Kumbi za starehe, majumba ya kamari n.k

Ambition plus

JF-Expert Member
Feb 23, 2018
4,198
2,000
Ciaaao?

Niende moja kwa moja kwenye mada harakaharaka. Nimeona waziri wa nchi akizungumzia nyumba za ibada.Yuko sahihi sana mana kuna wakati pia nawaza kama hawa ndugu zetu walokole. Mara nyingi wakishushiwa upako huanza kukemea, Kulia na kunena kwa lugha sambamba na kutoa mapepo. Wakati hayo yakiendelea sidhani kama swala la maelekezo ya wizara husika ya afya kama watakumbuka kuyafata.

Linalonitatiza hasa kwanini waziri wa nchi azungumzii swala La kumbi za starehe,ma bar na vilabu vya pombe, madanguro, kumbi za miziki na kamari, minada na magulio. Je hizi sehemu sio hatarishi hasa hasa kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa mapafu?

Kama wakiona yanayotendeka huko kwa kweli hali inatisha.

Walevi kama una povu ruksa.

Nawakilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Habun

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
73,028
2,000
Ila binadamu sisi ni wa ajabu, ushatambua huu ugonjwa ni hatari, umeshuhudia watu walivyokufa kama nzi bado unasubiri uambiwe na kiongozi eti usifanye A B C.... kweli
Kama huwezi kujijali mwenyewe unategemea nani akujali?
 

Ambition plus

JF-Expert Member
Feb 23, 2018
4,198
2,000
Ila binadamu sisi ni wa ajabu, ushatambua huu ugonjwa ni hatari, umeshuhudia watu walivyokufa kama nzi bado unasubiri uambiwe na kiongozi eti usifanye A B C.... kweli
Kama huwezi kujijali mwenyewe unategemea nani akujali?
Mkuu kila mtu na akili yake.Huku mitaani watu wanaendelea na mishe zao kama hakuna lolote vile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom