Kumbe Zitto Kabwe alishapokea ‘’mlungura’’ wa Barrick Gold, tutapona kama Taifa?

Kama amechukua nadhani haijalishi, kinachojalisha ni ripoti ya kamati iwe kweli, Zitto Kabwe atawezaje kuwabeba hapo?

Wamesema watalipa kama walikuwa wanaiba so badala ya kuanza kumlaumu Zitto tusubiri

Sent from my VF695 using JamiiForums mobile app
Nadhani hujasoma andiko lote!

Hoja zako ziko nje ya msingi wa mada.

Soma andiko lote kama unafahamu vizuri lugha ya kiingereza.
 
CCM kuanzia kuhangaika kumtafuta mchawi kwa sasa mnajichoresha tu. Tusubiri hizo trilioni 108 tukabidhiwe Noah zetu
 
Hakuna sababu ya kuwaunganisha wapinzani katika saga hili la mikataba mibovu ya madini,hicho kinachoitwa "kamati ya majadiliano"ni vizuri kikawahusisha ccm pekee kwa sababu ccm kupitia serikali yake,bunge lake na vyombo vyake ndiyo waliotufikisha hapa tulipo.

Wakati tunajaribu kuokoteza hoja dhaifu ili kuwahusisha wapinzani katika sakata la mchanga wa madini,tunapaswa kujiuliza swali gumu:mikataba hii ya kinyonyaji ya uchimbaji madini ilisainiwa chini ya serikali ya chama gani?Kwa nini viongozi wastaafu ambao kimsingi walishiriki kikamilifu katika mikataba hii ya kiharifu tunawalinda kwa ghalama yoyote ile ili wasihusishwe katika kadhia hii?

Tusijaribi kuuzunguka mbuyu,wakati viongozi wetu wanatuhadaa kwa kujifanya hawamjuwi Mchawi wetu,ukweli ni kwamba viongozi hao walikuwa sehemu ya wabeba tunguli katika ibada za kishirikina za kuliroga Taifa letu kiuchumi.Hao wanaotuhadaa leo na kutuziba vinywa tusiwahusishe wastaafu wa awamu ya 3&4 katika kadhia hii,walikuwa sehemu ya cabinet iliyojadili,kuridhia na hatimaye kupitisha mikataba hii iliyoruhusu wachimbaji kumiliki kila kitu kitakachopatikana katika mchakato wa uchimbaji,hao ndiyo waliowamilikisha wachimbaji hadi vumbi la makinikia na kuruhusu lisafirishwe kwenda nje.

Leo tunapomuona mtu aliyekuwa sehemu ya waliolihujumu Taifa kupitia mikataba hii akijigeuza malaika wa nuru aliyeshushwa kuja kuitoa Tanzania katika giza la mikataba ya kilaghai na kuileta katika nuru,wenye akili timamu ambao hatujaathiriwa na "vumbi la makinikia", tunaishia kuubeza na kuushangaa ujasiri huu wa kishetani anaovikwa mtu ambaye ameshajiapisha kutofukua makaburi ya watangulizi wake ambao kimsingi ndiyo waliobariki Wizi anaojaribu kupambana nao.

Sasa kama hataki kuwahusisha watangulizi wake katika ubadhirifu huu,atawezaje kukabiliana na mabeberu hawa ambao tuliwakabidhi madini yetu wenyewe?Hapa ndipo wenye akili tunapoiona " sanaa ya makinikia ni sanaa kama sanaa nyingine zilizowahi kuchezwa ndani ya Taifa hili,tofauti pekee ya sanaa hii ya makinikia na sanaa nyingine,ni kwamba inasimamiwa na muongozaji ambaye hana uwezo wowote wa kusimamia na kuongoza sanaa,matokeo yake badala ya kuifanya iwe na matokeo chanya yanayoweza kujibainisha hata katika mtiririko wa kuchezwa kwake,anarudi nyuma na kupiga marufuku kuhudishwa kwa washiriki nguli ambao walikuwa na nafasi kubwa katika ufanikishaji wa "muvi hii ya kiwango cha lami"

Upumbavu na ujinga wetu ndiyo mtaji wa watawala wetu,watu waliotufikisha hapa wanapotuhadaa na sisi tukageuka na kuwashangilia na kufikiria hata kuandaa maandamano ya kuwapongeza,wanabaki wanajiuliza kuwa sisi ni watu hai au wafu?Yawezekana sisi ni wafu,walio hai hawawezi kuchezewa akili kiasi hiki na wakabaki kupiga makofi na kushangilia.

Kuna mstari mwembamba sana wenye kipenyo cha 0.000001 micron unaoweza kuwatenganisha waheshimiwa wa awamu za 3&4 katika mikataba yote ya uchimbaji wa madini na gesi,kuzuia wasihusishwe kwa namna yoyote ile na sakata la mikataba hii,kunalifanya sakata lote kuwa ni la kizushi zaidi kuliko uzushi wenyewe!Ripoti zote mbili hazina mahali popote zilipomtaja Mh.Zitto Kabwe,iweje leo tuanze kuokoteza hoja za kumuhusisha Zitto wakati hajawahi hata kukanyaga corridor za chumba ambacho cabinet ya ccm ilikutana kujadili namna ya kuugawa utajiri wetu kwa wawekezaji?Kama wenyeviti wa cabinet hizo hatutaki kuwahusisha kwa kigezo kuwa hawakutajwa na ripoti zote mbili,iweje leo tumuhusishe muhanga wa mikataba mibovu iliyotiwa sahihi Hotelini Londoni lakini Zitto alipojaribu kuihoji serikali juu ya uadilifu wake kwenye mikataba hii iliyosainiwa nje ya nchi aliishia kufukuzwa bungeni?
 
Black mailed ni kitu kibaya naona jamaa anafakuchunguzwa pia.
Mtu haiwezi kum critised Rais Magufuli wakati na yeye ni mtuhumiwa.
Mkuu,

Una maana gani unaposema black mailed? Nani amekuwa black mailed?

Nifafanulie.
 
Mimi binafsi hata ile kauli ya Magufuli kuwa kuna msg walizidaka zinaomba data Barrick kwa Mnyika naamini ni Zitto huyo. Kama raisi Magufuli anataka kufanikiwa katika uongozi wake aachane kabisa na wabunge, wale ni njaa kali. Afanye mipango yake bila kutumia bunge
 
Hii nchi inawapumbavu wengi sana.
Hivi kuna mpinzani yeyote mwenye uwezo wa kufanya ufisadi tena wa kitaifa?

Yaani serekari na ccm kwa ujumla imuangalie mpinzani akiingia mikataba na kuhakikisha kwa njia moja au nyingine ufisadi unafanyika?

Jamani tulishajikwaa tufanye tu madiliko ili tusipotee tena.
 
hilo ndio jibu ambalo huwa linatolewa mtu anapotaka kujua ni lini zzk alinyamaza kupigania mali zetu.

ila pia angalizo suala la madini ni la kutaaruma. Tukiruhusu siasa tunaweza kujikuta tunafuraha za moto wa mabua. yawezekana kweli aliwahi kupewa mlungura maana sijawahi kusikia nje ya maeneo krb na migodi mgodi kufanya shughuli hizo za maendeleo . ajitokeze afafanue....

only truth and not politics will set this nation free
Mkuu;
Hiyo truth kuipata kwa mwanasiasa ni nadra sana!

Mazingira yanaonyesha ukweli pamoja na kwamba ni vigumu sana ukweli huu kumlazimisha aseme ukweli.
 
Wengi andiko hili naona kama hamkulielewa sana, labda ya malkia imekuwa sumu, lakini andiko lina kina chake cha kulitafakari.

1. Kuna mchangiaji kachangia hapo page two kaonesha vema kuwa haya waliyowahifanya barrick kama ambavyo ripoti inataka kudadisi pengine yakafanyika na leo na tayari mnaona Rais kama keshaingia mkenge, kwa maneno mengine katika vita usitangulize pesa mbele, utapewa utanyamaza so did ZZK

2. Ripoti hii inaamsha udadisi wa miaka ya 2011 na uzoefu wa sakata la madini, wengi mnaijibu kama vile ni part and parcel ya makinikia leo, this article can be used on current saga to reflect kile kilitokea enzi vuguvugu la madini lilipoongozwa na ZZK kitu kilipelekea akafukuzwa Bungeni.

Pia nimependa Research ya Huyu Adam inasema wabunge wengi ni Mazwazwa, hadi Barick walifikia kuona kama ZZK ndio Tishio wakati huo, na alipojengewa shule (hii ndio inayoonekana) akawa kama amezimwa na hata jamii ilitegemea Zito awe msumbufu wakati wa kuunda sheria lkn alikuwa kimyaaa ( udadisi wa rushwa unaibuka hapa katika tafti za mtafti husika).

Mwisho the big picture inayoamshwa ni hisia za kutafakari juu ya kile kilifanya zito kuwa kimya na Barrick kupeleka mradi Kigoma, inaweza kuwa ndio trick ileile waliofanya Barrick juzi, hasa ukizingatia kabisa weakness ya Rais wetu nikupenda Pesa, barrick wakatumia hiyo kumzima ay kum soften.

Nnaposema Rais wetu anapenda pesa yaweza isiwe (direct) anapenda kuongwa la! Rais huyu Anatamani kupata pesa either za maendeleo au kujiwekea stock serikalini, sasa hii Barrick wanaweza itumia vema na akashindwa kwenda kwenye kiini cha tatizo la nchi ila akahairisha tatizo kwasababu ametanguliza pesa na mihemuko, mbeleni madudu yakaendelea.

Note: Rais amedhihirisha mara kadhaa akiwa excited tu anakurupuka kufanya tamko, juzi ujio wa Barick ulimkuna akawaambia ni wanaume. Hii ilikiwa ni failure namba moja katika battle alioanzisha
 
Mkuu,

Una maana gani unaposema black mailed? Nani amekuwa black mailed?

Nifafanulie.
Unapotuhumu kampuni and then kampuni inakuziba mdomo kwa kukujengea shule what do you expect.
Kwenye zilizoendelea hiyo ni scandal kubwa Zitto angejiuzulu haraka.
Tutegemee mengi kutoka Barrick hawawezi kukubali aibu hii iwe yao watasema mengi.
 
MsemajiUkweli Unatakiwa Utambue kuwa kwa sera za nchi hii, adui wa taifa ni adui wa kila mtanzanania na vivyo hivyo kwa kinyume chake.

Zitto kabwe alipambana kadiri ya alivyoweza, lakini alishindwa kuwafanya lolote kwani walikuwa wanakingiwa kifua na serikali, na hapa ndipo usemi usemao "IF YOU CAN'T BEAT THEM, JOIN THEM" (Kama huwezi pambana nao, basi ungana nao). ZZK hakupenda kufanya hayo unayotaka kutuaminisha, bali mfumo mzima ulikuwa haupo upande wake na ulimlazimisha kufanya na kutenda kinyume na maono na misimamo yake.
 
Back
Top Bottom