Kumbukizi: Masomo ya Arts sekondari tuliyaita Masomo ya kike

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,318
Maisha kweli ni Safari ndefu toka unazaliwa mpaka kifo Kama Mungu akikujalia kuishi miaka aliyokupangia kuishi na ukafa kifo halali yaani kifo cha uzee kwa umri.

Kwa kupitia maisha ya shule toka darasa la Kwanza mpaka chuo hapo katikati Kuna mengi sana mwanafunzi anapitia kitaaluma na kijamii bila kusahau kiuchumi.

Wapo wanafunzi walioacha Masomo kwasababu ya mimba,kufukuzwa shule kwa utovu wa nidhamu na hata wapo waliofariki.Nakumbuka tukio ambalo sitasahamu ni tukiwa darasa la Kwanza halafu mwanafunzi mwenzetu was darasa la Kwanza alipokuwa anakuja shule treni ya Tazara ikamgonga na kufariki kwasababu baadhi ya wanafunzi eneo walilokuwa wanaishi Ni lazima wavuke mto kupitia daraja la treni ya Tazara wafuate reli Kama barabara yao ndo wafike shuleni.

Tukiwa sekondari ilikuwa ukichagua Masomo ya Arts na wewe Ni mwanaume unazomewa na wengine kuwa hayo masomo wanatakiwa kusoma watoto wa kike na sisi kujifanya tunasoma Masomo ya sayansi ndiyo ya kiume.

Lakini ukiangalia zaidi Masomo ya Arts ndiyo yamekuwa yanawatoa watu kimaisha maana wengi wako taasisi za kifedha,vyombo vya habari,balozi mbalimbali,sekta ya biashara nk.

Wanasayansi wengi wako idara ya afya,mifugo,uvuvi madini nk.

Ukweli ni kwamba hakuna Masomo ya kike wala ya kiume la msingi ni mtu kifikia ndoto zake na si kutunishiana misuli kuwa Nani anasoma Masomo magumu na kujiona mwamba.
 
Back
Top Bottom