Kumbe Watanzania tuna uvumilivu mkubwa sana wa kisiasa; USA siyo, kosa la "upotofu wa kauli" linaondoa heshima ya Rais Trump

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
6,630
2,000
å Mimi mara nyingi humfananisha Rais Donald Trump wa Marekani na Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania kitabia na kwa staili yao ya uongozi.

å Kwa yanayotokea Marekani chanzo kikiwa ni tabia na mwenendo mbovu wa Rais Trump, laiti ingekuwa yanafanywa na kiongozi wa mojawapo wa nchi za dunia ya tatu kama Tanzania, hakika ingekuwa ni maafa makubwa.

å Hakuna ubishi kuwa Rais Donald Trump ana tabia na mwenendo wa viongozi wa nchi masikini za dunia ya tatu kama Tanzania na zingine. Wamerekani walifanya kosa kumpa madaraka makubwa ya Urais. Madhara yake ni hayo.

å Sisi Tanzania bila shaka, Magufuli ndiye Trump wetu. Chunguza kauli za Rais Magufuli za mara kwa mara ktk hotuba zake. Mara nyingi huwa zinabeba ujumbe wa kuhimiza ghasia toka kwa wafuasi wake dhidi ya wasio kuwa wafuasi wake.

å Lakini nini hutokea? Kwa kiwango kidogo sana huleta madhara. Hii ni tofauti na nchi kama Marekani ambako viongozi wanaaminika sana bila kujali wasemalo ni UKWELI au UONGO.

å Wafuasi wa Trump wanamwamini sana kwa kila litokalo ktk kinywa chake. Tukio la uvamizi wa Capitol Hill wiki jana ni matokeo ya kauli zake kwa wafuasi wake na wakafanya kweli sawsawa na maagizo ya kiongozi wao.

Sisi kumbe ni wavumilivu na waelewa sana.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,879
2,000
Ni kweli ulichokoandika, hao jamaa wanafana almost kila kitu, Trump ni mkurupukaji bahati nzuri yeye alizuiwa na misingi ya kuheshimu sheria na vyombo vya maamuzi waliyojiwekea wamarekani, sisi kwetu hilo halipo, wa kwetu anaharibu makusudi na hakuna wa kumzuia, yeye ndie kila kitu.

Mfano mbovu wa hilo, sasa hivi hapa kwetu kila mtu analazimishwa kuimba wimbo wa Chato hata kama hataki kuuimba, lakini inabidi kuimba tu kwasababu mwenye madaraka ana tabia kama za Trump na bahati mbaya hakuna chombo kingine cha kumbana asifanye anayofanya.

Hivyo Trump ameondolewa Marekani sio kwasababu ya maamuzi ya wapiga kura kwenye sanduku la kura pekee, lakini zaidi ni kwasababu taasisi walizoziweka zina misingi ya uhuru haziingiliani.

Kama hilo lingekuwepo hapa kwetu, hata huyu wa kwetu nina hakika muda huu ninaoandika hapa asingekuwa tena Rais wa nchi yetu, kinachombakisha madarakani ni misingi mibovu tuliyojiwekea kama taifa isiyoheshimu maamuzi ya wapiga kura, inayoasisiwa na Katiba mbovu tuliyonayo.
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,847
2,000
Ni kweli ulichokoandika, hao jamaa wanafana almost kila kitu, Trump ni mkurupukaji bahati nzuri yeye alizuiwa na misingi ya kuheshimu sheria na vyombo vya maamuzi waliyojiwekea wamarekani, sisi kwetu hilo halipo, wa kwetu anaharibu makusudi na hakuna wa kumzuia, yeye ndie kila kitu.

Mfano mbovu wa hilo sasa hivi hapa kwetu kila mtu analazimishwa kuimba wimbo wa Chato hata kama hataki kuimba, lakini inabidi kuimba tu kwasababu mwenye madaraka ana tabia kama za Trump na bahati mbaya hakuna chombo kingine cha kumbana asifanye anayofanya.

Hivyo Trump ameondolewa Marekani sio kwasababu ya maamuzi ya wapiga kura kwenye sanduku la kura, lakini zaidi ni kwasababu taasisi walizoziweka zina misingi ya uhuru haziingiliani.

Kama hilo lingekuwepo hapa kwetu, hata huyu wa kwetu nina hakika muda huu ninaoandika hapa asingekuwa tena Rais wa nchi yetu, kinachombakisha madarakani ni misingi mibovu tuliyojiwekea kama taifa isiyoheshimu maamuzi ya wapiga kura, inayoasisiwa na Katiba mbovu tuliyonayo.
Mkuu huyu wetu ameendelea kuwa madarakani kutokana na ujinga wetu watanzania including hao wanaompa kiburi
 
UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
4,393
2,000
Mkuu huyu wetu ameendelea kuwa madarakani kutokana na ujinga wetu watanzania including hao wanaompa kiburi
Bwashee, wewe kuwa mjinga ni sawa kwa kuwa umejiona uko hivyo, lakini usituingize humo na sisi wengine. Jisemee nafsi yako; generalaizesheni haikubaliki.
 
lebabu11

JF-Expert Member
Mar 27, 2010
2,061
2,000
Absolutely, chief kwa hanayo yafanya Tramp, na yanayoendelea Tanzaniagiza ni the same thing
But different ni kwamba US wana Strong institutions out of that
Wangepata tabu kama ss nchi za giza.
Tupambanie taasisi imara yenye kulinda katiba yetu
Uimara wa taasisi ni watu au raia imara.
Watu wa hovyo huzaa taasisi za hovyo na mwisho taifa la hivyo.
Kujenga taifa imara, tunatakiwa kuwa na watu imara kifikra na siyo magoigoi.
Kufurahia raia wasiohoji kwa kigezo cha uzalendo uchwara ni upumbavu uliopitiliza.
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
2,696
2,000
å Mimi mara nyingi humfananisha Rais Donald Trump wa Marekani na Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania kitabia na kwa staili yao ya uongozi.

å Kwa yanayotokea Marekani chanzo kikiwa ni tabia na mwenendo mbovu wa Rais Trump, laiti ingekuwa yanafanywa na kiongozi wa mojawapo wa nchi za dunia ya tatu kama Tanzania, hakika ingekuwa ni maafa makubwa.

å Hakuna ubishi kuwa Rais Donald Trump ana tabia na mwenendo wa viongozi wa nchi masikini za dunia ya tatu kama Tanzania na zingine. Wamerekani walifanya kosa kumpa madaraka makubwa ya Urais. Madhara yake ni hayo.

å Sisi Tanzania bila shaka, Magufuli ndiye Trump wetu. Chunguza kauli za Rais Magufuli za mara kwa mara ktk hotuba zake. Mara nyingi huwa zinabeba ujumbe wa kuhimiza ghasia toka kwa wafuasi wake dhidi ya wasio kuwa wafuasi wake.

å Lakini nini hutokea? Kwa kiwango kidogo sana huleta madhara. Hii ni tofauti na nchi kama Marekani ambako viongozi wanaaminika sana bila kujali wasemalo ni UKWELI au UONGO.

å Wafuasi wa Trump wanamwamini sana kwa kila litokalo ktk kinywa chake. Tukio la uvamizi wa Capitol Hill wiki jana ni matokeo ya kauli zake kwa wafuasi wake na wakafanya kweli sawsawa na maagizo ya kiongozi wao.

Sisi kumbe ni wavumilivu na waelewa sana.
Haiwezakani ghafla tu watanzania waanze kuwa na mapenzi na ccm,waliichukia tangu enzi za Mkapa,nini kitawafanya waipende sasa hv,enzi ya Dikteta uchwara,
Alizima mtandao wakati wa uchaguzi(na Mseven wa Uganda kafsnya hivyo).
Anafanya miradi ambayo haipo kwenye mipango ya nchi.
Hashauriki,
 
greenwoods

JF-Expert Member
Sep 21, 2020
268
250
Mbona hujamzungumzia yule mabaga fresh aliyewahimiza wafuasi wake waandamane na kisha wakamtolea nje,yeye naye anakuwa ni kiongozi wa aina gani?
 
Bulesi

JF-Expert Member
May 14, 2008
8,980
2,000
Hatuna UVUMILIVU wowote zaidi UJINGA na UONGA WA KIKE basi.

Magufuli is running the country like a Mafia Don!! He demands total loyalty to his appointees and makes sure that whatever he decides is implemented irrespective of any implications!! Magufuli has also completely subordinated the Judiciary and the legislature, something that Trump failed to do during his four year tenure as POTUS ! Will Magufuli end the Trump way or may be worse; only time will tell!
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,879
2,000
Uimara wa taasisi ni watu au raia imara.
Watu wa hovyo huzaa taasisi za hovyo na mwisho taifa la hivyo.
Kujenga taifa imara, tunatakiwa kuwa na watu imara kifikra na siyo magoigoi.
Kufurahia raia wasiohoji kwa kigezo cha uzalendo uchwara ni upumbavu uliopitiliza.
Kuwa na raia wanaohoji ni jambo moja la msingi, lakini kuwa na taasisi imara zilizo huru zitachochea mabadiliko ya haraka zaidi kwa yale maoni ya raia kufanyiwa kazi upesi, lakini kama taasisi zilizopo ni dhaifu maoni ya raia yatabaki mitandaoni tu hayatafanyiwa kazi physically.

Mfano: Hapa kwetu raia akitaka mabadiliko kwa mbinu za maandamano baada ya kuona njia nyingine hazifanyi kazi kwa haraka, (kutaka Tume Huru ya uchaguzi).

Mambosasa ataibuka awaambie raia mkiingia barabarani nitawavunja miguu, hapa tatizo utaona sio raia, tatizo ni udhaifu wa taasisi yetu ya jeshi la polisi kushikiwa akili na chama tawala.

Marekani huu ujinga huwezi kuuona, tumeona afisa wa polisi akimgomea Trump kuwapiga waandamanaji kisa wanampinga, lakini pia tumeona yule mama Spika, Nancy Pelosi, nae akiendesha mijadala bungeni iliyosababisha hali ya Trump izidi kuwa mbaya zaidi kisiasa.

Na kuonesha jamaa wanavyojielewa, Pelosi juzi ameshinda tena kuendelea kuwa Spika wa bunge la Marekani wakati Trump ndio kwaheri.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom