Kumbe wale wanaotaka order ya kiti moto kilo 1.5 na ugali huwa wanapanua utumbo tu

Hii ni kweli, kula sana sio afya.

Binafsi nilishawahi kaa siku nne nakunywa chai kavu na maji mengi.

Maji ni muhimu sana.
hii n kawaida sana, fatilia akina mama walokole.... wanafunga wanakunywa maji tu na juis kidogo kwa siku 21 na kazin bado wanaenda wanapiga kazi kama wanakula vile
 

Huyu Mzee mwaka 1550 alijiona anachoka sana, Aliangalia chakula anachokula na kukipunguza kufikia 350g na 414 mls za wine kwa siku.

Kwa hesabu za haraka haraka alikula yai moja asubuhi kama kifungua kinywa.

Kipande cha nyama, kuku au samaki saa kumi jioni kikiwa na kiazi na mboga. Ukubwa wa kopo la Coca Cola aliweka wine. Maji ni muhimu hapa kati kati.

Tunakula vyakula vingi tusivyo vihitaji. Wakati wa WWII, wanajeshi wa Magharibi waliotekwa Japan walilishwa kibakuli cha wali na kipande cha nyama kila baada ya masaa 24. Wengi waliishi mpaka kurudi makwao wakiwa wamekonda sana.

Iliwachukua zaidi ya mwezi kuzoea milo mitatu kwa siku.
Nadhani kwakuwa msosi wa siku hizi una kemikali za kutosha hata ukijibana unakula sumu,
Nina wazee wangu wamevuta tumbaku Ile ya kunyonga mwenyewe ,wameishi umri mrefu wa kutosha kuwaacha watoto na wajukuu na vitukuu
 
Watanzania wengi wanakula hovyo sana.
Unaweza kukuta watu wawili wanakula kilo moja ya kitimoto, ndizi nne na pepsi au bia kwa mlo mmoja!
 
Ndio maana tatizo la kiribatumbo linazidi kuongezeka kila siku Africa. Zamani Waafrika hawakuwa wanakula kama wengi wanavyokula sasa hivi mikate meupe, ugali sembe, wali, vitumbua, maandazi, masoda, bia n.k. Lishe mbovu ni janga haswa nchi wakati wetu, na kwa kiasi kikubwa inachangiwa na ukosefu wa maarifa ya mlo bora.
Kulaaa msosi wa kiafrika.

Tena kula vizuri tu vyakula vya asili. Si lazima tufate wazungu. Piga ugali mchicha pilipili mixer maharage na shushia na maji kisha kafanye kazi.

Kama huna kazi ngumu chukua mkeo mshughulikie mpaka atake kukurudishia mahari akulipie yeye.

TUSIENDEKEZE SANA UZUNGU SISI NI WASWAHILI.
 
Huu utopolo umenishinda. Hata nikila nusu yai kwa siku nzima bado nitakufa tu. Nimeona wengi waliofanya diet wametangulia mimi ninayekula kitimoto kilo moja na nusu nipo nadunda tu
 
Back
Top Bottom