mtoto wa mchungaji
JF-Expert Member
- Oct 24, 2020
- 279
- 480
Kuna vitu hapo awali nilikuwa sielewi kabisa, kuna wakati wanasiasa halisia walikuwa wanakosea kabisa na hata mtoto ukimuuliza anakwambia kuwa hilo ni kosa lakini wanasiasa wa mtandao walikuwa wanalipongeza sana.
Wakati mwingine uliweza kuona hali ya siasa za upinzani zinapita katika shida na kipindi kigumu mno, lakini hawa wanasiasa wa mitandao wanasema hali ni nzuri na tunachukua nchi mapema asubuhi.
Kuna kipindi nakumbuka hali ilikuwa mbaya sana ktk upinzani watanzania wote walikuwa wanajua uwe CCM au upinzani, unaona kabisa hapa ni kama wamewekewa goti shingoni kama Joji Floidi lakini ukiingia katika wanasisa wa mitandao wanasema chama kinaimarika kwa kasi ya ajabu.
Angalia leo katika uhalisia wa siasa halisi Tanzania upinzani ni kama haupo kwani nchi nzima kati ya wabunge zaidi ya 300 wa kuchaguliwa wapinzani wamepata wabunge ambao hawazidi 3.
Kinachonishangaza mimi huku kwa wanasiasa wa mtandao ukiangalia wanavyoandika ni kama CCM ina wabunge 3 na wapinzani wana wabunge zaidi ya 300.
Jamani hivi hii imekaaje? Mimi naona kama kuna tatizo. Mimi nasema kama kuna components nyingine zilizosababisha kuua upinzani basi hii ya taarifa za kupotosha zitakuwa zimechangia sana kuua upinzani Tanzania kwasababu watu wa siasa za mtandao ni kama vile hali ya mgonjwa ni mbaya anakaribia kufa wenyewe wanasema mgonjwa afya yake inazidi kuimarika kwa kasi ghafla tunasikia mgonjwa kafa.
Je, kulikuwa na mahusiano ya moja kwa moja kati ya wanasiasa wa halisia na hawa wa mitandaoni au ni makundi mawili tofauti kwasababu inashangaza.
Hebu nisaidieni mimi mkusanya sadaka sielewi kitu hapo.
Mtoto wa mchungaji.