Kumbe wajumbe wa nyumba kumi hawamo katika serikali ya mitaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe wajumbe wa nyumba kumi hawamo katika serikali ya mitaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Fredrick Sanga, Jan 20, 2012.

 1. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nikijiuliza, hivi ni kwanini wajumbe wa nyumba kumi hawamo katika muundo wa utawala wa serikali lakini wanajifanya kama wanatawala wananchi wote. Hata serikali za mtaa hutaka utambulisho kutoka kwao. Hivi hawa huchaguliwa na wanachma wa CCM au na vyama vingine. Hapa nahisi kuna changa la macho. Tusilisahau hili katika katiba mpya, liwe bayana

  Samahani kwa kuwaudhi.:hatari:
   
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  He - kumbe!

  Mimi nilifikiri wako chini ya Mtendaji wa mtaa na nilidhani wanalipwa mshahara na serikali.
   
 3. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Wajumbe wa nyumba kumi ni organization ya chini ndani ya CCM, haipo katika uongozi wa serikali. Ngazi ya chini katika uongozi wa serikali ni Mtaa ambapo kuna Mwenyekiti wa mtaa na Katibu wa mtaa pamoja na kamazti zake.
   
 4. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Wengi wao bado wana dhana ya chama kushika hatamu zote za uongozi. Miongoni mwa vitu ambavyo watu walikuwa hawajui ni pamoja na hawa jamaa kuwa siyo watumishi wa umma.

  Ukienda vijijini bado wana power na wanasikilizwa na wamekuwa ni watatuzi sana wa migogoro ya kijamii kwenye level ya kaya, labda iwe changamoto wabadilishwe ile iwe ni sehemu ya muundo wa utawala.
   
 5. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hawa mabalozi ndo nguzo ya uhai wa ccm. Ukitoka kwa Rais ktk ranking mtu chini kabisa ni mjumbe wa serikali ya mtaa\ vijjiji, kwa mjini na vijijini ( usisahau wenyeviti wa vitongoji kwa vijijini.
  Viongozi wa vijiji na mitaa wanamalekezo yasiyorasmi toka serikali ccm ya kuwatumia hawa jamaa ili kuwapa nguvu.
  Hawa ndo sasa hivi watakuwa watu muhimu huko Arumeru wakati wa uchaguzi kwa upande wa ccm.
  Hapa Dsm Chadema tumeshaanza kuwaweka na sisi mabalozi wetu ili tubanane vizuri 2015.
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  alaaaaa kumbe????

  mjumbe wangu alikuwa ananiletea za kuleta acha nikamuanzishie leo (joke)
   
 7. P

  Ppkanjibhai Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono , hilo ni jambo la msingi sana na si kwa DSM tu pekeyake bali iwe kwa TZ nzima na level zote hadi vijijini, la sivyo basi ipiganiwe iingizwe kwenye katiba mpya ili uongoziuanzie chini na uwakilishi wao uwe wa kupigiwa kura kama viongozi wengine. Hili la cell leaders ni la msingi sana kwani uongozi utaanza level ya chini kabisa.
   
 8. d

  daniel paul Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  barozi sio kiongozi wa serikali bali ni mwakilishi wa chama chochote katika kila nyumba kumi. hivyo basi usishangae kusikia hapo mtaani kwenu kuna barozi wa ccm chadema, nccr, udp na wengineo . na pia kumbuka kuwa barozi anachaguliwa na wanachama wa chama husika tu. lakini ukienda polisi hasa huko vijijini utasikia polisi anakuuliza je umepita kwa barozi ? sasa sijui anataka nije na barua ya barozi yupi wa ccm au wa chama changu.? ndio sababu kwa barozi hakuna bendera ya taifa bali ipo bendera ya chama husika tu.toa elimu zaidi kwa wasio jua hili. ebu chadema nasi tuweke mabarozi kila nyumba kumi uone tutakavyoshinda chaguzi kwa kishindo . [asante niko tayari kukosolewa na kama kuna kasoro ktk maelezo yangu]
   
 9. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,826
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  Mr. Aweda umechukua nafasi ya regia hapa jf?
   
 10. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Mi sireport kwa balozi wa nyumba kumi ambaye ni mwakilishi wa sisiem, ambaye hata mke na mme wakigombana eti wanaenda kwa balozi kusuluhishwa! sisiem ukitaka kura za wananchi ndo inakumbuka kuwapelekea chumvi na khanga za india, huku ikiwahadaa kwa kuwapa jina lenye hadhi kuuubwaaa. Mi namtambua kiongozi wangu wa msingi wa chadema na nikipata nyumba mtaa ambao ni wa magamba siendi jitambulisha namtafuta huyo wa kionngozi wa msingi hata kama atakuwa yuko 500mt.
   
 11. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Tupeni maujuzi zaid.
   
 12. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  we muuza sura acha kupotosha watu. mimi balozi wangu wala si mwanachama wa ccm. na ninawajua mabalozi wengi tu na wala hawajitambulishi kwa vyama vyao. You always speak and write nasty. unapoingia kwa jina lako halisi better you write the reality kuliko hizi pumba zako.
   
 13. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  :hat:
  Sasa hapa hawa mabalozi kumbe waliachwa makusudi ndani ya CCM kudhoofisha upinzani. Kama ndivyo hii ni hatari kwa usalama wa nchi, kwani wanafanya kazi za serikali. Hili liende bungeni kama suala la dharuala tena ni janga la taifa. Waache kufanya kazi za serikali. Mfano ukiingia kwenye ulingo wake unatakiwa ujitambulishe kwake.
   
 14. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,443
  Likes Received: 4,727
  Trophy Points: 280
  Hii ni chini ya Ibara ya 10 ya Katiba ambayo kabla ya mfumo wa Vyama vingi ilikua inatoa nafasi na mamlaka ya madaraka kichama, Ibara hii ilifutwa na ujio wa sheria ya Vyama vingi ya mwaka 1992, someni vizuri hii ibara
  na tujitahidi kuwaelimisha wananchi si tu wa vijijini hata mjini wanaopewa reference kwa wajumbe............
  ,
   
 15. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Cha kusikitisha hawa wajumbe hawajaelimiswa, na kama hiyo ibara ipo basi wana jinai nyingi. Tena jiani zevuka kwa idara nyingi.
   
 16. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  :lol:Wajumbe wa nyumba kumi kuweni macho na hili.
   
 17. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Je, ndugu naomba tufahamishane hivi huko mtaani kwenu mnapotaka kufanya uchaguzi wa Balozi wa 10 nyumbas

  (a) mnakuwa na kura za maoni.
  (b) Uchaguzi unashirikisha vyama vingi.
  (c) Mwaka gani hapo mtaani kwenu mlifanya uchaguzi wa balozi wa 10 nyumbas mara ya mwisho.

  ANGALIZO: HAPA TUNATOA MAONI NA SIYO KUTUKANA / MANENO MAZITO.

  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!!
   
 18. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nimekusoma, yaani umefafanua vizuri sana, hapa atakayejibu hili atatusaidia sana. Hili ni suala la dharula, maana hawa wajumbe wanafanya jiai bila kujua.
   
 19. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kuna wanachama wa chama fulani hawakupata chandarua kwa sababu ya wajumbe kuruka nyumba zao katika kutoa taarifa.
   
Loading...