Polycarp Mdemu
Senior Member
- Jun 2, 2019
- 165
- 209
+ Katika Vitabu maarufu vya historia vinavyotolewa na "UNESCO World Heritage" kuna Makala ambazo huwa zinahusu orodha ya miji mikongwe ambayo mpaka leo inakaliwa na watu (List of oldest continuously inhabited cities) hapa utakutana na majina ya miji mingi ya kale japo mingine haikaliwi na watu lakini ipo inayokaliwa bado, ndio hupewa heshima katika makala hizi......
Katika nchi za Ocenia kuna mji unaitwa Sydney, huu ndio unaongoza katika bara lake, Ukienda nchi ya Ulaya utakutana na mji unaitwa ARGOS nchini Ugiriki, huu ndio mji wa kalr zaidi ulaya, haujulikani ulianza miaka gani lakini Monuments zake huonyesha una umri zaidi ya miaka 7000, Moja ya Watu maarufu wa Enzi hizo walikuwa akina Acrisius, Ageladas kiufupi hata elimu ya "MYTHOLOGY" ilianzishwa na watu wa hapa.
Barani Asia kuna mji unaitwa RAJGIR kule India, huu unadhaniwa kuwa ulikaliwa na watu toka miaka 2000 K.K Mwanzilishi na Kiongozi wa kwanza alikuwa akiitwa Brihadratha ambaye alikuwa mtoto wa Mfalme Uparichara Vasu.
Ukienda bara la Amerika kuna mji unaitwa Flores kwa sasa lakini zamani uliitwa Nojpetén nchini Guatemala unakadiriwa kukaliwa na watu toka miaka 900 K.K
Ukija Barani Africa tunaweza Gawanya bara hili mara mbili kwakuwa upande wa Kaskazini ulikuwa mashuhuri zamani kuliko Kusini (Sub Saharan) hivyo kwa Upande wa Africa Kaskazini mji wa kale zaidi uliitwa LUXOR japo ulijulikana zaidi kwa jina la kigiriki THEBES mji huu unakaliwa na Watu toka miaka ya 3200 Kabla ya Kristu,
Ukija Kwenye nchi za Kusini mwa jangwa la sahara Mji wa kale huitwa Benin City unapatikana nchini Nigeria unafuata mji wa Ife upo Nigeria Pia, miji hii miwili yote hukaliwa na Watu toka miaka ya karne ya kwanza.
Mji wa Tatu ni Zanzibar, Ukikaliwa na watu toka Karne ya Kwanza, Uthibitisho wa Uwepo wa mji huu haukuwepo toka zamani sana, lakini kuna maandishi ya Kigiriki-Kirumi (Greco-Roman) yaliyoandikwa karne ya Kwanza yanayoitwa "Periplus Maris Erythraei" hii ilikuwa kama maandishi au jarida linaloelezea Fursa za biashara Kwa warumi na wagiriki walioishi Huko Misri na Ulaya kwa ujumla, Katika Jarida hilo kilitajwa kisiwa kimoja chenye fursa ya biashara kilichoitwa "Menuthias" ambacho bila shaka ndio "Unguja" ya sasa, Maandishi yale kwa kiingereza huitwa "Periplus of the Erythraean Sea" na ndiyo huonyesha Mji huu mkongwe Tanzania ukifuatiwa na Tanga.
Polycarp MdemuView attachment 1796245View attachment 1796242
View attachment 1796243View attachment 1796244View attachment 1796246