Kumbe Wanufaika wa CCM ni pamoja na Watendaji wa Serikali WEZI

apolycaripto

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
644
225
Nakumbuka kauli ya Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Cleophas David Msuya kuwa "Majengo ya kifahari yaliyotapakaa baadhi ya maeneo kama vile tegeta,boko,kunduchi,mbezi na Bunju B" ni ya Watumishi wa Umma. Hawa ni wanufaika na mfumo uliopo wa kifisadi hivyo kamwe hawatapenda kuona CCM ikitoka madarakani mpaka "damu imwagike". Leo hii ata kazi ya Jeshi "inalipa" na watu wa fani hii wanaishi kwenye makasiri kama wafanya biashara maarufu. Nilipata fursa ya kumtembelea jamaa yangu mmoja "Mpiganaji" mwenye cheo cha Ukanali, mazee kwenye yard tu full vigae na urefu wa Ikulu na gari za kuchagua ipi ya kupanda. Nikajiuliza je! wale walio juu yake wako vipi?.Maongezi yake kwa sehemu kubwa yalitawaliwa na maneno "Kikwete Mzuri" ,hakuna chama kama CCM. Wakati nashangaa shangaa mahala pale Boko nikakutana na mjengo mwingine wa "kutisha" huku gari ya Serikali ikinipita na kufuatana na ya kiraia.

Baadae nilikuja kubaini ni Mkurugenzi wa Manispaa moja hapa jijini, bahati nzuri Shamba boy alinishtukia mshangao wangu na mimi nikampotezea kwa kumwambia natafuta plot na mimi ni Mtumishi wa Serikali, huku nitaweza kweli? maake ni maorofa yameota tu. Shamba Boy kwa kunishangaa akaniambia wengi wenye makasiri hayo ni watumishi wa Serikali akiwemo aliyenipita muda si mrefu, kunimaliza zaidi akanionyesha njia panda kuwa umeona jengo la orofa 2 linaelekea kukamilika? nikamjibu ndio, akaniambia ni mali ya Mkurugenzi huyu. Ili kunimaliza kabisa akaniambi nyumba anazo nyingi na juzi amekula viwanja vitatu Mabwepande.

Jamani huu ni mfano mdogo tu wa Watanzania walioonja pepo.Hivi kweli Mkurugenzi huyu mbali na huyo Mpiganaji maisha haya wanayatoa wapi?.Sikatai kujikwamua katika "umasikini" lakini mbona mimi mbali na kusoma kwangu mpaka level ya uzamili tena fani ya Fedha mbona bado life linanigonga kichizi?.Hivi ndani ya Serikali kuna mishahara ya siri mbali na TGS-A,B,C,D,G,H ambayo hatuijui? ata kama ni safari za kikazi hapa kuna jambo. Kwa level yao (hasa Wakurugenzi) ni TGS I lakini haiendani na mali wanazomiliki.

Watumishi wa Serikali wa aina hii wapo wengi na uwekezaji wao ni wa kutisha kwani anayeiba Mwanza anaporomosha Dar es Salaam na aliyepo Bongo anawahi Mwanza. Kweli ujanja "kupata" na kamwe watu hawa hawatopenda kuona mabadiliko ambayo yatahitaji watueleze pesa hizo wametoa wapi.

Wazee nimeandika hivi si kwa "wivu" kama wanavyopenda kusema vijana wa "familia bora" waliomo humu. Haya nimeyashuhudia kwa macho yangu na kuamini kuwa ''KUMBE WANUFAIKA WA CCM NI PAMOJA NA WATENDAJI WA SERIKALI WEZI''.Angalau kusema nayo ni dawa, ngoja nivute kipande changu cha "muhogo" na "nguru" nitulize fikra niangalie kesho patafikaje.
 
Watumishi wanufaika na mfumo wa kifisadi ni wachache sana, tuliowengi jua linatuwakia ile mbaya!kawaulize makoplo majeshini na walimu!
 
Back
Top Bottom