Kumbe wanaomchonganisha Rais na wananchi ni watendaji wa ngazi za mikoa na wilaya.

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,344
Katika kipindi cha chini ya miezi miwili mheshimiwa Rais ameshuhudia kwa macho yake jinsi wateule wake wanavyomchonganisha ama na wananchi ama na viongozi wa vyama vya upinzani katika ngazi za mikoa na wilaya.

Bila shaka katika sherehe za ufunguzi wa daraja la mwalimu Nyerere Kigamboni mheshimiwa Rais aligundua jinsi watendaji wake wanavyofanya kazi kwa visasi na roho mbaya pale walipoacha kuwaalika bw Ramadhan Dau aliyekuwa mtu muhimu katika ujenzi wa daraja hilo pamoja na mstahiki meya wa jiji la Dar es Salaam.

Katika ufunguzi wa leo wa mpango wa polisi kuboresha usalama wa jamii na mali zao, Leo kama ilivyokuwa kwa Dau, Rais ametumia zaidi ya dakika tatu akimtafuta na kumwita meya wa wilaya ya Kinondoni bila mafanikio, hii inatosha kuwa indiketa tosha kwa mheshimiwa Rais kwamba watendaji wake wanamchonganisha.

Kibaya zaidi wale waliofanya upuuzi wa kutomwalika meya hawakujishughulisha hata kumweleza ukweli Rais kwamba hayupo kwa sababu hawakumwalika, badala yake wamebunda tu nadhani ili aonekane ni mjivuni na mwenye dharau.

Tunaomba vitendo hivi vya kipuuzi viepukwe na tujenge tabia ya kuwapa ushirikiano viongozi wa watu bila ya kujali wanatoka vyama gani.
 
Back
Top Bottom