Kumbe Wanasheria wetu wana nafasi kubwa ya kubadilisha ustawi wa Taifa hili

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Kwa nchi zilizoendelea wanasheria ni huduma iliyo wazi na yeyote mwenye madai huwa hasiti kuitumia pale anapoihitaji. Mwanasheria ni mtu anayependa kushinda kesi kubwa. Hii inamuongezea credit. Ni sawa na Jaji anavyopenda kutoa maamuzi kwenye kesi kubwa.

Screenshot_2019-09-01-19-58-19-1.png


Kuna vilio na malalamiko mengi yanayosikia kutoka kila pembe ya nchi ambayo kwa sababu ambazo tumekuja kuzielewa ni vilio ambavyo vimeshindwa kujibiwa na mamlaka zinazohusika ikiwemo hata chombo chao cha uwakilishi yaani Bunge.

Sisi kukimbilia kwa mwanasheria bado ni jambo ambalo wengi tunasita kulifanya hata pale tunapokuwa tumeumizwa sana.

Niliwahi kusema dawa ya mitandao ya simu inayokiuka usiri wa wateja wake hadi kufikia kuhatarisha usalama wa wateja ni kuyashitaki makampuni haya pamoja na makampuni yao mama katika mahakama za huko nje.

Haya makampuni ambayo yapo kwenye stock exchange markets huko nje yataacha ujinga mara moja. Nilisikia namba ya simu ya Ben Saanane imegawiwa kwa mtu mwingine, can you imagine that?

Hata mikataba tunayoambiwa ni siri mfano ya madini, tungepata wanasheria wasio na woga na walio wafuatiliaji na wenye uelewa tungejua kila kitu. Ni suala la kuyabana haya makampuni huko huko nje katika mahakama zao. Kuna hela nyingi sana za nchi hii zinapotea kwa wizi au uzembe na hakuna anayewajibishwa.

Ni kwamba hatujawa tu na wanasheria machachari wenye kusaka watu wenye madai, huko nje wanawaita 'ambulance chasers'.

unnamed (3).jpg


Malalamiko ya wakulima (mfano wa korosho na pamba), wafanyakazi (malimbikizo ya nyongeza za mishahara), wafanyabiashara, watu waliowahi kutekwa, kupotea au kudhuriwa na watu wasiojulikana yanaweza kupatiwa ufumbuzi katika mahakama za nje.

Kibaya zaidi sheria zetu zinawabana wanasheria. Nasikia hawaruhusiwi hata kujitangaza. Sijui sheria kama hiyo imewekwa kwa faida ya nini ukizingatia mahitaji mengi ya kisheria tuliyonazo.

Kiufupi, mambo ya hewala yamepitwa na wakati, kila mtu apiganie chake kwa nguvu zake zote.

Niliwahi kuleta mada nyingine ikizungumzia umuhimu wa wanasheria, wafanyabiashara na wasanii katika mabadiliko ya kisiasa.
https://www.jamiiforums.com/threads/nguzo-tatu-tishio-kwa-ccm.1496283/
 
Back
Top Bottom