Uchina anaiihitaji sana Afrika kuliko ambavyo Afrika inauhitaji Uchina. Sababu kuu ni hizi zifuatazo:

MOSI, Uchina inatoka kwenye uchumi wa kuzalisha kwenda kwenye uchumi wa kutumia kwasababu ya kuzaliwa kwa kundi kubwa la watu wenye kiwango cha kati cha Uchumi (The Middle Class). Leo hii kwenye soko la ajira la dunia, soko la bei ndogo na lenye wataalamu ni lile la Uchina. Ukiwachukua mainjinia wa Uchina na Ujerumani wa kiwango cha shahada, yule wa uchina atalipwa mshara mdogo kuliko yule wa Ujerumani kutokana na hali za maisha za nchi zao. Sasa kadiri wachina wanavyokuwa matajiri watataka mishahara mikubwa, hivyo kupelekea viwanda kutafuta soko la chini la ajira (Cheap Labour) sehemu nyingine duniani.

Unadhani siku Uchina akianza kuhamisha viwanda atavipeleka Ulaya ?? Jibu ni Hapana. Viwanda vyake atavileta Afrika kwasababu za kiuchumi na kibiashara. Takwimu za kisayansi zinasema kwamba japo Uchina wana soko la chini la ajira (Cheap Labour), barani Afrika kuna soko la bei ndogo zaidi kuliko Uchina. Mtaalamu wa kiwandani kutoka Uchina ana mshahara mkubwa mara kumi kuliko mtaalamu wa viwanda kutoka kenya na Ethiopia wa kiwango kilekile cha Utaalamu.

Henry Kissinger na Richard Nixon walikimbilia Uchina mwaka 1972 na kumbembeleza Waziri Mkuu wa Uchina wa wakati huo bwana Zhou Enlai akubali kufungua milango yake ya kibiashara ili viwanda vya Marekani viingie kule Uchina kwasababu kipindi hichi makampuni yalikuwa yanaogopa gharama za kuwalipa wafanyakazi wengi wa nchini Marekani wanaotaka mishahara mikubwa. Raisi Nixon aliwaambia wachina hivi "When you see an opportunity the best way is to cease it". Raisi Deng Xiaopinga hakuzubaa kabisa. Lakini leo sasa Uchina nako wanaanza kuwa na mishara mikubwa, sehemu iliyobaki kwenye mishahara ya chini kwa hawa wawekezaji ni huku kwetu Afrika.

PILI, Uchina ni taifa lenye uhaba na njaa kali ya madini na rasilimali ambazo Afrika sisi tunazo kwa wingi. Peter Navarro, ambaye ni mshauri mkuu wa Raisi Donald Trump kwenye mambo ya viwanda na hasahasa isitoshe kwamba yeye ni moja wa waanzilishi wa hii vita ya kibiashara baina ya Uchina na Marekani anasema haya yafuatayo: Uchina anatumia nusu nzima ya thaluji (Cement) ya dunia, karibia nusu ya chuma(steel) cha dunia , moja ya tatu ya madini ya kopa (copper) ya dunia na theluthi ya madini ya aluminium (Aluminium) ili kulisha viwanda vyake na kuendesha uchumi wake.

Haya madini yote yanapatikana vizuri huku Afrika, na kama siku Afrika wakiamua kumfanya Uchina apige magoti kama ambavyo nchi za Uarabuni zinamfanya Marekani na mataifa ya Ulaya wapige magoti basi tunaweza kufika mbali. Sioni kama kuna kitu cha kutuzuia sisi kubadilisha mwelekeo wa dunia hii.

Uchina na India hawana ulinzi wa nishati (Energy Security) kwasababu kama Uchina anategemea sana makaa ya mawa kuendesha viwanda vyake. Makaa ya mawe siyo chanzo kizuri sana cha nishati hivyo ni lazima aagize mafuta na gesi kutoka nchi za Uarabuni na Urusi. Hapa kwetu Tanzania wanataka kuja kuchukua gesi ya Mtwara, ambako kama tukiwa makini tunaweza tukalamba gharasha kubwa sana kutokana na hizi njaa za Uchina. Leo hii kama Marekani akizuia mafuta yasitoke pale Mashariki ya kati basi Uchina lazima akae chini alie. Mwaka 2017 Uchina ndiyo iliongoza kwa kuagiza mafuta kutoka nje: Hebu soma hapa uone mwenyewe: Crude Oil Imports by Country

TATU, kuna kitu kinaitwa The Malacca Strait Dilemna ambacho Raisi wa Uchina Huo Juntao alikisema mwaka 2003. Kwamba Uchina inategemea sana Bahari ya Pasifiki na mfereji wa Malacca kupitisha mafuta yake na bidhaa zake zinazotoka Ulaya, Mashariki ya kati na Afrika. Ubaya zaidi ni kwamba mfereji wa Malacca upo sehemu ambayo ina mgogoro mkubwa wa mataifa makubwa. Marekani ameshajua kwamba kama wakiziba huo mfereji basi uchina lazima ataumia tu. Kuna Jemedari moja wa Marekani alisema hivi "The Strait of Malacca is where we will get the Chinese".

Sasa Uchina kugundua hili akaanzisha The Belt Road Initiative (One Belt One Road Initiative) kwa kujenge reli na bandari zitakazomsaidia kukwepa hii kadhia. Akaja Tanzania kujenga Bandari ya Bagamoyo "The Bagamoyo Mega Project" ambayo ndiyo itamuunganisha na nchi karibia zote za Afrika ya kati, Afrika Kusini na Afrika Mashariki. Ukisoma The Bagamoyo Master Plan, utaona kwamba lile eneo litakuwa ni la kiuchumi au Special Economic Zone (SEZ), ambapo sheria zake zitakuwa ni za tofauti kabisa na sheria za sehemu nyingine za nchi ili kuwezesha uwekezaji ufanyike vizuri.

Reli itatoka pale bandari ya Bagamoyo na kuungwanishwa na reli ya reli nyingine huko Dar es salaam, pia itapita Malawi, Congo DRC, Burundi hadi Kigali. Kulikuwa na wazo kwamba watumie reli ya TAZARA
kuunganisha nchi za ukanda huu. Lile eneo litaunganisha Tanzania na sehemu kubwa ya Afrika na kuiweka Tanzania sehemu nzuri kiuchumi kwasabababu kwa mwaka bandari hiyo inaweza kuwa inashusha makontena 100,000. Ndiyo maana Tanzania ilivyotaka kujitoa TAZARA serikali ya Uchina ilimsihi Raisi Kikwete asifanye hivyo. Hebu soma hapa:China in rail upgrade talks with Tazara owners

Soma tena hapa kuhusu utanuzi wa reli kutoka Bagamoyo: Tanzania-Zambia Railway to be extended to four countries

Iko hivi kuhusu Bandari ya Bagamoyo na Uchina. Makubaliano ni kwamba Uchina angetumia bandari hiyo kwa miaka 30 na kutuachia. Huku upande wa pili amesaini Mkataba wa namna hiyo hivyo na Serikali ya Pakistani kwamba atatanua Bandari yake iitwayo Gwadar ambayo kwenye mkataba wao, Uchina itaitumia kwa miaka 40 na kuwaachia Pakistan. Hebu soma hapa: The Port of Bagamoyo: A Test for China’s New Maritime Silk Road in Africa

Njia ya Uchina ya usafirishaji wa majini itabadilika kutoka kwenda Mfereji wa Malacca ambapo bidhaa zake zitakazo toka Afrika ya Mashariki na kati hasa kwenye nchi zisizo na bahari zitapitia bandari ya Bagamoyo kwenda Bahari ya hindi hadi bandari ya Gwadar nchini Pakistani ambako bidhaa zitapakuliwa na kuwekwa kwenye reli na barabara ambazo zinafika Uchina. Hii itamsaidia Uchina kuepukana na kadhia ya kupita kule Mfereji wa Malacca na Bahari ya Kusini ya Uchina (South China Sea) ambako Marekani ana manowari za vita zaidi ya 300.

Bidhaa za mafuta zinazotoka Ghuba ya Uajemi( The Persian Gulf) zinapita nazo bandari ya Gwadar nchini Pakistani na kupakuliwa kwenye barabara na reli hadi kufika Uchina. Bidhaa zinatoka Ulaya nazo zitapika mfereji wa Suez hadi Bandari ya Gwadar bila kupita Mfereji wa Malacca.

Ili Uchina alinde biashara zake huku bahari ya Hindi atahitaji kutengeneza kambi ya kijeshi sehemu ambapo wataalamu wanasema nchi iliyokaa vizuri kimkakati ni Tanzania. Hebu ona nukuu hii: "Chinese facilities at Djibouti and Gwadar/Jiwani are unlikely to be the end of China’s expanding military presence in the Indian Ocean. China will also require facilities or staging points in or around east Africa, to help protect its massive energy trade from West Africa travelling around the Cape.........Many analysts think TANZANIA would be a good location. China has a close and longstanding relationship with Tanzania and recently took control of the newly built port of Bagamoyo, around 50 kilometres north of the Dar es Salaam" Kwa maelezo zaidi soma hapa: China's New Network of Indian Ocean Bases

china-silk-road.jpg

Ramani ya pili ya barabara mpya ya majini ambayo itaanzi Bagamoyo:
Malacca and Asia (2).jpg

NB: Rangi ya chungwa ndiyo Barabara mpya ya majini

Hapo kwenye mstari mwekundu kutoka Afrika, nchi zitakazouungwanishwa ni Ddjiboti, Kenya na Tanzania kupitia bandari ya Bagamoyo. Njia kuu itakuwa ni Bahari ya Hindi kutoka Bagamoyo hadi Pakistani ili kukwepa michezo ya Marekani.

Pakistani inapendekezwa sana kwasababu Waziri Mkuu wa India Narendra Modi mwaka huu alikataa kabisa kuruhusu Barabara na reli za Uchina zipite nchini kwake.

Hivyo waafrika tuache uoga na tuangalie dunia inavyobadilika. Hili la bandari ya Bagamoyo na gesi ya Mtwara tukishindwa kutumia vizuri kujenga ushawishi wetu kisiasa na kiuchumi hapa barani Afrika na Asia basi tusije tukamlaumu Mungu siku ya Mwisho.
 
Mkuu unapojibu usiwe unachagua sehemu ya kujibu
You seems unajibu zinazokupendeza tu nilikupa mfano wa central africa republic as a case study with the project of airport
Kuvunja mkataba wa kibiashara haimaanishi kuvunjika kwa mahusiano.
Hao Jamhuri ya Afrika ya Kati imevunja mikataba mingine na Uchina ndugu yangu ??
 
View attachment 958195

Hapo kwenye mstari mwekundu kutoka Afrika, nchi zitakazouungwanishwa ni Ddjiboti, Kenya na Tanzania kupitia bandari ya Bagamoyo. Njia kuu itakuwa ni Bahari ya Hindi kutoka Bagamoyo hadi Pakistani ili kukwepa michezo ya Marekani.

Pakistani inapendekezwa sana kwasababu Waziri Mkuu wa India Narendra Modi mwaka huu alikataa kabisa kuruhusu Barabara na reli za Uchina zipite nchini kwake.

Hivyo waafrika tuache uoga na tuangalie dunia inavyobadilika. Hili la bandari ya Bagamoyo na gesi ya Mtwara tukishindwa kutumia vizuri kujenga ushawishi wetu kisiasa na kiuchumi hapa barani Afrika na Asia basi tusije tukamlaumu Mungu siku ya Mwisho.

CC: chige , Wick , Red Giant , TUJITEGEMEE, Eli79 , muyovozi
Mkuu asante kwa ufafanuzi nimeelewa mengi humu
Ila kilichonishangaza ni uoga wa mwafrika na kutokujikubali kuwa sisi ni matajiri wakubwa tusioutumia utajiri wetu.

Waarabu kabla ya mafuta walikuwa wana dhiki kubwa sana kwa ajili ya jangwa na walikuwa hawana chochote si kilimo wala wanyama zaidi ya ngamia na mbuzi tu,
Walikuwa wanakula kenge na panya wa dessert tu
Lakini walipopatiwa uchimbaji walitaka nao waishi kama USA na Europe hapo nina maana wawekewe kila kitu kama wao yaani barabara, mahospital, na kila kitu ambavyo nchi yenye uwezo inaweza kuweka.

Sisi bado tunawaogopa na kuweka mikono nyuma pindi tunapokutana nao
Mpaka tuwape masharti yetu na kuwaambia unataka hiki na sisi tunataka hiki in return

Kuna sehemu pia umeandika mfano wa mishahara ya engeneer wa Kichina na Kijerumani duu nimekumbuka nilifanya kazi sehemu kulikuwa na sergeant wa USA na Captain wa urusi believe me sergeant alikuwa na mshahara mkubwa na heshima zaidi

Thanks anyway kwa uchambuzi
 
Kitu ambacho sina ushahidi au sikuwahi kusikia ni kuwa Warusi na Wacuba walikuwa/ au mpaka sasa wanainyonya/ kuiibia Afrika.
Siwezi kujua hata walikuwa wanafaidika nini na sisi. Ila watu wetu wengi wamepata elimu kutoka Urusi na Cuba. Wanajeshi (pamoja na silaha), wahandisi, tabibu n.k.
Si sawa na hawa tunaowaona wanatukumbatia na kuingia mpaka vijijini kwetu (wamarekani/wachina/waingereza) ambao wanatuibia na tunacheka nao.
 
Kitu ambacho sina ushahidi au sikuwahi kusikia ni kuwa Warusi na Wacuba walikuwa/ au mpaka sasa wanainyonya/ kuiibia Afrika.
Siwezi kujua hata walikuwa wanafaidika nini na sisi. Ila watu wetu wengi wamepata elimu kutoka Urusi na Cuba. Wanajeshi (pamoja na silaha), wahandisi, tabibu n.k.
Si sawa na hawa tunaowaona wanatukumbatia na kuingiza mpaka vijijini kwetu (wamarekani/wachina/waingereza) ambao wanatuibia na tunacheka nao.
Mkuu wakati huo tulikuwa na viongozi wenye upana wa kufikiri.
Ndio maana tukapata wataalamu wengi waliosoma huko.
Ni suala la kuwaambia je na sisi mnatupa nini?
 
Kilichomfanya Uchina kuwa taifa kubwa leo hii ni kuachana na siasa za kinazi na kuanza kufikiria mbele.
Siasa za woga (Politics of fear) mpaka lini mkuu wangu ??? Katika masuala ya ambayo yamenifanya nisielewana sana na Raisi wangu Magufuli mojawapo ni hili la bandari ya Bagamoyo na gesi ya Mtwara.

Siku moja tulikuwa tunaongea na mkuu chige akaniambia kwamba kama Raisi angekazia vizuri hii mikataba ya gesi na bandari basi asingehangaika kabisa na suala zima la makinikia na hesabu inaonyesha kwamba angeweza hata kununua bombardier zaidi ya 50 kutokana pesa za hii miradi.

Marekani na ujehuri wake woteee, mwaka 1973-1974 kipindi cha mgogoro wa mafuta (The Oil Crisis) waarabu waligoma kumuuzia mafuta kwa kuwaunga mkono wayahudi kwenye vita ya Yom Kippur. Marekani ilisimama na watu walikuwa wanapanga foleni kununu mafuta. Tena kipindi hicho hicho haya mafuta ya waarabu yalipelekea sana kwenye maamuzi ya nchi za kiafrika kuvunja mahusiano na Israel.

Sasa Uchina ana njaa sana na rasilimali, na Tanzania ndiyo nchi iliyokaa vizuri kimkakati kuliko nchi zote za Afrika sasa sijui tunashindwa nini. Nchi kama hii wangepewa watu wa Irani au Korea Kaskazini, nakuhakikishia dunia nzima ingesimama. Leo hii Urusi, Marekani na Israel wanaogopa kumchokonoa kabisa Mturuki kwasababu wanajua kabisa kwamba hawawezi kufanya kitu mashariki ya kati bila yeye.

Tena akigoma Urusi anaweza asipite kabisa kwenda bahari ya Mediterannean kwasababu lazima apite kwenye The Bosphorous ili afike Mashariki ya kati. Huku Marekani anategemea anga la Uturuki kupambana nchini Syria, Iran, Iraq na Urusi. Kama Uturuki akiamua kufunga Incirlik Air Base basi Marekani na Israeli watapata tabu sana.

Sasa Tanzania Uchina, Pakistan na India wanatuhitaji mno ili kufika sehemu za ndani za Afrika. Tumezungukwa na nchi nane zenye utajiri mkubwa. Congo DRC, Malawi, Zimbabwe, Zambia, Rwanda, Burundi na Uganda watategemea sana bandari zetu kupata vitu kutoka bandari zetu. Sasa kama tutaunganishwa kwa reli nchi kama Uchina, India, Pakistani na nyinginezo za Asia zitajipanga pale magogoni kuleta madili ya kibiashara.

Lakini ndiyo vile, kwenye miti mingi hapana wajenzi: Ukisema sana wanakwambia wewe siyo mzalendo.
Tuendelee kuishi hivihivi tu, maana ndiyo maisha tuliyojichagulia.
Mkuu bandari inanyanyua uchumi wa nchi,
Kuna nchi zimetajirika kwa bandari tu
Laiti angeelewa thamani ya bandari kweli tungekuwa tunaongelea mengine.

Nikiangalia Singapore ambao walipata uhuru baada yetu nashangaa tu kwani wao kwanza kodi iko chini sana na ni free trade pia ukitaka kufungua biashara inachukua masaa matatu tu
Umemalizia kwa uchungu sana lakini ukweli umeuweka, nimekuelewa sana mkuu
 
Pale Singapore ndiko kuna mfereji wa Malacca "The Malacca Strait".
Asilimia 50% ya bidhaa za dunia (world Merchandise) zinapita kwenye ule mfereji: Inamanisha Singapore anakusanya kodi kutoka Afrika, Ulaya na Asia. Safari ya majini inaanzia Ulaya, inapita bahari ya mediteranea, Inapita Misri kwenye mfereji wa Suez Canal, Bahari ya Hindi, Pasifiki, Inafika Malacca na kuelekea Mashariki ya Mbali: Ramani yake hii hapa:
Malacca Route.jpg

Sasa kama na sisi tukiwa makini lazima tulambe karata dume ambayo itabadilisha uchumi wa nchi yote.
Malacca and Asia (2).jpg

NB: Rangi ya chungwa hiyo ndiyo inaonyesha barabara mpya ya majini ambayo Tanzania tunaweza kuitumia sana kiuchumi kuanzia Bagamoyo kuunganisha Afrika na Asia.
 
View attachment 958310

Sasa kama na sisi tukiwa makini lazima tulambe karata dume ambayo itabadilisha uchumi wa nchi yote.
View attachment 958301

NB: Rangi ya chungwa hiyo ndiyo inaonyesha barabara mpya ya majini ambayo Tanzania tunaweza kuitumia sana kiuchumi kuanzia Bagamoyo kuunganisha Afrika na Asia.
Kwa hakika tuna kila haki ya kuongelea hili tena nyie ndio wa kulibebea bango haswa,
Hiyo route ndio nimeiona kwa kweli mkuu, maana mimi naijua ya majirani zetu wa mbali kidogo, Somalia
Ambapo meli zote zinapita hapo Red sea na ndipo walipoanza uharamia baada ya kuibiwa sana samaki na wachina.

Yaani tungeshikamana kwa sheria kali na maendeleo Africa kwa kweli tungefika mbali sana
Thanks again mate
 
Uchina ana bandari nchini Djibouti ambayo itamsaidia kulinda meli zake kwenye mfereji wa Suezi lakini ili kulinda njia yote ya bahari ya Hindi wataalamu wanasema itabidi atengeneze kambi nchini Tanzania , Sri Lanka na Maldives.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom